Diamond Platinumz Katika Hili Umekosea,Umekosa Busara ni vyema Ukajifunza Kuweka Akiba ya Maneno

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Nime yaandika haya baada ya kuona post ya
Diamond akikosoa vikali tunzo za kill hadi amepitiliza na kuandika yasiyo tarajiwa pengine alikuwa na hasira sana lakini tusisahau kuwa hasira haijengi!
Kwangu mimi naona amekosea sana!

Hakuna busara iliyo kuu kama ku kaa kimya! Hapa ndio naamini wasanii wana hitaji washauri wa karibu kabla ya kuandika au kusema chochote!

Diamond umekosea sana tena sana..ulikuwa na nafasi ya kukaa kimya kuonesha busara kuu!Kuna mtu alisema ukitaka kutambua mtu mwenye busara subiri akiwa na furaha sana au akiwa na hasira sana!

Naanimi Diamond hukufikiri mara mbili kabla ya kupost uliyo yapost! Kila mtu anajua wazi kuwa hizi tunzo hazijakamilika na haziwezi kukamilika kamwe na hata kama kuna mtu atapewa kuziendesha kamwe haziwezi kuwa satisfy watu wote na wakati wote!

Pengine ni kweli anayo jaribu kutuambia Diamond lakini ninacho jiuliza hii ndio busara yako ya mwisho?
Kila mdau wa muziki anajua fika kuwa hakuna mwaka ambao umekuwa na hit song nyingi kama mwaka jana na mimi nilijua utaleta malalamiko mengi sana lakini niliamini kuwa busara ndio itatumika zaidi kuliko hasira au meneno ya kuwa vunja moyo waandaji waonekane hawajafanya lolote kwa kuwa tulio wategemea hawapo!

Diamond una sahau kuwa wakati unapewa tunzo wewe kuna watu wali lalamika kuwa umependelewa na wengine wakajitoa na wengine wakatumia busara na kukaa kimya!

Jamani kama maneno ya namna hii yangekuwa yana andikwa basi yangetoka kwa Bell 9 ambaye watu walikuwa wanaamini kuwa ana stahili tunzo kila leo..lakini kijana wa watu amekuwa ni mwwnye hekima sana na nina mpongeza kwa hilo!

Diamond kusema kuwa hata usipopewa tunzo huwezi kushuka ni kuwakosea heshima Kill na Basata kwani hizi ni tuhumu zisizo na msingi kutoka kwa msanii mkubwa kama wewe ...ni kweli wana lengo la kukushusha?
Diamond umekosa busara kabisa kabisa ulipaswa kukaa kimya maana ni wachache wataamini una watetea hao ulio wataja!

Diamond jifunze kuvumilia na si kila kitu cha kukifanya public..Diamond ina maana kusema kwako hukuhangaika kuwambia watu jinsi ya kupiga kura maana hukupendezwa ina maana umegomea tunzo? Ni kweli Kill na Basata wamekuwa wabaya kiasi hiki hadi una diriki kuuliza kama wanau au kukuza muziki?

Diamond umenishangaza sana tena sana lakini na kukumbusha ujifunze kuweka akiba ya maneno na ndio busara iliyo kuu kuliko kuongea!

Diamond umeshindwa kujiuliza kwanini wengine wame nyamaza?

Mimi naamini hizi tunzo ni nzuri na ni msaada kwa wasanii pia si tunzo zilizo kamilika na hakuna tunzo zilizo kamilika duniani!

Uzuri wasanii huwa mnapewa semina kwa hiyo mnaweza kusema huko huko malalamiko yenu lakini kuongea kwenye media tena kwa njia uliyo tumia itachukuliwa ni kutaka watu wagomee tunzo hizi!

Wasanii ni vyema mkawa mnaweka akiba ya maneno ili msiwa katishe tamaa walio jitoa kuikwamua tasnia hii kwani nao hawaja kamilika!

