Polisi Yazuia Wafuasi Wa Askofu Gwajima.....Vikosi vya Mbwa, Farasi,Magari sasa kila Kona.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jeshi  la  polisi  kanda  maalumu  ya  Dar  es  salaam  limesema  wafuasi  wa  Askofu  mkuu  wa  kanisa  la  ufufuo  na  uzima,Josephat  Gwajima  wasithubutu  kutia  mguu  eneo  atakalohojiwa  askofu  huyo.

Kauli  ya  jeshi  hilo  imekuja  siku  chache  baada  ya  Askofu  Gwajima  kuwataka  wafuasi  wake  kumsindikiza  leo  kituo  cha  polisi  kanda  maalumu  ya  Dar  es  salaam  ambako  anahitajika  ili  kuhojiwa.

 Msimamo huo  ulitolewa  jana  na  kamishna  wa  polisi  katika  kanda  hiyo, Suleiman  Kova  wakati  akizungumza  na  mtandao  huu  ambapo  alisisitiza  kuwa  anayehitajika  kufika  katika  kituo  hicho  ni  Gwajima  na  mwanasheria  wake.

Kamishna  Kova  alisema  ni  vema  wafuasi  hao  wakaendelea  na  kazi  zao  za  uzalishaji,kwani  kwenda  kituoni  hapo  bila  mwito  au  kukamatwa  ni  kosa.

Kova  alisema  eneo  hilo  haliruhusiwi  watu  kukusanyika, hivyo  kwa  usalama  wao ni  vyema  wakaendelea  na  shughuli  zao  na  kuliacha  jeshi  hilo  lifanye  mahojiano  na  Askofu huyo  wakiwa  huru.

"Napenda  kutumia  nafuasi  hii  kumuomba  Gwajima  awaambie  wafuasi  wake  hawahitajiki  kufika  eneo  hilo  kwani  anayehitajika  ni  yeye  na  mwanasheria  wake," alisema  Kova.

Kova  alisema  iwapo  kila  mtu  atafuata  taratibu  hakuna  nguvu  itakayotumika  kutoka  jeshi  la  polisi, lakini  endapo  watakiuka  hakuna  njia  mbadala  ambayo  inaweza  kutumika  zaidi  ya  kutumia  nguvu.

Kauli  ya  Kova  inakuja   kutokana  na  kauli  ya  Gwajima  aliyoitoa  wakati  wa  sikukuu  ya  pasaka  kuwataka  wafuasi  wake  kujitokeza  katika  kituo  hicho  wakati  atakapokwenda  kuhojiwa.

Gwajima  alisema  lengo  la  kuwataka  wafuasi  hao  kujitokeza  ni  ili  waweze  kujua  kila  kitu  kinachoendelea  katika  sakata  hilo  kwani  kuna  taarifa  ambazo  zimekuwa  zikizushwa  na  watu  kupitia  mitandao  mbalimbali.

Akizungumzia  hali  ya  usalama  katika  jiji  la  Dar, Kova  alisema  ni  shwari  na  kuahidi  kuwa  wanaendelea  na  oparesheni  ya  kukamata  wauza  dawa  za  kulevya, wahalifu  na  kulinda  maeneo  ya  fukwe.

Pia, alisema  wamejipanga  kukabiliana  na  vitendo  vya  kigaidi  ambapo  wanafanya  uchunguzi  kila  mahali  kwa  kutumia  vikosi  vya  mbwa, farasi,helkopta, magari, pikipiki  na  kutembea  kwa  miguu  katika  maeneo  yote  ya  jiji.

Toa Maoni yako Hapa Chini:
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wapewe kichapotu, kama mkusanyiko wa Waislam ulitawanya kwa bakora, itakuwaja Gwajima aachiwe? Ni kichapo tu yeye na wafuasiwake

    ReplyDelete

Top Post Ad