Aunty Ezekiel na Kajala Masanja Wamseng'enya Wema Sepetu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MASTAA wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel na Kajala Masanja, juzikati walikutana na kutumia muda wa takriban nusu saa (dakika 30) kumsengenya aliyekuwa shosti wao, Wema Sepetu.

Tukio hilo lilijiri  hivi karibuni kwenye Bustani za Ndoto Polepole zilizopo Bagamoyo, ambapo mastaa kibao walihudhuria sherehe ya Baby Shower ya Aunt, iliyokuwa imesheheni vituko kibao huku gumzo likiwa ni kutokuwepo kwa Wema.

Awali paparazi wetu aliwashuhudia wawili hao wakimzungumzia Wema tena huku watu wengine wakisikia, kubwa likiwa kumshangaa kwa namna anavyotaka kila anayekuwa rafiki yake, awe adui wa maadui zake.Mjadala huo ulikuwa mkubwa, ambapo Kajala kuna wakati alimuuliza Aunt sababu ya Wema kutokuwepo eneo hilo ndipo alipompa mkasa mzima.

Mazungumzo hayo ya Kajala na Aunt yaliwafanya hata waalikwa wengine kumteta Wema, wakidai kuwa anatakiwa kujiangalia kwani ni staa ambaye hadumu na marafiki zake na mara nyingi wakiachana, huachana kwa ubaya.Ijumaa lilijaribu kuingilia mazungumzia hayo ili kujua kisa cha wao kutumia muda mwingi kumjadili Wema lakini wote waliishia kuguna kisha kuendelea na sherehe hiyo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. WASENGE WAKUBWA MNASAIDIWA HALAFU NG'ENG'E

    ReplyDelete
  2. Acheni ugonganishi.

    ReplyDelete
  3. ACHENI UCHONGANISHI UDAKU OVYOOOOOOOOOO

    ReplyDelete
  4. Nisaidieni Nini maana ya PEDESHEE jameni?

    ReplyDelete
  5. Wema kuwa na mimi sitokuteta ushosti utakuwa poa kweli.

    ReplyDelete

Top Post Ad