Madansa Wanne wa Diamond Wamejenga Nyumba Kupitia Muziki Wake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Si Diamond pekee anayenufaika na muziki wake – hata madensa wake pia.
Diamond amesema madansa wake wanne tayari wamefanikiwa kujenga nyumba zao kutokana na kipato wanachopata.

Akiongea na gazeti la Mwanaspoti, staa huyo amesema amekuwa akiwashauri madansa wake mambo mazuri ya kimaisha ili kuwajenga.

“Ni kama kaka zangu na ninawapenda sana kwani tumetoka nao mbali na wanajua kuwa tunafanya kazi pamoja kutengeneza maisha hivyo ni kama ndugu zangu na tunasaidiana kwenye kila jambo ukizingatia kuwa kile tunachokipata tunagawana,” alisema Diamond.

“Kwa kweli najitahidi sana kuwaambia hasa kuhusiana na masuala ya kimaisha, nahusika katika maisha yao ya kila siku na nijuavyo mimi nikikosea tu mmoja akapotea kundi langu litakuwa limeharibikiwa maana kila mtu namtegemea kwa upande wake. Kwa sasa wamejenga nyumba zao na wanaendelea vizuri kimaisha hilo ndilo sharti langu lazima wafanye mambo ya maendeleo kwa kile tunachokipata.”

Bongo5
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hongera Domo

    ReplyDelete
  2. BIG UP DIAMOND. WANAOSEMA WASEME USIKU WANALALA!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad