Picha Zikionyesha Hali Ilivyokuwa Nyumbani Kwa Gwajima Leo Baada Ya Kuzingirwa Na Jeshi La Polis

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Askari wakiwa nyumbani kwa Gwajima.
  
Makamanda wa polisi wakiwa tayari kwa lolote.
  
Gari lililombeba Gwajima likitoka ndani ya nyumba yake kuelekea kituo kikuu cha polisi kwa ajili ya mahojiano.

Mawakili wa Gwajima wakisalimiana na mmoja wa maofisa wa polisi mara baada ya kufika eneo la tukio.
  
Waandishi wa habari wakiwa eneo la tukio.

Waumini wa Gwajima wakiwa wamezunguka nyumba wa askofu wao.
  
Kundi la wafuasi wa Gwajima wakifika nyumbani kwake mara baada ya polisi kuondoka eneo la tukio.
  
Baadhi ya watu waliokuwemo ndani ya nyumba ya Gwajima wakichungulia dirishani.
 
****
Wakati  taarifa zikisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya jamii kuwa nyumba ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, imezingirwa na polisi, habari kamili ni kwamba zoezi la kumkamata askofu huyo lilishindikana baada ya kugoma kufungua geti lake.
 
Polisi hao waliokuwa na silaha walifika nyumbani kwa askofu huyo maeneo ya Salasala jijini Dar wakiwa kwenye magari zaidi ya manne ambapo walipiga kambi katika eneo hilo kwa saa sita huku njia hiyo ikiwa imefungwa kwa saa kadhaa kabla ya waandishi wa habari na baadhi ya waumini wa askofu huyo kuruhusiwa kupita.
 
Hata hivyo baada ya polisi hao kuzungumza na mawakili wa Gwajima na viongozi kadhaa wa kanisa hilo, waliamua kuondoka huku wakitoa amri kiongozi huyo afike kituo kikuu cha polisi  kwa ajili ya mahojiano zaidi ambapo alifika na baadaye kufikishwa katika Mahakama ya Kisutu ambapo alisomewa  mashitaka  mawili  ya  kutoa lugha ya matusi na kushindwa kutunza silaha.
  
Askofu  huyo  ameachiwa  kwa  dhamana  na  kesi  yake  itaendelea  Mei 4  mwaka  huu.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Du bonge la jumba huyu ni mtanzania mwenzetu raia tu wa kawaida

    ReplyDelete
  2. ANAISHI KAMA MFALME

    ReplyDelete
  3. na nyie pambaneni muwe na mijengo ya maana sio unafki kwa staili hiyo umaskini hautaisha

    ReplyDelete
  4. KHAA MIYE SISHANGAI MJENGO MAANA MBONA IKO MINGI TENA ZAIDI YA HUO????????NINACHOSHANGAA NI POLISI KUTUMIA NGUVU KUBWA NA SILAHA NZITO ZA MOTO ??????????NGUVU KAMA HII INGETUMIKA KUSAKA MAJAMBAZI WANAOVAMIA VITUO VYAO NA WAUAJI WA ALBINO NA WAZEE KWENYE MACHO MEKUNDU KWA AJILI YA MOSHI WA KUNI ZA MAVI YA NGOMBE

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha ushamba wewe hapo polisi tulitumia nguvu gani mbona hatukuvunja mlango na kuingia ndani kumkamata huyo tapeli wenu?Sisi tuliketi outside tukimsubiri atoke twende naye lakini hakutii amri ya jeshi la polisi hivyo tukaamua kuondoka baadaye mwenyewe kajileta polisi.Acheni ushabiki wa kijinga nyie ndio mnaopenda kutoa comment za kuchochoe matukio yasiyopo,poor you!

      Delete
    2. WEWE NDO MSHAMBA HAYA MASILAHA YOTE YA NINI?? INA MAANA HUYAONI?? HAPO NIMECHOCHEA NINI? UKWELI UNAUMA SIO???MABOMU NA SILAHA NZITO ZA MOTO ZA NINI??? KWA AJILI YA LUGHA CHAFU TU?? ONENI AIBU BASI. KATAFUTENI WAUWAJI WA MAALIBINO NA VIKONGWE NA WALE WALIOPORA SILAHA NA KUUWA ASKARI VITUO VYA POLISI.AIBU YAKO!!!!!!!!

      Delete
  5. KWELI MSHIKAJI MAGUVU MENGI KUMKAMATA MCHUNGAJI WAKATI VITUO VYAO VINAVAMIWA NA MAJAMBAZI WENYE MAPANGA TU.

    ReplyDelete
  6. HAWA MAASKARI WATZ NI WAJINGA SANA NAKUUNGA MKONO MDAU 10:28 AM

    ReplyDelete
  7. kamata muuza unga uyo

    ReplyDelete
  8. askari wa bongo kama M B W A

    ReplyDelete

Top Post Ad