ZITTO: Msimamo wa ACT Wazalendo kuhusu Ushirikiano wa vyama

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Msimamo wa ACT Wazalendo kuhusu Ushirikiano wa vyama

Kumekuwa na shauku ya wananchi kwa sisi kushirikiana na vyama vingine vya siasa ili kufanikisha malengo yetu ya kuleta mapinduzi ya kiuchumi kwa kuubomoa mfumo ...wa uchumi unaonyonya wananchi. Msimamo wetu upo wazi na tumeueleza mara kadhaa

1 tunaunga mkono juhudi zozote za kushirikiana kwa vyama na hili linathibitishwa na jina letu ALLIANCE na Msimamo wetu kuhusu mabadiliko ya Katiba.

2 tunataka ushirikiano utakaonufaisha wananchi na sio ushirikiano wa kugawana nafasi za uongozi.

3 hatuna shida na Tupo tayari kushirikiana na chama chochote kilicho tayari kushirikiana na sisi ikiwemo UKAWA ili kuunganisha nguvu kuitoa CCM kwa malengo ya kujenga uchumi shirikishi wenye kuzalisha ajira nyingi na bora, wenye mfumo wa hifadhi ya jamii kwa wananchi wote na wenye kutokomeza umasikini.

ACT Wazalendo haijatoa kauli yeyote dhidi ya UKAWA kama inavyoaminishwa na baadhi ya watu. Bali tumeweka wazi kuwa lazima misingi ya kiitikadi na kifalsafa izingatiwe katika ushirikiano. Tupo tayari kwa UMOJA. UMOJA ni moja ya misingi mikuu 10 ya chama Chetu na Umoja ni nguvu.
Tupo tayari

Zitto Kabwe
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad