Huku Diamond Akitangaza Ndoa na Kusubiri Mtoto, Zari Na Pedeshee Katunzi Laivu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

KABAAANG! Wakati supastaa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akitembea kifua mbele huku akijinasibu kuwa anasubiri kwa hamu kupata mtoto kutoka kwa mchumba wake, Zarinah Hassan ‘Zari’, imevuja picha inayomuonesha laivu mwandani wake huyo akiwa na pedeshee maarufu Bongo, Muzamili Issa Katunzi ikidaiwa kuwa ni mtu wake wa nguvu, Ijumaa lina stori kamili.

TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, Katunzi ni mtu wake Zari kitambo kabla hata Diamond hajaanzisha naye uhusiano wa kimapenzi mwishoni mwa mwaka jana na walikuwa wakikutana mara kwa mara.“Katunzi na Zari walijuana kitambo sana. Yaani suala la Zari kuibuka Bongo na kufanya mambo yao haikuwa ishu na hata Katunzi alikuwa akiibuka Sauz (Afrika Kusini anakoishi Zari) na kuwa pamoja,” kilisema chanzo hicho.

KATUNZI ALIWAKUTANISHA ZARI NA DIAMOND
Kuonesha kwamba kina ubuyu kamili, chanzo hicho kilizidi kufunguka kuwa, hata safari ambayo iliwakutanisha Zari na Diamond kwa mara ya kwanza, mrembo huyo alikuja Dar, kumfuata pedeshee Katunzi, ndipo ‘dodo lilipomdondokea’ Diamond kama kumsukuma mlevi vile.

“Kweli Diamond ana zari kama lilivyo jina la mrembo huyo mwenye asili ya Kiganda. Siku hiyo ya kwanza kabisa walipokutana, Zari alikuwa anaibuka Bongo kuitikia wito wa mtu’we Katunzi.

NDANI YA NDEGE SASA
”Diamond alichangamkia fursa, alipoona ‘dhahabu’ inaelea ndani ya ndege katika daraja la  juu (business class), akaomba namba, akakubaliwa na ndipo wakaanza kupiga mapichapicha ya selfie ambayo yalivuja na Wabongo wakaanza kujiongeza kwani wakati huo tayari Diamond alikuwa ameshaachana na Wema Sepetu ‘Madam,” kilitiririka chanzo hicho.

PICHA ZAMSHTUA KATUNZI
Kwenye mazungumzo yake, chanzo hicho hakikusita kufunguka kuwa baada ya picha za Diamond na Zari kuanza kuvuja kwa mara ya kwanza, ilidaiwa kuwa zilimshtua Katunzi kiasi cha kumtumia ujumbe mfupi wa simu Zari kumuuliza ni kitu gani kilikuwa kikiendelea kati yake na mwanamuziki huyo.“Katunzi ilibidi amuulize Zari kuhusu picha hizo, Zari akamwambia hakuna kitu chochote ni urafiki wa kawaida, hata hivyo jamaa hakujali.

DIAMOND UPOOO!!
“Diamond kama aliingia katika himaya ya Zari pasipo kujua kuna watu wanamjua kitambo atakuwa amechelewa. Pedeshee Katunzi alimjua kitambo sana Zari,” kilimalizia chanzo hicho.

PICHA TOFAUTI ZANASWA
Mbali na kumwaga ubuyu huo, chanzo hicho kilivujisha picha tofauti katika dawati la Ijumaa zinazomuonesha Katunzi akiwa kwenye pozi la pamoja na Zari kuthibitisha kwamba wawili hao ni watu wanaofahamiana.

KWA NINI URAFIKI WA SIRI?
Ijumaa lilifanya uchunguzi wa kwa nini urafiki wa Zari na Katunzi ulikuwa wa siri na kubaini kuwa wawili hao hawakutaka watu wajue kwa sababu ambazo wenyewe wanazijua lakini kitu walichokuwa wanazingatia ni mpango wa ‘kula bata’.
Timu yetu ya uchunguzi imebaini pia kuwa, wawili hao wamekuwa wakiwasiliana mara kwa mara kupitia simu zao za mikononi, mawasiliano ambayo bado yanafanyiwa kazi ili baadaye yapakuliwe yakiwa yameiva.

KATUNZI ANASEMAJE?
Baada ya kumsaka Zari bila mafanikio, mwanahabari wetu alimvutia waya Katunzi ili kumsikia anazungumziaje ukaribu wake na Zari, alipopatikana alijibu kwa kifupi.“Zari namfahamu, kuna nini kwani?” Alihoji  Katunzi. Alipoambiwa kuwa kuna picha na habari zake kuhusu Zari alikata simu na hata alipopigiwa tena hakupokea.

