Askofu Gwajima Asimamisha Mvua Dar "Mvua imekoma kuanzia sasa na haitaharibu tena, na ninaiamuru ardhi imeze maji yote yaliyojaa juu ya nchi".

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Askofu Gwajima....." Watu wa utabiri wa hali ya hewa wanasema mvua itanyesha zaidi LAKINI mimi nasema HAPANA mana tumezijua Hila zake shetani"

Katika mahubiri yake jana jioni tarehe 08/05/2015 siku ya Ijumaa, Askofu Mkuu wa Makanisa ya Ufufuo na Uzima alifundisha juu ya somo liitwalo "VITA VYA HALI".

Katika somo hilo Askofu Gwajima alibainisha wazi ya kuwa sio kila mabadiliko ya hali ya hewa yanayotokea duniani ni matokea ya nguvu za kiasilia za dunia yaani Nature au ni mabadiliko ya majira ya mwaka bali wapo watu pia wenye uwezo wa kubadili hali ya hewa kwa njia za kichawi na kusababisha mafuriko makubwa, vifo, uharibifu Wa mali na hasara zinazoweza kuwarudisha watu nyuma.

Katika kudhihirisha mambo hayo Askofu Gwajima alitolea mfano mtu mmoja aliyewahi kuishi duniani aitwaye Nicolas Tesla ambaye alikua na uwezo mkubwa juu ya kubadili na kutawala(control) hali ya hewa.

Baadaye nikaunganisha ujumbe wa Askofu Gwajima na nikagundua jambo hili ni kweli kabisa baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Sadick kutangaza kuwa MVUA HIZI ZINASAIDIA SANA KUWAONDOA WATU MABONDENI pasipo kuwaza kuwa watu hawa ndio walipa kodi wake na ndio wanaomlipa mshahara wake!

Kwa maneno yale sasa tunaamini ya kuwa Sio kila mvua, mafuriko, ajali za moto, ajali za magari au kiangazi ni mambo ya asili bali mengi hutengenezwa na wanadamu(wachawi) na mashetani ili kuwaangamiza wengine.

Kabla ya kumaliza Ibada hiyo jana jioni majira ya saa moja na nusu, Askofu Gwajima ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu wa Jeshi la Bwana la Ufufuo na Uzima aliyaongoza majeshi yote kwenye maombi ya kusambaratisha mvua na mafuriko yote na hali kuwa ya kawaida.

Maarifa makubwa aliyonayo Askofu Gwajima juu ya mambo ya rohoni na mwilini umefanya watu kuzijua hila za wachawi na mashetani wenye nia ya kuangamiza watu na kuwafanya masikini kwa njia ya maji..

"Mvua imekoma kuanzia sasa na haitaharibu tena, na ninaiamuru ardhi imeze maji yote yaliyojaa juu ya nchi"... alisema Askofu Gwajima katika kumalizia ibada.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

16 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Endeleeni kuwapotosha watu kwa kuamini imani zenu za kichawi hata makanisani ambako nilitegemea hilo halipo na mvua kwa bahati zikisimama basi mtaamini kuwa yeye ndiye aliyezimamisha hiyo mvua ya mshindo na kusahau kuwa sisi binaadamu ndiyo tumechangia sana kuyaharibu mazingara yetu wenyewe bila ya kujali kuwa tunajichimbia kaburi na sasa nature is hiting us back tunasema ni uchawi please people wake up and see the reality

    ReplyDelete
  2. wacheni ujinga usokuwa na tija. huyo askofu ni nani haswaaaaaaaaaaa. lol

    ReplyDelete
  3. kwakweli mnachekesha walonuna. du!

    ReplyDelete
  4. Huyu mchungaji ni msanii,mwizi na mshirikina. hana lolote zaidi ya kuwadanganya waumini wake

    ReplyDelete
  5. Hana lolote. Kaangalia weather online na kuona mvua itapungua kuanzia kesho yeye anasema kaisimamisha. Angalieni accuweather, mvua itasimama hadi jumamosi.

    ReplyDelete
  6. MWANDISHI USIPOTOSHE WATU WALIAMBIWA WAHAME HAWASIKII EE WANAHAMISHWA NA MVUA KAMA WAMWAMINI MCHUNGAJI KULIKO MUNGU NI SHAURI YAKO

    ReplyDelete
  7. Kafiri ni kafiri tu.

    ReplyDelete
  8. huyu mchungaji, kwanza anabiashara ya cocein, na ndo ilomtajirisha, anatumia uongo kuwadanya waumin wake. mnafiki mkubwa iko cku mungu atawadhihirishia watu uongo wake.

    ReplyDelete
  9. WAKATI AMINA CHIFUPA ALIKUFA SI ALISEMA ATAMRUDISHA MBONA MPAKA LEO HATUJAMUONA? WAJINGA NDO WALIWAO.

    ReplyDelete
  10. Hata wewe unae hukum una mkosea mungu anae mjua zaid ni mungu piga vita vizuri umalize safari salam maana kila mtu atatoa hesabu ya matendo yake hakuna atakae simama badala ya mwenzake kumbuka dhambi zote nisawa hakuna dhambi ndogo wala kubwa aliye mshirikina, alie mzinzi, alie mlevi, alie muongo alie mbea kuto mpenda unae muona pia nidhambi usihukum usije ukahukumiwa Mungu atusaidie kila mja atengeneze njia zake kwa kumuogopa Mungu sio mwanadamu yako hayajulikan kwa sababu haujulikani lakini kumbuka hakuna mwenye haki hata mja wote wametenda dhambi wew ni nani uhukumuye............

    ReplyDelete
  11. Penye ukweli siku zote wengi huonyesha chuki. Alisemalo Gwajima ni sahhi kabisaa!

    ReplyDelete
  12. Asimamishe mvua yeye Mungu? Hebu aishie zake huko asijemkasirisha Mungu akatuangamiza kwa kufuru za watu kama yeye.

    ReplyDelete
  13. Mbona alishindwa kuzima kesi yake,hana lolote ni mpuuzi tu.

    ReplyDelete
  14. watanzania amkeni achene kudanganywa na mpumbavu,unabii na mitume ilishakwisha,hakuma tena huyo ni nabii wa majini na freemason allah alishamaliza mitume na manabii uyo ni mfuasi wa shetani hana cha kanisa wala chochote tulishaambiwa watakuja watu kama hao lazima tuwee macho pia baba yao massi dajal atakuja atakua na uwezo kuliko huyo,turudi kwa mola wetu na kuongeza Imani na kuomba msamaa nusra sana kwa machafu yanayoendelea allah atuongoze,hakuzahajazaliwa,hanamfano na ituchochote pia hana mshriki tumuogope allah

    ReplyDelete
  15. Na huyu jamaa ni wa kabila gani ni mgagagigikoko nini?

    ReplyDelete
  16. oooh! wajinga ndiyo waliwaoo.. oooh!

    ReplyDelete

Top Post Ad