January Makamba Azomewa Jimboni Kwake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mheshimiwa January Makamba, Mbunge wa Bumbuli, leo amekumbwa na kitu ambacho hakukitarajia katika maisha yake baada ya kukutana na hasira za wananchi wake jimboni.

Mbunge huyo ambaye sasa yuko katika ziara jimboni kwake kwa zaidi ya siku tano, amekuwa anatembelea baadhi ya vijiji na maeneo katika kutimiza ahadi zake na ilani ya chama chake.

Ziara ya Mh. January ilianza kwa kasoro ambazo wananchi wengi wamekuwa wanaziita usanii, wengi wanalalamikia utaratibu wa ziara zake jinsi unavyoenda, kwanza amekuwa akiitisha mikutano mapema na yeye kutokea akiwa amechelewa, halafu akifika kwenye mkutano hataki kuulizwa maswali wala kuchukua maoni ya wananchi kwa kisingizio cha muda kuisha, katika mikutano yake amekuwa akiongozana na viongozi wa chama wilaya na wale wa halmashauri ambao pia wamekuwa wakitumia ubabe kuendesha vikao na mikutano, viongozi wote wanalazimishwa kumsifia kila wanapopewa nafasi ya kuongea.

Ziara ya Mh. January imekuja baada ya yeye kutoonekana jimboni kwa muda mrefu na wananchi kuona kama aliwatelekeza, wengi wanadai hawajawahi kumuona mbunge toka achaguliwe na leo amekuja kisa kuna uchaguzi unakuja na ameona upinzani umekuwa mkubwa kwa nafasi yake.

Leo Mh. January wananchi wa kata ya Mgwashi ndio waliamua kumtolea uvivu baada tu kufika kwenye mkutano na kuanza kuzomewa na kurushiwa maneno na wananchi, wananchi hawakumruhusu kuongea na walimuambia aondoke hawataki kumuona kwani katika miaka yote mitano aliyokuwepo madarakani amekuwa mbunge wa mitandao na ameshinda kuwa karibu na wananchi waliomchagua, kulitokea vurugu kubwa sana leo mgwashi na viongozi waliokuwa katika msafara wake wengi walipata wakati mgumu sana kutuliza wananchi hao wenye hasira.

Wananchi walimuambia wazi kwamba hawataki kumuona na hajalifanyia jimbo lao lolote zaidi ya kuleta migogoro jimboni na kuwaletea wananchi maisha magumu, vurugu hizi zilidumu mpaka saa 2 usiku na kulikuwa na zomeazomea mpaka mwisho, wananchi wanasema WANATAKA MABADILIKO.

Kuna dalili kubwa sana kwamba Mh. January ana upinzani mkubwa sana jimboni kwake kupitia UKAWA lakini hata ndani ya CCM kwani mpaka sasa wameshajitokeza wagombea wengi kulitaka jimbo hilo, badhi ya wagombea hao ndani ya ccm ni pamoja na mwandishi wa habari wa raisi PREMI KIBANGA, MNEC wa Wilaya Lushoto NAJIM MSENGI na Bwana Abdul Kanik, upande wa UKAWA wengi wanatajwa na kwa hali inavyoendelea UKAWA unaamini una nafasi kubwa kwani umekuwa unakuwa jimboni humo kwa kasi.

Mh. January analalamikiwa kwa kutokuwa karibu na wananchi, uamuzi wake wa kufunga kiwanda cha chai ambacho ndio tegemeo pekee la wakulima kwa sababu za kutoelewana na mwekezaji na uongozi wa kiwanda, kushindwa kutatua mgogoro wa kidini ulionzishwa na baba yake dhidi ya bakwata.

By busaraza2015/JF
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. aseme pia wametumwa na lowassa

    ReplyDelete
  2. Na bado natamani tuwapige na mifuko yenye mavi wakione cha moto.,mnapewa ubunge mnakaa mjini kuuza sura na kununua machangu.,kipindi hiki mambururaaz wote km we kipara ni mawe tu.,mnaleta bongo muvi kwenye utumishi???pumbaaavu na bado....,we admin wewe???acha ushoga nawewe ndo msg zenyewe...,

    ReplyDelete
  3. Halafu anataka urais??mandumilakuwili km hawa dawa yao ndio hiyo na atazomewa sana maana kote wamejaa wamaotaka maendeleo sio bongo fleva km wewe

    ReplyDelete
  4. kama jimboni kwake tu hakubaliki je huo urais itakuwaje, DOGO acha makubwa wakati madogo yamekushinda

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hana tofauti na padri Slaa aliyeshindwa kuchunga kondoo 400 za bwana kanisani halafu anataka aongoze nchi yenye watu 50,000,000!Ni aibu sana yaani sijuhi hawajielewi,au mazuzu!

      Delete
  5. TAMAA NDO ZILIZOWAJAA HAO VIONGOZI MCHWARA, WANAFIKIRI WATZ NI WAJINGA, WANGEMPIGA NA MAYAI VIZA KABISA PUMBAVU ZAKE.

    ReplyDelete

Top Post Ad