google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Mwigizaji Jack Wolper Ashutumiwa Kumsahau Aliyemtoa Kisanii Katika Tasnia ya Filamu Bongo | UDAKU SPECIAL

Mwigizaji Jack Wolper Ashutumiwa Kumsahau Aliyemtoa Kisanii Katika Tasnia ya Filamu Bongo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ubuyu Mpya Kutoka Instagram kwenye page ya mrekebishatabia kuhusu Mrembo Mwigizaji Wolper Kumsahau aliyemwingiza katika Tasnia ya Filamu:

'HISTORIA: Je unajua aliyemtoa kisanii Jackline Wolper mpaka kupata umaarufu nchini ni nani? Ni mdada mkali wa wa siku nyingi kwenye masuala ya sana Lucy Komba ambaye hivi sasa anaishi na familia yake nchini Denmark.

Alikutana nae kwenye ofisi moja bongo akamuomba namba ya simu walipoachana baada ya kama dk 10 akamuandikia msg anaomba amsaidie kwenye sanaa awe kama yeye @iam_lucykomba , Jackline alikuwa na saloon ya nywele kipindi hiko baadae saluni ya Jackline Wolper ilifungwa sababu ya kushindwa kulipa kodi, ikafikia hatua akauza gari yake na akaanza kutumia gari ya Lucy Komba... anam-drive Lucy kazini anatumia gari jioni anarudi kumfuata kazini... mambo yakawa magumu kwa Jackie mpaka akauza vitu vya saluni, wakati huo ndo Lucy kwa bidii anamfundisha jinsi ya kuigiza...mpaka baba watoto wa Lucy akawa anamuonea huruma Lucy kumtaka apate muda apumzike!! Haikuishia hapo Lucy akamuunganisha kwenye filamu akawa anaharibu wadau wanamlaumu Lucy kuwa Jackie atoke maana hajui lakini akamtetea na kuendelea kumfundisha mpaka akacheza vizuri.

Filamu za Lucy mbili ya kwanza ilikuwa inaitwa AMA ZAKO AMA ZANGU ya pili KIPENZI CHANGU  baada ya hapo Irene Uwoya akampigia simu Lucy kumuuliza kama ana mtu anataka kufanana naye. Lucy akampigia Jackline na kumwambia akaonane nae na Kanumba na Ray wakaridhia ndo wakamchezesha ile scene ya Ophra baada ya hapo akaanza kudai Ray ndo amemtoa kwenye sanaa kwa ile scene moja aliyocheza.

Lakini baada ya watu kumponda ndo akabadilika na kusema Lucy ndo kamtoa na mpaka leo ndo kisa cha watu kumfahamu Jackline Wolper.... kuumbe Lucy ndo kakufikisha hapo @wolperstylish?? Kila mmoja ana mahali alianzia lkn jaribu kukumbuka Wema hata kama ni kidogo...Halafu jinsi alivyo hata harusi yake hukuudhuria ukaishia kuiponda!! Watu hawakumbuki walikotoka aisee' 

~Mrekebisha tabia
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. DAH BINADAMU WATU WA AJABU SANA TENDA WEMA UENDE ZAKO, HAKIKA WEMA HAUOZI NI AKIBA YAKO YA KESHO.MM PENDA SANA WW LUCY MMWAAAAAAAAAAAAA

    ReplyDelete

Top Post Ad