Baada ya Kupata Mamilioni, Diamond na Zari Ndoa Yafungwa Rasmi, Yadaiwa ni Kujibu Ndoa Aliyojitangazia Wema Sepetu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

HUKU wakidaiwa kuogelea kwenye utajiri wa mabilioni ya fedha, nyota  wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ameibukia kwenye Gazeti la Amani na kusema kuwa, amefunga ndoa ya kimyakimya na mpenzi wake wa sasa, Zarina Hassan ‘Zari’ ambaye ni nyota wa muziki wa kizazi kipya, nchini Uganda na Afrika Kusini.

Diamond aliyasema hayo juzi jijini Dar es Salaam alipofanya mahojiano na waandishi wetu baada ya kumuuliza kama ana mpango wa kufunga ndoa na Zari.

SIKIA MAHOJIANO HAYO
Amani: “Zari ameshakubebea ujauzito, ameshaandaa shoo ya nguvu ile ya Zari All White Party hapa kwenu Tanzania na ameonekana kukubalika na baadhi ya mashabiki wako. Je, una mpango gani wa kufunga naye ndoa sasa?
Diamond: “Khaa! Mbona kama ni ndoa na Zari nimeshafunga kimyakimya!”
Amani: “Si kweli bwana! Lini na wapi?”

Diamond: “Hapahapa Dar. Lakini siwezi kusema ni wapi kwani tulishaamua iwe kimyakimya na imepita tayari, siku chahe kabla ya ile shoo ya Mlimani City.”Amani: “Kama ni kweli kwa nini haikuwa na mashamsham kama ndoa za mastaa wengine?”

KISA CHA KIMYAKIMYA
Diamond: “Unajua bi mkubwa (mama yake mzazi, Sanura Kasim) alikuwa anaumwa, kidogo ana nafuu kwa sasa. Ndiyo maana sikutaka mashamsham.”Amani: “Zari mwenyewe amekubaliana na uamuzi wa ndoa ya kimyakimya?”
Diamond: “Hakuwa na shida.”

KUHUSU DINI YA ZARI
Amani: “Amebadili dini? Maana ilisemekana alikuwa Muislam, akabadili kuwa Mkristo.”
Diamond: “Ilikuwa rahisi kurudi kwenye imani yake ya kwanza kwa hiyo ataendelea kuitwa Zarina.”

DIAMOND SASA
Rafiki wa karibu wa Diamond ambaye hakupenda jina lake kutajwa gazetini lakini wengi wanamjua, alipoulizwa kuhusu ndoa ya Diamond na Zari alisema:
“Jamani! Jamani! Jamani! Hivi kweli mnavyomjua Dangote (Diamond) nyie anaweza kufunga ndoa kwa siri au kimyakimya?”

Amani: “Amesema kwa sababu mama yake bado hajakaa sawasawa kiafya?”
Rafiki: “Mbona kaenda kutumbuiza kwenye Zari All White Party, Mlimani City, si angekaa na mama yake nyumban? Hivi Dangote mnamjua, mnamsikia? Acheni kabisa.

“Dangote anapenda kiki! Kila siku anawaza kiki. Kwa hiyo kusema amefunga ndoa na Zari sidhani kama ni kweli inaweza kuwa ni kiki. Tena afadhali kama Zari asingekuwa na mimba, lakini ameshambebea ule mzigo ndiyo kabisa maana Dangote yeye hana cha kupoteza. Lakini anyway, labda kweli.”

NI SIKU CHACHE BAADA YA WEMA KUDAI AMEFUNGA NDOA
Hivi karibuni, mpenzi wa zamani wa Diamond aliye pia Miss Tanzania 2006 na staa wa sinema za Bongo, Wema Sepetu naye alitupia kwenye mtandao wa Instagram picha inayomwonesha amefunga ndoa kwa siri.

Baada ya picha hiyo kuwa gumzo, baadhi ya vyombo vya habari, hasa vya kielektroniki vilimpigia simu Wema ili kumuuliza kama kweli amefunga ndoa kwa siri kama inavyoenea kwenye mitandao, Wema alikiri.
Kwa ile sauti yake ndogo: “Yeah! Nimefunga kweli ndoa.”

Swali: “Sasa Wema wewe ni supastaa, kwa nini ufunge ndoa kwa siri mpaka wadau wako wasijue?”
Wema: “Mume wangu hapendi ijulikane. Hata mimi sipendi ijulikane.”

YALIYOMKUTA WEMA BAADA YA KUKIRI
Amani lilizungumza na mtu mwingine wa karibu na Wema ambapo alisema:
“Jamani Wema amejitakia matatizo, ndugu zake, dada yake na mama yake wamemjia juu. Kwanza walimuuliza kama ni kweli amefunga ndoa bila wao kujua, akasema hajafunga.

“Mama yake alimwambia alichokifanya cha kukiri kwenye redio ni nuksi kubwa kwake na Watanzania hawatamwamini tena hata akisema ukweli.“Unajua ndugu zake waliweka kikao. Walikubaliana kwamba, kama ndoa yake ilikuwa kwenye filamu si mbaya lakini walilaani kile kitendo cha kuulizwa na watangazaji wawili wa redio tena kwa muda tofauti akakiri. Pale ndipo penye tatizo. Leo hii Wema atazungumza ukweli gani kwa watu wakamuelewa?”

WEMA NA GAZETI LA AMANI
Wema alipotafutwa juzi na gazeti hili na kuulizwa kuhusu ndoa hiyo alikiri kuwa ilikuwa filamu ambayo itatoka hivi karibuni.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Bongo enheee, Bongo dar es salaa....Manjooonjo eeeh ndani ya Dar es salaam

    ReplyDelete
  2. Hehehehhehehehe mtakoma na mtoto Wema utadhani ye ndo Star pekee Bongo mbona hampumui mchana kutwa juu yake.

    ReplyDelete
  3. Wema kupenda attention paka kudanganya umeolewa kweli we ni Mtumwa wa scandal

    ReplyDelete
  4. Heeeeee yani hawa watu ni shida kweli yanini sasa kujitangazia ndoa ya uongo?

    ReplyDelete
  5. Hakuna ndoa ya kiislam inafungwa wakati mwanamke ni mjamzito wasitufanye wajinga labda waliifungiya kanisani

    ReplyDelete
  6. Hakuna ndoa ya kiislam inafungwa wakati mwanamke ni mjamzito wasitufanye wajinga labda waliifungiya kanisani

    ReplyDelete
  7. Anafunga ndoa ya siri kwa sababu mama yake anaumwa lakini anaandaa party kubwa na kila siku anakula bata au yuko njiani kumtoa mama yake Msukule ili azidi kuwa tajiri?

    ReplyDelete
  8. Hebu tuwekeeni video ya Diamond akimnengulisha Zari, haya wajameni si mlimsema Wema mjinga anakubali kukatishwa mauno stegini na huyu mama mjamzito kilimsibu kitu gani kukatika mauno kwenye party na tumbo lake. Halafu anabingirika mpaka chini mhh isijekuwa kafunga Silicon tumboni hakuna mwanamke mwenye tumbo kubwa kiasi kile anaweza kukatika mauno mpaka chini, kwanza unafanyaje kwani. Nina experience ya kubeba mimba tayari inavyokuwa tumbo zito limekaza unakataje mauno kwanza? Unless kama hakuna mtoto waweza kata lakini kama tumboni kuna mtoto subutuuuu hiyo kukaa kitako tu kasheshe seuze kukata mauno.

    ReplyDelete

Top Post Ad