Maelezo Ya KINA Ya Edward Lowassa Kuhusiana Na Sakata La Richmond, Afya Yake, Utajiri Wake Na Kwa Nini Alikuwa Kimya Kwa Miaka Yote 7

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Hatimaye  Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, jana alivunja ukimya wa muda mrefu alipofanya mahojiano ya ana kwa ana na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari.

Katika mkutano huo,Lowassa aliitumia nafasi hiyo kutangaza msimamo wake wa siasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Lowassa aliitumia fursa ya mahojiano hayo, yaliyofanyika nyumbani kwake eneo la Area C mjini hapa, kuwaeleza wahariri kuwa hana mpango wa kuhama CCM licha ya kuwapo shinikizo la chini kwa chini la kumtaka aondoke na kwamba wale wote wanaomtaka au wanaotamani aondoke, wanapaswa kuondoka wao.
 

 Sakata  La  Richmond:
Kuhusu sakata la Richmond, ambalo lilimfanya ajiuzulu uwaziri mkuu, Lowassa alisema tatizo kubwa halikuwa kuhusu mitambo hiyo ya umeme ila uwaziri mkuu.

“Ajenda haikuwa kuhusu Richmond, ila uwaziri mkuu ndiyo maana niliwaachia. Tunajifunza  nini katika hilo, wakubwa wawili wa Marekani, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje (Hillary) Clinton na Rais wake (Barack) Obama, wote wamekuja Tanzania na wamethibitisha kuwa ile mitambo ni mizuri. Lakini jingine tulilojifunza katika ubishi ule umeisababisha nchi hasara ya Dola 120 milioni,” alisema Lowassa.

“Moja ya ushauri wangu wakati ule ilikuwa ni kutaka kuvunja mkataba wa Richmond nikaita wataalamu, nikawaelezea kuhusu habari za magazeti kuwa zinasema hawa jamaa (Richmond) hawana fedha, hebu angalieni, nikaita wataalamu na mwanasheria mkuu, nikawaambia kuna hii habari kuweni makini.
 
"Pamoja na hayo nikaweka kwa maandishi kwa mwanasheria mkuu, pia kulikuwa na timu ya mashauriano ya Serikali iliyokuwa chini ya makatibu wakuu nao walikuwa na vikao vyao, ilikuwa inaongozwa na (Katibu Mkuu Wizara ya Fedha (Gray Mgonja) nao wakakutana chini ya Katibu Mkuu Kiongozi na baada ya kukutana wakatoa uamuzi ambao sina haja ya kuujadili. Lakini ubishi ule umetugharimu Dola 120 milioni."

“Nilipotaka mkataba uvunjwe nilikuwa nimetoa uzoefu wangu kwani kabla ya kuwa waziri mkuu nilikuwa nimekuwa waziri wa maji na mifugo ambako nilivunja mkataba wa kampuni ya Kiingereza iliyokuwa imewekeza katika mradi wa maji Dar es Salaam ya City Water.

“Chini ya uongozi wa Rais (Benjamin) Mkapa tukagundua hawa jamaa (City Water) ni matapeli…tulifanya kikao saa tisa alasiri, tukachukua kibali cha kumkamata yule Mzungu wa City Water na tukamfukuza akaondoka siku hiyohiyo kwa ndege kurudi kwao, tulifanya saa tisa alasiri ili asiende mahakamani kupata zuio, kwa hiyo tulivizia muda huo ili asije kwenda kupata zuio."

Nini tofauti ya Lowassa nje ya Serikali na ambaye angeendelea kuwa waziri mkuu na kisha kugombea urais?

 “…Naamini kuwa kama tungeanza kwa kasi ile tuliyoanza nayo nikiwa waziri mkuu, sasa ningepita napunga mkono ningepata kura zote… lakini kinachonisikitisha tumekuwa hatufanyi maamuzi magumu au rahisi, kila kitu kinakwenda legelege.
 
"Rais amefanya jitihada kubwa, lakini kuna mambo katika nchi hayaendi, matokeo yake Uganda, Kenya na Rwanda zinatupita sasa, haifai, lakini nawaachia uhondo nitaelezea vizuri Jumamosi, Arusha.”

Kwa  nini  Alikuwa  Kimya  Kwa  Miaka  Yote 7?
Lowassa aliyejiuzulu uwaziri mkuu mwaka 2008 kutokana na kashfa ya mtambo wa kufua umeme wa Richmond, alisema kimya chake baada ya tukio hilo kilitokana na siasa nyingi za uhasama na kutishiana.

