google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Mtanzania Akamatwa Akishukiwa Kuhusika na Shambulizi la Al Shabaab Lilioua Watu 147 Kenya | UDAKU SPECIAL

Mtanzania Akamatwa Akishukiwa Kuhusika na Shambulizi la Al Shabaab Lilioua Watu 147 Kenya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mtanzania mmoja ambaye hajafahamika amekamatwa kuhusiana na shambulio la kigaidi katika Chuo Kikuu cha Garissa, Kenya.

 

Taarifa zilizopatikana jana usiku na kutangazwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), zilieleza kuwa Mtanzania huyo anahojiwa kuwapo kwake katika eneo hilo hasa ikizingatiwa kwamba siyo mwanafunzi wala mtumishi katika chuo hicho.

 

Taarifa hizo zinasema kuwa Mtanzania huyo ni miongoni mwa watu wanne waliokuwa wamejificha  katika mabweni ya chuo hicho na kati yao, wawili walibainika kuwa ni wanafunzi.

 

Hata hivyo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba alipoulizwa jana kuhusu Mtanzania huyo, alisema atatoa taarifa rasmi kwa taratibu za jeshi hilo.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad