Hivi wanandoa wenzangu na wake zenu pia wako kama huyu wangu?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Baba yangu mzazi kaja juzi kutoka kijijini kwa matibabu.Nilimkatia tiketi ya ndege akapandie mkoani, mke wangu akadai ni uharibifu wa pesa kumsafirisha Mzee kwa ndege angepanda basi wakati mzee wake mwezi uliopita alikua hapa kwetu na kaja kwa ndege kwa hela yangu wakati haumwi ni mzima na baba yangu alikua mgonjwa.

Kana kwamba hiyo haitoshi mizunguko yote ya muhimbili naenda mm na ndugu zangu Wa ukoo yeye yupo busy na kazi, anaenda kwa kusukumwa mno.

Ukiachana na hilo hata misiba ya ukoo wetu either atatafuta sababu inayokaribiana na ukweli asiende au ataenda akifika pale anageuka mgeni hashughuliki na chochote.

Wazazi wake wakiwepo hapa itakua ni kama wageni wametoka ulaya nitapigiwa simu nije na grant, sijui ninunue jack Daniels kwamba baba anapenda sana hiyo pombe njoo nayo dear.Weekend tuwapeleke wazazi wake beach yaani inakua ni mikiki ndani.

Tofauti na wazazi wangu wakija hakuna kinachoendelea ndani, hakuna mabadiliko ya vyakula wala nini mimi kwa kuepusha shari huwa namwambia baba twende tukale bar maana anatakiwa ale vyakula chukuchuku au vya kuchoma.

Jana usiku baba aliniuliza kuwa huyu mwanamke mlifahamiana muda gani kabla ya kuoana nikamwambia miaka 4 akasema si kweli hakuamini.Nikajiuliza kwa nn baba kaniuliza swali hili.

Hayo yote ni Tisa Kumi hufanya mambo yake ya maendeleo kimya na kwa siri kubwa humtumia mdogo wake wa kiume kufanya hayo yote I.e kujenga kwa siri. Nikiamua kumweka chini kwa utulivu na kumuhoji kikao hubadilika na kuwa vurugu tupu kwamba namfatilia, kwamba simpi nafasi apumue, kwamba mwanaume nina gubu mimi.

Anyway mimi ni mfanyakazi wa shirika la kimataifa, nina masters, wife ana bachelor degree yeye ni banker
Tuna watoto wawili mmoja yupo primary school standard one na mwingine nursery school.

Wakuu nawauliza hivi:-
(1) Hili ni hali ya kawaida kwa ndoa zote?

(2) Inawezekana sikumfaham huyu mwanake kwa undani?
(Relationship 4 years) je muda huo hautoshi kumjua mtu? Au alificha?

(3) Nimuite mzee yupi kuja kuzungumza nae maana wazee wote wa ukoo wangu anawaona hawana maana

(4) Kuna yeyote kati yenu ndugu zangu wana JF mwenye shida kama hili? Na aliitatuaje?

(5) Wazazi wangu wamechoka na hali hii niwaeleze nini wanielewe?

(6) Nimfanyeje mwanamke huyu?

Naomba ushauri wenu kwa dhati ya moyo wangu maana mimi mwenyewe nimechoka na hali hili iliyodumu kwa miaka 8
Sasa nafikiria REGIME CHANGE

NB: Sijawahi kuchepuka ila kwa sasa ndo nimeanza kufikiria replacement

By didier kinuani/JF
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

21 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hakupende huyo, anajiandaa kukimbia.

    ReplyDelete
  2. Wewe komaa tuu!! Kwani wanawake wote ndivyo walivyo, usihangaike wala nini.

    ReplyDelete
    Replies
    1. koma, kama wakwako yuko hivyo sio wote. tena omba radhi

      Delete
  3. Pole we nenda nae taratibu umwambie ambacho hupend akifanya, pia kuhs kukuficha anayofanya inawezekana na ww unavowapa ndg zako uwa unamficha, mfn unakuta mume anasomesha wadogo zake labda mnakaa nao humo humo ndan lakn anampa hela pemben hakwambii hata kam anamsomesha kwa ada hii, labda naul nampa kias hiki anakuficha na anampa hela ww huon mpk anafanya wadogo zake waamin labda mke hapend kumbe hushirikishw, anaombana hela na wazaz wake juu kwa juu we unakuja kukutana na pay slip za bank mda wa kufua nguo au msg za m pesa kwenye sim, kiukwel hii inaumiza sana

    ReplyDelete
  4. pole mwana jamvi,
    inaelekea kuna kaugomvi fulani hivi hapo kwenu hutaki kukaweka wazi, inawezekana ndugu yako mmoja au wengi waliwahi kumkera akakueleza na ukapuuzia. unajua wanawake wanapenda attention ndogondogo sana, so toka siku hiyo akaweka kinyongo na ndugu zako. haiwezekani kwa hali ya kawaida mtu akachukia ndugu zako. lakini pia kaa naye umuulize kwa upole na ujue anashida gani?
    asipotaka kujibu hilo litakuwa jingine lakini mchepuko na kulewa sio suluhisho.
    ikishindikana bora ufanye divorse mchepuko atakusumbua maana utamuelezea siri za mkeo na yeye atazifanyia kazi kila ukifika kwake utamuona yuko pefect 100% atakuja kukutesa pia utakuwa mtumwa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Naungana na ww hata mim kuna ndg m1 ndo kero yangu kwa tabia zake anazofanya kwangu na akienda kwao anapeleka maneno bas nimejikuta nawachukia wote kwasababu naona lao moja, wanaume mjitahid kua na misimako sina unaruhusu wadogo zako wa kike kiume au mama ako kuendesha ndoa zenu hicho kitu kinakwaza sana wanawake mtu unakosa uhuru kwa nyumba yako kisa wifi anakuongilia kila kitu lol

