Lemutuz Apinga Matokeo ya Tuzo za Watu Adai Matokeo Yamepangwa..Ali Kiba Hawezi Mshinda Diamond Kwa Kupendwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kama mjuavyo hakuna tunzo inayo kosa mikasa na maneno na hii uonesha jinsi tunzo zinavyo wagusa wengi!

Na Tunzo iliyokuwa ina wagusa wengi ni tunzo ya msanii wa kiume anaye pendwa na wengi ambayo imekwenda kwa msanii Alikiba!
Baada ya utoaji wa tunzo huo wengi wamesema na kunena lakini leo hii kuna kitu kipya kimezuka ambacho kinaweza kuwa kivutio kwa wengi na wengi watatamani kujua kilicho nyuma ya haya yote!

Mh Lemutuz au Sauti ya Umeme amesema wazi kabisa kwenye Tunzo za watu haki haikutendeka kabisa na hakuna msanii anayependwa Tanzania zaidi ya Diamond!

LEMUTUZ AMEANDIKA HAYA KUHUSU TUZO HIZO:

Well, thank "Tuzo za Watu" for the best Show but I have a big problem kuamini kwamba1. Millardayo hakupata zawadi zote isipokuwa ya Blogu tu 2. Ali Kiba ameshinda Tuzo ya Mwanamuziki anayependwa against The King Of Pop in East Africa 3. Mzee Majuto kashindwa kupata hata zawadi moja.....nilichokiona ni Manouver and Manipulation by somebody very powerful behind the scene anayetaka ku create a balance katika Field ambayo ni unbalanced by Nature and TALENT in the end ni kuvuruga competititon ambayo tayari ipo na kuwakatisha tamaa waliofanikiwa kwa VIPAJI VYAO...the Idea inatakuwa kuwa ni kupiganisha Vipaji uwanjani sio ku balance the Field from somebody's Office....mapokezi ya Diamond leo Mwanza na LONDON WIKI ILIYOPITA ni EVIDENCE ya kutosha kwamba HAKUTENDEWA HAKI NA TUZO ZA.LEO.....ninawaheshimu sana watayarishaji wa Show ya leo lakini NAOMBA KUKUBALI KUTOKUBALIANA NANYI na we remain kool SIAMINI KWAMBA MATOKEO YA LEO YALIKUWA FAIR na nitashukuru sana kuona process iliyotumika kufikia matokeo ya leo!

...UPDATE: well nimesoma arguments nyingi against my prior post kuna wachache sana wanaojaribu ku make a sense lakini at the end of the heart of all the TRUTH STANDS alone kwamba kulikuwa na unfairness I mean eti KING MAJUTO ana mpinzani Tanzania? Please eti Millardayo ana mpinzani Tanzania? Diamond Platznumz ana mpinzani Tanzania? hahahahahahah that is a joke infact the biggest joke of my life...I mean wananchi wanajaa kwenye Show za Diamond kuliko za Wasanii wote Tanzania lakini hawakumpigia kura? hahahahha ninasema that is.the biggest joke of all the times Diamond ana followers wengi Instagram na FACEBOOK kuliko MTANZANIA YOYOTE ALIYEWAHI KUISHI.HAPA NCHINI lakini hawakumpigia kura? hahahahahha kuna mtu hukoooo anataka niamini that! hahahahah wanannchi wamekubali kununua meza kwa Shillingi Millioni Tatu kumuona Diamond lakini hawakumpigia kura? Ipi ni kazi ngumu kupiga kura kwenye simu au kulipia meza Shillingi Millioni Tatu?......I mean hata aliyetaja washindi alikuwa anatetemeka kutaja kushindwa kwa Diamond WHY? hahahahaha baada ya Category ya Diamond kupita ilikuwa ni rahisi kutabiri the rest of the TUZOS kila mtu alijua mapema kuwa Millard ameshinda blog WHY?....KIPAJI kinatakiwa kushindanishwa na KIPAJI sio otherwise....sina muda wa kujibu low arguments za Yanga na Simba eti mtumzima.na akili zako.unaweza kusimama na kusema Mwanamuziki anayependwa Tanzania sio Diamond eti kuna mwingine! hahahahahahahha namshukuru Mungu kwa kunijalia kwenda Shule niliyoyaona leo ni aibu tupu na ndio mwanzo wa kuua vipaji soon tutaanza tena kuwarudia kina Kandabongo Man ambaye huko kwao huwa.anapiga bure kwenye harusi...sio kosa la Diamond kwamba amewaacha wasanii wenzie maili 20 ni kosa la KIPAJI CHAKE kipaji hakitengenezwi na TUZO ila kukubalika na wnanchi ninasema DIAMOND NDIYE MWANAMUZIKI ANAYEKUBALIKA.KULIKO WOTE TANZANIA NI FACTS NA MIFANO IPO WAZI ni maoni yangu kama huyakubali andika FACTS sio ushabiki wa Yanga na Simba! - le Mutuz

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Lemutuz unatuletea yale ya Mrema enzi zile za NCCR alipokuwa anabebwa na wanachama wake juu juu, aliposhindwa kupata urais nayeye kama wewe hakuamini matokeo........hebu kubali mabadiliko mzee, TATIZO NYOTA!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. Kabla hujalalamika mukubwa, hebu jiulize wewe mwenyewe ULIMPIGIA KURA? Inawezekana watu hawakupiga kura, maana sio wote wanaozijua hizo tuzo za watu, hazikufanyiwa promo kiviiiiile. Mimi binafsi nilishtukia wakati zimeshafikia tatu bora!

    ReplyDelete
  3. DOGO ANUDHI WATU KWA MASHAUZI NDIO MAANA WATU WANA HASIRA NAYE. KWA MAELEZO ZAIDI NENDA KWENYE BLOG YA MANGE KIMAMBI IITWAYO U-TURN,KACHAMBULIWA VYA KUTOSHA KWAMBA MIENENDO YAKE INAFANYA WATU WAMCHUKIE PAMOJA NA KUWA ANA KIPAJI HASWA. ALI KIBA YUKO POA NA WATU,HANA MAKUU,KWA LUGHA YA MALKIA NI YUKO HUMBLE NA WATU,KWA MAELEZO ZAIT GOOGLE U-TURN.BLOGSPOT.COM

    ReplyDelete
  4. Huyu Le Mutuz haumwi lkn, haya mwenye uwezo wa m3 kulipia meza wakupigie kura kisha uliodhulumu buku 3 kwenye cmu wampigie mwengine.... meza za m3 zilikuwa ngapi na waliodhulumiwa bk 3 walikuwa wangapi?
    then mashabiki wa Madam waongeze upande mwengine, na baadhi ya wale wa kidoti.... kwa mbaali wanaomkubali dimpo na kuamini D anabeef nae wasogee upande huo mwengine bado tu unataka kuamini kashindwa kumagumashi..... mtizame mnapoteleza na sio kuwa na kiburi tu kwa kuwa mimi fulani kwenye account zangu nina idadi kubwa... mavi ya mbuuuuzi!!

    ReplyDelete
  5. Hivi huyu mtu anayejiita Le Mutuz hana career nyingine yoyote ya maana katika maisha yake zaidi ya kukalia haya majungu majungu ya kitoto????? Mbona anatuambia amekaa na kusoma Ulaya na sijui an Degree Mbili sijui Tatu sasa mbona kila tunachokiona na kukisikia kutoka kwake ni majungu na upambuva mtupu. Sasa hizo Degree na majidai mengine kutoka kwake yanawasaidia watu wengine nini???? Please, Blogger usiwe una post habari zake za maudhi hapa kwenye Blog hii......hatumtaki kabisaaaa humu ndani, by the way si anayo blog yake sasa humu anafanya nini?????? Kha!!!!

    ReplyDelete
  6. hapo ndo ana digree 3, je angekua na 1. sijui angesema nini. kweli ukizaliwa mjinga hata ufanye nini.

    ReplyDelete
  7. Watu tulipiga kura mara 3 3 kama hatuna akili nzuri vile. Nilimpigia Madame kura za tuzo zote alizokuwa anawania, na alipaswa ashinde zote zile kama hiyo moja alishinda. Na Ali Kiba pia nilimpigia kura kwa sababu ya kumuumiza Diamond tu. Yes mie ni mwanamke na wanawake wengi tulihamasishana tumtie adabu huyu Diamond, na ni mara yangu ya kwanza kupiga kura. Na kura za KTM pia nitampigia Ali Kiba categories zote anazowania.

    Yeye Lemutuz na Diamond waende wakaombe kura kwa wanawake wa Uganda hukoo, hapa hawana soko. Wanawake tukiamua tunaweza, sasa tuone hizo levels baby levels zitaishia wapi.

    ReplyDelete
  8. Mutu kubwa akili ndogo huyu le mutuz star wa kuomba kupiga picha na wasichana hebu jitambue uzee unakujia lkn unajidai kuupa kisogo.Wacha majungu mzee ww.Gadem super mburulaz

    ReplyDelete
  9. Kweli Domo amepaniwa, kwa mtazamo wangu naona Domo ni kama Mr John Smith, kesha pata hajui tena alikotoka iliyobaaki ni dharau kwa wa Bongo

    ReplyDelete
  10. Tatizo jamaa bwabwa,majungu na unafki Tu umemjaa,anataka atupanngie matokeo, see umeingia ktk mioyo yetu ukajua tuna mpenda nani? Tatizo misifa and his days are number, yeye Dai si ananua mashabiki , na bado, mm mwenyewe nilikua namzimia Sana Dai, skendo, dharau na mashauzi,hasa alipo iponda kili award mikaona Hana mama tena, walio mpandisha wata mshusha tena very soon

    ReplyDelete
  11. Mimi sina team yoyote ni mtanzania lakini naishi nje ya Tanzania. Kusema ukweli watu tumechoka mijigambo ya Diamond na bado tunaendelea kumshusha atambue heshima , majigambo , dharau na kauli zake ni vitu vinavyoweza kumpandisha na kumshusha pia. Staa yeyote ili akubalike anatakiwa ajue kinachofaa kuposti kwa fans wake. Kumbuka anayejikweza atashushwa na anayejishusha atakwezwa

    ReplyDelete

Top Post Ad