Karibuni wana jamvi!8
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

18 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. UKIWA NA DOMO KUBWA LAZIMA UTAKUA MTU WA KUBWABWAJA OVYO. ILA HUYU NAE UTOTO UNACHANGIA

    ReplyDelete
  2. Mbona upuuzi tu umeandika, umeng'ang'ania tu umekosea sana lakini husemi kipi amekosea. Katoa maoni yake na na kila mwenye akili timamu ameelewa kipi alichokisema wengi wameunga mkono. Au tuzo za baba ako, watu wanatumia pesa nyingi kuinvest kwenye mziki ili wafanye kitu bora kwa faida yao na mziki pia lakini wapuuzi wanafanya mpango kurudisha nyuma, kwa akili yako fupi tu unadhani video ya ndagushima na mwana ipi kiubora inastahili kuwepo kwenye video bora, au unahisi Kuna upcoming gani ambaye amehit kama basi nenda ya mo music, huo ndo unaitwa ubabaishaji lazima atokee giant mmoja athubutu kuongea kwa maslai ya wengine and trust me kuna effect inaonekana, and for your info mitandao mingi ya Africa imeandika hyo habari, na waandaaji wanahanya. Go platnumz go pave the way.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mbona mwaka jana akulalama aanze kulalama mwaka huu?? atuache tulale sisi sasa, yeye akeshe..

      Delete
  3. Acha uchocheaji,nawe pia umekosea,ungekuwa na nia ya kumrekebisha ungemwamwbia private ila hapo unamtengenezea maadui na si vizur

    ReplyDelete
  4. Domo alilopoka, Huwezi ukawa juu sikuzote

    ReplyDelete
  5. duh duniani hakuna haki hadi leo Belle 9 hajawahi kupata tuzo bongo!

    ReplyDelete
  6. Mbona last yr hakusema hayo mane I huyo daimond, tatizo Ana penda misifa, eti hawezi kushuka...Walio mpandisha wakichoka na misifa yake watamshusha, and it is very easy, aangalie hats wanamuziki wake marekani walio kuwa majina makubwa ambao walikuwa na dharau na skendo Wako wapi? Mashabiki wao wamewapiga chini, unatoa single or albam hakuna anaye nunua. Respect respect... He has long way to go aache majivuno ya kit to na kuona km ameshafika,

    ReplyDelete
  7. Domo kakosea eti yy hawezi kushuka ivi anajua kesho?ss mashabiki ndy tunamkubali tukigoma atapotea ebu ona BELE 9 hachukui tuzo ila yupo kimya hana tatizo kwani BELE haumii!

    ReplyDelete
  8. HAWEZI KUSHUKA KAJIUMBA HUYO!!

    HUYU NI MR. ROPO ROPO!! KUANZIA WANAWAKE MPAKA MAISHA.
    MXXXXXX

    ReplyDelete
  9. akili zake zipo pumbuni

    ReplyDelete
  10. diamond yuko juu 2 sema watanzania hatupendi kuapreciate kitu kizuri anachofanya mtu muandikeni vibaya but wakuamua kumshusha ni mungu 2 muacheni aseme coz akinyamaza kuna vitu watu watashindwa kujifunza

    ReplyDelete
  11. Hawezi kushuka kwani juu alikuwa lini!!!???
    Kanyeeeee huko
    Yote woga baaada yakuona kiaribu kila category yuko na king kiba mbweha huyo

    ReplyDelete
  12. wamepita mitume msikwambie yeye, kwan ye nan? na nyie wajiga mnaotetea upuuz wakat mtu kakosea na nyie wapuuzi vilevile akikosea asiambiwe kisa yuko juu. mna akili finyu nyie

    ReplyDelete
  13. wewe mwandishi hujielewei, unapoandika taarifa ueleze na ilivyokuwa, sasa kwa akina sisi hatuji diamond alichoandika ww unatusaidiaje, acha wivu wa kijinga.domo yupo juu utake usitake

    ReplyDelete
  14. Mawazo mmetoa na onyo pia imotional kama mtu ameumia lazima aongee kiukwel na alichokifanya mond nni his filings tufanye yetu wana

    ReplyDelete

Top Post Ad