USHAURI Kwenda Kwa Dada WEMA SEPETU Baada ya Kusema Anatamani Sana Kupata Mtoto Lakini Hawezi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Dada yangu Wema,
Salamu sana, nyingi na za upendo mkubwa zikufikie. Pole nyingi sana, it is sad to listen to what your heart is speaking about the reality of your life. Kwanza, that is relieving kwako kwa kuusemea moyo wako na hali yako. Inakupa moyo huru na uliopumua pumzi kubwa, ni ujasiri wa pekee na kwa hilo nakupongeza. Nakupongeza pia kwa kuonyesha moyo wako, licha ya kwamba unaumia kwa mengi, moyo wako si uliovunjika na kupondeka, sio uliopoteza matumaini na mapendo ndani mwako. Hilo ni paji la Kimungu ndani mwako na umeonyesha hilo kwa kutomlaumu Mungu bali kwa kumtumainia.
Personally I was touched, and my prayers are with you. Don't give up hope and trust which are in you. Maisha na hali za ubinadamu vina mipaka yake. Tumeumbwa na tupo jinsi tulivyo, na kwa njia ya hali zetu makusudio ya Mungu ni ya kipekee kwa kila mtu, malengo yake Mungu tunaendelea kuyang'amua siku hadi siku na kwa nguvu ya ajabu. 
Mungu azidi kukutia nguvu katika yote, harakati za maisha ya kila siku zipate Baraka zake, na kwa njia hiyo ukitambua what He calls you to do. For surely you will be our dada and mama to many other children who need your love and care as of what God has given you just for the sake of them. 
Kila jema dada yangu, nakutakia moyo mkuu

By Anonymous
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Action nyingi mbona time alikuwa na diamond izo action zote hatukuona sasa hivi nini anakusudiya

    ReplyDelete
  2. Wewe wa wapi?hata alipokuwa na Diamond alikuwa anasema sema ishu ya motto ila tu hakuweza wazi kama hivi.

    Pole mdada jipe moyo,mimi pia sizai ila nina ishi kwa amani na mume wangu kipenzi.Huu ni mwaka wa kumi but hatujakata tamaa,
    Mungu akusaidie umpate mwenza muelewa.

    ReplyDelete
  3. Ugumba sio utasa usijalu Mungu yupo nakuombea mwaka usipite hujapata haja moyo wako

    ReplyDelete
  4. Haya ndo matatizo ya utoaji wa mimba mara kwa mara

    ReplyDelete
  5. pole sana. mimi ninamiaka 17 naishi na mume wangu na sijawahi kuzaa, hatujakataa tamaa. Kwa Mungu yote yanawezekana

    ReplyDelete
  6. Kwani hiyo ni ripoti kutoka kwa doctor au?na je vp kuhusu mimba ya diamond iliyohalibika na je katika maisha yake amewahi kutoa mimba ngapi?wema atuweke wazi sisi mashabiki wake sababu zilizosababisha aseme hana uwezo wa kuzaa

    ReplyDelete
  7. Nimelia nimelia nimelia Sanaa, I love this gal to death, she doesn't even know me but wateva is goin on ktk maisha take hurts me so much, I feel this bond with her, I adore her so much. I wish I could talk to her sometimes....zis dunia bana is so fake sometimes, mtu unaumia moyo hadi hutamani kuishi tens lol...kaza moyo, kaza buti fanya kazi wema wangu mi nakupendaaaaaa. Naumia jamniii

    ReplyDelete
  8. Wema ukishaolewa tu utashangaa na mimba utabeba na watoto utazaa. Kwanza ni ile amani utakayokuwa nayo, pili stress zinazokufanya usibebe mimba hazitakuwepo. Hivi kwa mfano na huyo Diamond ungezaa nae saa ngapi? Kutwa kiguu na njia, mwili hata haukuwa na nafasi ya kupoa. Kingine mwanaume yule alikuwa anakupa stress wee acha tu, kutwa unakimbizana nae barabarani, mara leo umemkuta na VK wa Kenya, mara sijui anatoka na binti gani, mara sijui huko Houston ana mwanamke gani, achilia mbali stress za sijui kina H Kimzazi sijui stress za team nani na nani hivi stress zote hizo unapataje mimba hasa?

    Halafu hata kwa CK pia ilikuwa sio rahisi kuzaa vile vile kutokana na stress, unazaaje kwanza na mtu huna uhakika na future yenu? Wanawake wengine hawawezi kushika mimba kwenye mazingira ya aina hiyo, wanahitaji utulivu wa nafsi, kitu ambacho hujapata bado.

    Kwa hiyo kwanza pata utulivu kwa kuolewa, kisha utaona nafsi yao itakavyochanua na tumbo lako la uzazi litakavyofunguka, InshaAllah utapata watoto kadri Mungu atakavyokujaalia.

    Na nyie Mashankupe na Magumegume yaliyowashinda mitume mnavyomkazania mwenzenu azae azae, yaani anazaaje sasa? Mwanamke ana mbegu za uzazi mpaka azae? Yeye ana mayai tu ambayo kila mwezi yanapevuka na yakikosa mbegu ndio anapata siku zake. Sasa hizo mbegu mnataka akazinunue dukani kisha azimeze mdomoni? Au kila relationship mnataka azae mtoto? Mfyuuu nyio ndio design watoto 3 kila mtoto na babaake. Mwacheni mwenzenu apate mume ndio mna haki ya kumuuliza mbona hujamzalia mumeo watoto. Halafu msisahau pia watoto wanatoka kwa Mungu, humpa amtakae na humyima amtakae. Kama wewe kakupa usijisahau hiyo ni amana tu akitaka anaweza kuwachukua watoto wote aliokupa na wala huwezi kumzuia. Kwa hiyo komeni kuwaita watu ambao hajapewa watoto na Mungu kuwa ni Wagumba, tena nyie ndio mnakondesha wake za kaka zenu kwa gubu na masimango kisa hawajazaa wanawajazia choo. Sasa sijui huyu Wema huwa mnamlisha nyinyi mpaka mumng'ang'anize azae?

    ReplyDelete
  9. Haya mateam wanayoyaendekeza atalia Sana atatukanwa kila siku kuhusu kutokuzaa,Kuna siku nilimsikia kwenye kipindi chake anamsifia dougiemasta,huyo Dougie mwenyewe anatukana watu Kama nini unafikiria hao wanaotukanwa mashabiki zao watamuacha? Hawa mastar waache ujinga wa mateam hiyo ndiyo gharama yake pole Sana WEMA!

    ReplyDelete
  10. trust me unaweza kupata mtoto only if you mean it Dada Wemae

    ReplyDelete
  11. Na wadada wa kibongo wanajua kunyanyapa,mwenyewe walininyanyapa mpaka nilipokuja marekani niliweza fanyiwa fertile mungu amesaidia nina mtoto,njoo Huku marekani si una ndugu mdogo wangu.

    ReplyDelete
  12. Watoto wote uliopangiwa kuzaa na Allah umewatia chooni sasa huta wapata hapa duniani lakini huko kwenye malipo watakuja na watakuuliza mama kwanini ulituuwa? anza kutubia sio kuendelea kutafuta kuwepo kwenye magazine

    ReplyDelete

Top Post Ad