Wanachama wa Chama Kipya Cha ACT- Tanzania Wapigwa Marufuku Kushabikia UKAWA'

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Chama cha ACT-Wazalendo kimesema kila mwanachama anapaswa kuwaunga mkono wagombea watakaopitishwa na chama hicho katika nafasi mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu ujao, kwani kinyume chake ni kukisaliti na adhabu yake ni kufukuzwa.

Mwenyekiti wa chama hicho, Anna Mghwira alisema mwishoni mwa juma kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu, chama hicho kinahitaji nguvu za pamoja.

“Sisi bado hatujajiunga na Ukawa, hivyo wanachama wetu wanapaswa kulitambua hilo na kuepuka kushiriki kwenye ushawishi wa kufanya kampeni za wagombea wa vyama vingine. Hata kwenye katiba yetu tunasema sasa tunalenga zaidi katika kujiimarisha ili kutoa ushindani mzuri wa kisiasa katika uchaguzi huu,” alisema.

Katiba ya ACT, imeeleza wazi kuwa pamoja na sababu nyingine na kwa mujibu wa kanuni zitakazotungwa na Halmashauri Kuu, mwanachama yeyote ambaye atasaidia kushawishi, kujiunga, kutoa tamko la kuunga mkono chama kingine au mgombea wakati chama kimeweka mgombea wake kwa mujibu wa sheria za nchi, atakuwa amepoteza uanachama wake.

ACT- Wazalendo tayari imetoa ilani yake ya uchaguzi ikionyesha kwamba iwapo itaingia madarakani, itawajibika kwa wananchi kwa kuweka kipaumbele katika maeneo manne ambayo ni hifadhi ya jamii, uchumi shirikishi wenye kuzalisha ajira nyingi na bora, afya na elimu.

Kauli hiyo ya ACT linakuja huku kambi ya vyama kadhaa vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ikiwa kwenye mchakato wa kuunganisha nguvu ili kusimamisha mgombea mmoja wa urais na kuachiana majimbo katika baadhi ya maeneo.

Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, James Mbatia amewahi kunukuliwa akisema kuwa umoja huo unaoundwa na Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD umehamishia nguvu zake kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Mbatia alisema tayari umoja huo umeunda kamati maalumu kutafuta namna ya kumsimamisha mgombea mmoja wa urais na kuachiana majimbo.

Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, alisema tayari kamati zimeundwa na zinaendelea na kazi ya kuratibu mpango huo mahsusi, unaolenga kuiondoa CCM madarakani.

Lengo letu ni kuhakikisha Ukawa ina nguvu ya kushika dola katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 na katika mpango huo, vyama vitaachiana majimbo na viti vya udiwani kulingana na nguvu ya chama katika sehemu husika,” alisema.

Mkakati huo uliopangwa na Ukawa, unaelezwa na wachambuzi wa masuala ya kisiasa kuwa ni kombora kwa CCM, kwani endapo utafanikiwa, utakiweka chama hicho tawala katika wakati mgumu katika Uchaguzi Mkuu uliopangawa kufanyika Oktoba mwaka huu.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad