Mtoto wa Mwisho wa Rais Kikwete Ataka Ubunge B’moyo, Atamba ana Uwezo wa Kuongoza

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Makada wawili wa CCM wilayani Bagamoyo,  wameonyesha nia ya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha ubunge katika jimbo hilo kupambana na mbunge wa sasa, Dk Shukuru Kawambwa.

Makada hao ni Mwenyekiti wa CCM kata ya Dunda, Yusufu Mrisho Kikwete ambaye ni kitinda mimba wa familia ya Rais Jakaya Kikwete na Abdursharrif Zahoro ambaye  ni mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi  CCM wilayani humo.

Wakati  makada hao wakitangaza nia hiyo  juzi, tayari  mbunge wa jimbo hilo Dk Shukuru Kawambwa  alikwisha tangaza nia ya kutaka kutetea nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Naye Yusuph Kikwete alisema  ana matumaini makubwa ya kushinda kwa kuwa, amekuwa akiungwa mkono na makundi mbalimbali, wakiwamo vijana ambao wamekuwa wakimshawishi kugombea nafasi hiyo.

 “Ni kweli kuna makundi mengi, yamekuwa yakinishawishi kuingia katika kinyang’anyiro na baada ya kutafakari sana na kujipima kama ilivyo kwa wanasiasa wengine, nimeona siwezi kukataa ushawishi huo, maana kuna watu wameona uwezo wangu  wa kiuongozi,” alisema.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad