Eti Wema Mrembo Kuliko Zari!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Imebainika kuwa maneno ‘gold digger’ katika ulimwengu wa fursa yanamaanisha kuwa ni mtu anayeona fursa na kuzitumia katika ‘kufaiti’ kupata mafanikio (utajiri) kwenye maisha.

Ndivyo alivyo mwandani wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ambaye humwambii kitu linapokuja suala la kuona fursa na kuzifanyia kazi.

Pamoja na sifa hiyo iliyomfanya Zari kuwa mmoja wa mastaa matajiri Afrika Mashariki lakini kwa mujibu wa mashabiki waliomuona ‘laivu’ usiku wa Ijumaa iliyopita kwenye shoo yake ya Zari All White Party katika Ukumbi wa Mlimani City walisema aliyekuwa mpenzi wa Diamond kabla yake, Wema Isaac Sepetu ni mrembo zaidi kuliko yeye.

Gazeti la Ijumaa liliwashuhudia wadau wengi ambao walimuona Zari kwa mara ya kwanza kwenye show yakewakimshangaa na kudai kuwa yupo tofauti na anavyoonekana.

Kwa mujibu wa mashabiki hao, picha ambazo wamekuwa wakiziona kwenye mitandao ya kijamii zinakuwa zimeeditiwa (kuhaririwa) na kwamba ukimuona ‘live’ huwezi kuamini.

“Jamani siamini kama huyu ndiye Zari tunayemuona kila siku kwenye Instagramu maana yupo tofauti sana.

“Kwa waliokuwa wanasema anamzidi Wema wamenoa. Wema ni habari nyingine,” alisema mmoja wa warembo waliokuwa wakisukumana kumuona Zari.

“Mimi nadhani ni kwa sababu labda amezaa watoto watatu na sasa ana ujauzito wa Diamond wa mtoto wa nne so hawezi kumfikia Wema ambaye bado hajazaa,” alisema mrembo mwingine akimtetea Zari.

“Hamna bwana, kinachombeba Zari ni make-up (vipodozi) ambavyo anatumia kwa asilimia mia moja lakini Madam (Wema) hata asipotumia make-up lazima utampenda tu,” alisema mwingine aliyedaiwa ni Team Wema.

Kuhusu make-up, gazeti hilo lilizungumza na mmoja wa watu wa Timu ya Diamond ya Wasafi Classic Baby (WCB) ambaye yupo kitengo cha mapambo ambaye alithibitisha kuwa Zari hufanyiwa make-up kwa muda mrefu hadi mwenyewe akubali kuwa yupo sawa.

Mdau mwingine aliliambia gazeti hilo kuwa Zari ni mjasiriamali na ameona kwa Diamond kuna fursa ndiyo maana akakubali kumbebea ujauzito lakini si kweli kwamba ni mrembo kuliko Wema.

“Ameona fursa kwa Diamond. Kwa mfano shoo kama hii (Zari All White Party) asingeweza kuifanya bila kuwa na ‘koneksheni’ na Diamond,” alidai mdau mwingine.

Habari zinasema kuwa Zari ameona kuna fursa nyingi Bongo ndiyo maana amekubali kufunga ndoa na Diamond bila kujali kigezo cha umri. Ana umri wa miaka 34 wakati Diamond ni 26.

Akijibu swali juu ya uraia wake wa Uganda na Afrika Kusini na kwamba yeye na Diamond wanatarajia kuishi nchi gani mwanamama huyo alifunguka:

“Tutaishi hapahapa (Bongo). Kwa utamaduni wetu (Waafrika) inabidi mwanamke uondoke nyumbani kwenu umfuate mpenzi wako mkaishi wote.

“Watanzania ni watu poa sana, siwezi hata kuwalinganisha ni wakarimu sana.”

Kuna madai mazito kuwa Zari si mtu wa kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na mtu ambaye hana fursa ya kimaendeleo kwani historia inaonesha kwamba wanaume wengi aliowahi kuwa nao walikuwa ni watu wenye nazo.

Baadhi ya wanaume waliowahi kuwa naye wanaosemekana kwamba hawakuwa watu hoehae ni pamoja na aliyekuwa mumewe, Ivan Semwanga ambaye alizaa naye watoto watatu akiwa ni mmoja wa mabilionea nchini Uganda.

Wengine ni Isaac Lugudde ambaye ni staa wa mpira wa kikapu nchini Uganda, mtoto wa mjini nchini Uganda, Farouk Sempala, Jenerali Jeje Odong, wasanii wa muziki, Moze Radio na  Weasel, Aziz Azion, Isaiah, Robert Ogwal a.k.a Rasta Rob, Exodus, DJ Shiru, mfanyabiashara mkubwa wa Nigeria na sasa ni zamu ya Diamond.

GPL
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ACHENI KUJIONGOPEA, WEMA ATAMPATA WAPI ZARI, ZARI MREMBO MIMI SIPO TEAM YOYOTE LAKINI ZARI MZURI KULIKO WEMA, KWANI HUYO WEKA HATUMII MAKEUP? NA HAPO KAZAA WATT WA 3 NA NI MJAMZITO BADO ANALIPA, SASA HUYO WEMA HAJAZAA YUPO HIVYO AKIZAA ITAKUWAJE????

    ReplyDelete
    Replies
    1. Usiseme hajazaa sema hajalea hata kuflash mimba ni kuzaa pia

      Delete
    2. Kuzaa si tatizo la kuweza judge m2 eti akizaa atakaaje kujiweka vizuri ndo siri ya urembo kwa kila m2. hata Wema akizaa maitenance poa ndo itazidisha urembo acha kujisahau.

      Delete
    3. Usiangalie kuzaa au kutozaa kwani hayo ni majaaliwa ya mungu, angalia urembo unaozungumziwa. Zari hampati Wema hata kwa bahati mbaya

      Delete
  2. mbaya ana watoto watatu na miaka 34 na wanne juu anakuja lkn akisimama na wema zari bado kjn sana wema akizaa apo kushnehi maana mwili wake ni wa kutepeta mbaya lkn ndo kashatia bl1 kibindon mzur wetu ana nn jmn

    ReplyDelete
  3. Dooo! Kumbe kaburuza sana wanaume, chunga basi Diamond manake inabidi uwe makini kwa kutaka kuoa wazee waliokuzidi maalifa kitaandani..huenda hata hiyo mimba si yako domo

    ReplyDelete
  4. Ukilitafakari hilo neno la "ETI.....tayari linaashiria uchonganishi wa hizo pande mbili za hao mabinti duh waandishi jirekebisheni noma kuchonganisha halafu nyie mmekaa pembeni mnacheka tu au ili magazeti yenu yapate soko chapchap

    ReplyDelete
  5. haya wekeni na aliolala nao Wema sasa,na kwani wema sio gold gigger?mbona mnawasakama watoto wa watu,

    ReplyDelete
  6. Muweke wema bila make up na zari bila make up afu ndo use me hayo..zari ni mama wa watoto watatu lakini ukinwangalia ni nyororoo...wema hana ata wa kusingiziwa angalia huo mchina wake. Nlimpenda wema zamani ila aliponenepa ghafla na kujikoboa nkaona ni wale waleee.wakatu kalikua kazurii na ngozi yake natural na kaumbo kamis

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mmmhh ndugu yangu ukiwaweka Wema na Zari bila makeups Zari atatisha sana, na hivi hajawahi kuweka picha ya bila make up hata kwa bahati mbaya au kwa kukosea acha tu.Picha za Wema bila make up tushaziona sana na tunajua urembo wake na ndomaana tunausemaa bayana. huyo Zari mbona hata mwenyewe anajiogopa???na hata make up artist wake keshasema kuwa wanampamba kwa muda mrefu ndo akubali hata kutoka nje, hv kwanini muendelee kubishia uhalisia??? Zari mbaya hata mwenyewe anajitambua ndomaana anajitundika mi kontua kila saa kila sekunde

      Delete
  7. wema hamfikii zari hata kwa chembe, angalia hata miguu, wema hana!! zari kitu bana! sema ndiyo hivyo tena nae anamambo yake!

    ReplyDelete

Top Post Ad