      Delete
  5. mhhh my friend kwa ufupi huyo mwanamke akupendi mtu ambaye awezi kupenda wazazi wako yuko selfish anataka wazazi wake sio kabisa miaka minane unavumilia ujachepuka na matatizo yote hayo ulikuwa wapi au kakuroga pole she is not a wife material ongea naye asipobadilika find another option ila watoto tu ndio nawahurumia STUPID WOMAN sio wanawake wote wako hivyo huyo ana roho ya shetani tu hadi kwenye misiba ama hiyo degree yake ndio inampa jeuri .

    ReplyDelete
  6. huyo mwanamke ni selfish. kesho ukiumwa hapo atakutesa maana mtu ambaye hawezi kuonyesha ushirikiaona muogope kama ukoma.

    ReplyDelete
  7. KAMA SIO MCHAGA MPALE AU MHAYA SIJUI. MMH ILA POLE WEE

    ReplyDelete
    Replies
    1. Pole sana mkuu kwa hayo yanayokukuta, na ndio mitihani ya maisha hiyo. Lakini kama unaweza nitafute nikushauri kitu, mi ni Counseling Psychologist tutaongea vizuru. Naamini wanajamvi wanaweza kukusaidia lakini unaweza usilione jibu kwa haraka. 0717052328, asante.

      Delete
  8. Man usifanye mzaha na wazazi wazazi ndo wametoka mbali na ww yani Huyo wife yupo ki masilah zaid achana nae andika Hii tareh maana jambo linalotaka kutokea mbele lazim utasema su usicheze na mama wala baba

    ReplyDelete
  9. Asikwambie mtu!! Kila mtu anao udhaifu wake katika maisha!! Sasa kwa bahati mbaya sana huo ndio udhaifu wake huyo mwanamke ila pia ni vizuri utuelezee mambo yake ambayo ni mazuri. Kwani haiwezekani akawa ana upungufu na udhaifu wa mambo kwa asilimia 100. Inawezekana hata wewe mwenyewe unao udhaifu wako tena pengine ni mbaya kuliko hata wa kwake. Wewe mvumilie tu na jaribu kuongea nae ili muweze kuzisahihisha hizo kasoro. Kumfukuza na kutafuta bibi mwingine sio suluhisho.

    ReplyDelete
  10. Pole sana kaka mtangulize Mungu atakupa jibu michepuko cio dili

    ReplyDelete
  11. Pole sana kaka, si wote ila wanawake walio wengi ni wabinafsi sana kama anajenga hakuambii huyo ni hatari sana,,for my experience hapo hakuna love tena na inaonekana huko upande wa mwanamke kuna vikao au mawasiliano ya hayo anayoyafanya hayupo peke yake,,,huo ni mwanzo tu kaka ataleta timbwili hapo hutakuja amini,,,na wewe anza kutokuwa muwazi kwake na ikiwezekana mwambie kama anawa treat wazazi wako hivyo marufuku kuona wazazi wake wanakanyaga kwako,,,she will be aware of that bad behaviour maana sometym u need to be a bit harsh to bring peace in the house

    ReplyDelete
    Replies
    1. "Marufuku kuona wazazi wake wanakanyaga kwako" well said Dear.Wakati mwingine inabidi uwe very harsh ndo atakaa akifiki dah kumbe huyu nae siwakuchezea.
      .

      Delete
  12. hafai yuho mbinafsi na roho mbaya, ha huyo chokodinko nae mwenye mke wa aina hiyo na wewe zigo hilo unalo nyoko wewe. SIO WANAWAKE WOTE WAKO IVO TENA WENGINE WANYENYEKEVU SN KWA WAKWE ZAO KUSTAWISHA NDOA ZAO.

    ReplyDelete
  13. OA MKE WA PILI.. HUYO SI MKWELI, YUKO NAWE KIMASLAHI ZAIDI SI MAISHA YA MKE NA MUME... KUA MUANGALIFU KATIKA KUCHAGUA MKE BORA ASIWE KAMA HUYO.

    ReplyDelete
  14. Mmmm jipange kaka huyo ikatokea siku una kazi wa chochote atakutesa sana

    ReplyDelete
  15. Pole sana kaka kwa mkasa huo mbaya inawezekana ndugu zako wanakudanganya inawezekana ulikuwa ukimkosea mkeo akikushitakia kwa wazazi wako wanakua upande wako bila kujali kuwa wewe ndo mkosaji.hivyo ameamuakuwa kivyake kwa sbb na yeye hana roho ya chuma anaumia kama wewe unavyoumia.N.B mwanamke akifanya kosa ni kosa ila mwanaume akifanya kosa si kosa.Mimi mwenzako nimeacha kushitakia wakwe matatizo yangu kwa sbb wanampendelea mwanawe wa kiume hivyo kukaa kimya ni majibu tosha.

    ReplyDelete
  16. Hawa jamaa ni wepesi sana kuumia jamani mambo wawe wanafanya wao wakifanyiwa wenyewe wanaumia balaaaa tena na kufa wanaweza kufa. Ndugu kaa chini na mkeo uongee nae kwa upole lazima kuna tatizo.

    ReplyDelete

Top Post Ad