KUTOKA DAWATI LA IJUMAA
Kufuatia kuwepo kwa minong’ono mingi kuhusiana na ukaribu wa Zari na Katunzi, dawati la Ijumaa linaendelea kuchimba undani wa habari hii kwa kumtafuta Katunzi, Zari na Diamond ili wote wafunguke kwa kirefu

Source: GPL
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

19 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ya walimwengo hiz habar ziliwah kuandikwa insta mpk wengn wakasema kwamba inawezekana mimba ya katunz, vyovyote vile yote heri mimba ikue salama

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani Siri ni mimba ya katunzi ndio. Mwache diamond ailee.

      Delete
  2. mbana hizo ni old news jamani!!! tafuteni habari mpya

    ReplyDelete
  3. Old news au new news angalau huyo Katunzi ameshaonekana anafananaje tusubirini sie mawifi na wakwe za Kimanyema tufanye DNA test yetu ya kiswahili, kuanzia mdomo mpaka sura. Mtoto wa hivyo huzaliwa copy na baba yake.

    ReplyDelete
  4. Kwani huyu Katunzi sio mume wa mtu huyu? Sasa mbona Team Zari na Team Diamond kila siku kumsema Wema kuwa anatembea na Mume wa Mtu sasa huyu nae ni nani mume wa mdudu?

    ReplyDelete
  5. Du! kweli niamini malipo ni hapa hapa duniani, matusi yoote alokuwa akitukanwa Wema leo tumepata majibu, na udaku pia alikuwa na upande wa Zari. kiko wapi Penny alisema kweli Nassibu alee tu mtoto si wake.

    ReplyDelete
  6. Wema malaya mmbaya anatembea na waume za watu na huyo je? mambo hadharani sipati picha walokuwa wanajipendekeza kwa bi kizee. limewashuka.

    ReplyDelete
  7. MBONA TUNAJUA KITAMBO KAMA ZARI NA KATUNZI NI WAPENZI? DOMO KAINGIA CHOO CHA WENDAWAZIMU, NA ALIAMBIWA AKAJIFANYA HASIKII WALA HAONI. NA KIKI NYIIINGI SASA ABISHE.

    ReplyDelete
  8. Malipo hapa hapa mbinguni kupumzika, domo utaweka wapi sura yako ulivyomtukana wema Jamani

    ReplyDelete
  9. The man has a family, what the fk...? Zari alihairisha safari take akashuka na Dai kwenye ndege have sex with Dai while fees days before alikuwa na katunzi, she did the shit km rafiki take huddah, kaalikwa kwenye pati ya zari kapata mshua WA nguvu kaamua kuitosa the white pati, this woman she is in business I feel sorry for mamake Dai,amehangaika na Dai sasa Ana hela anakuwa kichwa maji,poor boy,ILA dunia itamfunza

    ReplyDelete
  10. Zari All Newz Party......Kimenukaaaa

    ReplyDelete
  11. Mbona habari nyingi tena kuna mafuriko na vifo andikeni hayo acheni kuchokonoa maisha ya watu

    ReplyDelete
  12. hapa ndio mtachangia mpaka basi lakini yakitajwa mafuriko au mambo ya msingi wote kimyaaaaaaaa jmn watanzania tubadilike kdg hii nchi haitaendelea kwa style hii ya maisha kwa kweli,
    angalieni post za mafuriko ya mvua km kuna mtu kachangia hata mmoja kule..lakini wema,diamon sijui zari weee kila mtu atashuhulisha akili andike kitu..too bad.

    ReplyDelete
  13. shuuuuu, siri imefichuka, tukisema ooh mnamuonea wivu zari. kiko wapi show off nyiiingiii kumbe xxx aibu yao aibu yenuuuuuuu?????

    ReplyDelete
    Replies
    1. Aibu yako wewe na malaya wenzako. Kwani watu wakipiga picha pamoja lazima wawe wanatiana?? Mbona huyo Wema wenu haishi kupiga picha na Idrisa mara Ommy mara JB na wengine kibao. Ina maana wanamdinya?? Pumbaf wee. Kanye kuleeeeee. Aibu yako wewe na timu Wema mnaogawa uroda kama ubwabwa wa maulidini. Mshafulia kubalini yaishe.

      Delete
  14. goons wa diamond watafanya mbaya.tumechoka na udaku tunataka real story aseme kama anatoka na katunzi diamond ajikatae jembe letu.tamaa ikizidi waachie wenyewe.mwana unanyota tuu.katunzi sifa tuu.bongo tungekuwa marekani gunsnjenje haaaiseee.pangechimbika. kisa we kaaa.

    ReplyDelete
  15. Wakati mlipokuwa mnamsema Wema mlikuwa hamuoni kuwa issue ni nyingi ila kwa Zari ndio issue za kuandikwa ni nyingi? Akwendreee huko huyo Mule na atamponza Diamond na biashara zake za ajabu ajabu. Shauri yake huyo Diamond kama kanogewa na pesa za sembe atakiona cha moto.

    ReplyDelete
  16. Kumbe huyu Demu ni CHECHEE in Diamond voice, hahahahaaaaaa

    ReplyDelete
  17. Katunzi meenyewe minyepaaa hanalolote

    ReplyDelete

Top Post Ad