Basata Yalaani Tabia Chafu na Isiyo na Maadili Iliyoonyeshwa na Shilole Akiwa Jukwaani Nchini Ubelgiji

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa na burudani nchini limeona picha chafu na zisizo na maadili za Msanii Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole alipokuwa akifanya onesho lake nchini Ubeligiji hivi karibuni.

Katika picha hizo ambazo zimelaaniwa na watanzania wengi nchini kupitia njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii, Shilole anaonekana akiwa Jukwaani huku viungo vyake vya sehemu za siri vikiwa hadharani na zaidi akionesha tabia ambazo kwa kiasi kikubwa zimefedhehesha na kuidhalilisha sekta ya Sanaa na Taifa kwa ujumla.  

Aidha, BASATA limepokea malalamiko kwa njia ya simu na mawasiliano ya internet kutoka kwa watanzania waishio ughaibuni wakilaani tukio la Msanii huyo. Katika mawasiliano yao wameeleza kwamba wamefedheheshwa na kudhalilika na tabia hiyo chafu iliyooneshwa na msanii huyu.

Ikumbukwe kwamba, Shilole ni msanii aliyesajiliwa na Baraza la Sanaa la Taifa, hivyo anapokwenda nje ya nchi kabla hajapata visa anapewa barua ya utambulisho kama msanii wa Tanzania, hivyo anapokuwa nje ya nchi anatambuliwa kama msanii Mtanzania, anapofanya kinyume na misingi ya kazi ya Sanaa, anajifedhehesha yeye mwenyewe, kazi ya Sanaa na nchi yetu pia.

Aidha, ikumbukwe kwamba BASATA limeshapata kumwita na kumuonya msanii huyu kutokana na tabia yake ya kutokujiheshimu pale awapo jukwaani na yeye aliahidi kubadilika na kuachana na tabia hiyo chafu. Kwa hiyo kuendelea kwake kufanya matukio hayo na kwa sasa katika ardhi ya nchi nyingine ni uthibitisho kwamba hajabadilika na kwa maana hiyo ameendelea kuidhalilisha Sanaa na wasanii wa kitanzania wenye kujitambua na kuiheshimu Sanaa kama kazi nyingine.

BASATA linapenda kueleza kwamba;

Litamuita kwa mara nyingine tena kumtaka ajieleze kwa nini alifanya onesho hilo la kujidhalilisha na kudhalilisha hadhi ya mwanamke, msanii na Sanaa kwa ujumla
Kama maelezo yake hayataridhisha hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake maana tayari ameshadhihirisha kwamba akifanyacho si Sanaa na hakina uhusiano na kazi ya Sanaa ambayo ina heshima yake na inahitaji ubunifu, weledi na kujitambua
BASATA linawakumbusha wasanii wote nchini kuwa Sanaa ni kazi kama kazi zingine lakini siku za hivi karibuni wasanii wengi wamekuwa wakikiuka suala zima la maadili kwa kutengeneza kazi chafu zisizofaa mbele ya jamii ya watanzania wanaoipenda na kuiheshimu kazi ya Sanaa yenye staha. Tuungane kwa pamoja kukemea kazi chafu zinazozalishwa na wasanii wasiojitambua kwani suala la maadili ni suala mtambuka na linaanzia katika ngazi ya familia.

Aidha, BASATA linawataka Wasanii wote nchini kufuata sheria, kanuni na taratibu mara wanapopata mialiko ya kikazi kwenda nje ya nchi. Linawakumbusha kwamba haiwezekani msanii kutumia picha chafu na mavazi dhalili na kuonyesha utupu katika kuvuta mashabiki.

Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini

Godfrey Mngereza

KATIBU MTENDAJI
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu anatakiwa kufungiwa

    ReplyDelete
  2. KWANINI WASIMFUNGIE KWASABABU VITU ANAVOVIFANYA SI VYAKAWAIDA TANAOMBA WAMUFUNGIE ASHIKE ADABU KIGODO KAMA MCHUMBA WAKE ANAMTETEA SIKEASABABU AKILI ZAWO ZIKO SAWA KWASABABU NAYE SANAIFADHIWA TUU HANA LAKUSEMA ANDEKUWA MWANA UME WAKWELEWEKA ASINGE MTETEA LAKINI NA MCHUMBA MWENYEWE NDIO HIVYO HANA NYUMA WALA MBELE LAKINI BASATA MTUSAIDIE MUMUFUNGIE MKIKATA TUTAJUWA KUWA MNATEMBEA NAYE

    ReplyDelete
  3. waungwana husema ukienda ugenini ukakuta wenyeji wanalia basi na wewe lia maana ukianza kucheka utaonekana mchawi, kwahiyo hata unapokuta tamaduni za watu hao ni tofauti na zile za kwenu basi yapaswa na ww kufanya bahadhi ya mambo ambayo wao wanayafanya hivyo basi tusiwe tunawalaumu sana hawa wasanii kwa yanayo wakuta huko ugenini maana wao wanatafuta maisha na kwenye kutafuta maisha kila mtu ana mbinu zake katika kazi yake husika,wengine wezi maofisino, wengine vibaka, wengine ilikupata maisha mazuri wanaroga. Hivyo basi tusiwe wepesi kuhukumu maana hata huyo shilole sidhani kama kweli kabisa alidhamilia yatokee hayo yaliyotokea sema ndo hivyo ajali kazini, au waungwana mlikuwa mnataka avae dela kwenda kufanya shoo yake!?. Hivyo ushauri wangu kwa basata tena nyie ndo mnaojua changamoto zinazowakuta wasanii wetu hasa wakike mnatakiwa kuwa makini sana katika kufanya maanuzi yenu na sio kusikiliza maneno ya watu wasio elewa hata changamoto ambazo wasanii wanazipitia hadi kufikia walipofikia.kila nchi inatamaduni zake shilole angeyafanya hayo hapa nchini basi hata mimi ningemlaumu japo si sana maana lazima ningezingatia vigezo na masharti kimazingira. Niwaache naswali dogo kwa basata '' hivi ni basata walio gharamia safari na mahitaji yote ya msanii huyo alivyokuwa huko nje au amejigharamia mwenyewe???????''

    ReplyDelete

Top Post Ad