“Kwa miaka saba, niliona ni hekima kunyamaza, askofu mmoja alinifundisha kuwa ukimya ni hekima kutoka kwa Mungu. Nilichagua kuwa kimya.
 
"Nilinyamaza kwa sababu ilikuwa salama kunyamaza, ningezungumza ningeweza kutibua mambo kwenye nchi na kusababisha mambo ambayo hayapo.

“Nilinyamaza ili kuipa muda Serikali ifanye kazi yake.... sikupenda kuzungumza kwa sababu ya siasa nyingi za uhasama na kutishiana kwingi, kuna kusingiziana kwingi, kufitiniana kwingi.

"Kukaa kimya ni jambo gumu sana kwa mwanasiasa, lakini nashukuru Mungu niliweza hilo,” alisema Lowassa ambaye Jumamosi atatangaza nia ya kuwania urais mjini Arusha.
 
Ni Kweli  Afya  Yake  Ni  Mbovu?
Alipoulizwa kuhusu madai kuwa afya yake inaterereka, alisema anaamini yupo fiti na akashauri wagombea urais wote wakapimwe.

“Hata nikikimbia kilomita 100 watasema mimi mgonjwa. Hivi karibuni nilitembea kilomita tano na albino jijini Dar es Salaam, kuna watu wakasema nimechoka sana, nimepata ‘stroke’ na nimekimbizwa Ujerumani kutibiwa, huo ni upuuzi mtupu.
 
"Kuna chuki imeingia katika siasa zetu na kutakiana mabaya. Afya ni neema kutoka kwa Mungu tu. Napenda kuwahakikishia kuwa nipo fiti na nipo fiti na kwa lolote.
 
"Nadhani ni wakati sasa kwa chama chetu waweke utaratibu wanaogombea nafasi hii ambayo nitaitangaza Jumamosi, tukapime wote afya na mimi nitakuwa wa kwanza kujitokeza kwenda kupima.

“Twendeni tukapime tuone nani mgonjwa. Tuonane kwenye uwanja wa mapambano katika mchakamchaka wa maendeleo, ninajua nitawashinda kwa mbali,” alisema.

Utajiri wake
Alipoulizwa ana utajiri kiasi gani na fedha anazochangia kwenye harambee makanisani na misikitini zinatoka wapi, Lowassa alisema anatamani angekuwa tajiri, lakini anachukia umaskini.


“Tatizo siku hizi kuna maneno mengi, kila nyumba nzuri wanasema ya Lowassa. Mimi nina nyumba chache na ng’ombe kati ya 800 na 1,000.
 
"Kwetu Umasaini unapokuwa kiongozi unapewa ng’ombe ili usipate taabu kwa ajili ya kuwakarimu wageni wanapokuja wala usiwe ombaomba au usichukue rushwa. Lakini kama kuna mtu mwenye shaka na utajiri wangu aende Sekretarieti ya Maadili kule ataona kila kitu,” alisema.


“Nachukia umaskini, napenda utajiri, natafuta uongozi wa nchi hii ili kuwasaidia Watanzania kuwa matajiri na si kukumbatia umaskini. Hii kudanganya watu kwamba nikiwa maskini ndiyo nafaa kuwa kiongozi ni ujinga ambao inabidi tuuache.
 
"Nataka watu wawe matajiri, tuache kuwabeza matajiri, matajiri wawe ni mfano kwa wengine, watu kama (Reginald) Mengi, (Said) Bakhressa na (Nazir) Karamagi wanatakiwa kuwa mfano kwa wengine, tungekuwa na watu kama hawa 20,000, nchi hii ingekuwa haikopi nje. Naukataa umaskini na nauchukia umaskini. Nakataa umaskini na ninataka watu wanihukumu kwa hilo,” alisema.

Kuhusu kushiriki harambee nyingi na anakopata fedha alisema: “Sina fedha ila nina marafiki wengi, nikipata mwaliko wa kuchangia nawatafuta marafiki zangu wanachanga. Mfano ‘juzi’ nilipomwakilisha Makamu wa Rais mjini Arusha, marafiki zangu walichangia Sh100 milioni, Makamu wa Rais alichangia Sh10 milioni na watu wa Arusha wakatoa Sh100 milioni. Hizo hazikuwa fedha zangu, ila ni watu walichangia.
 
"Nafurahia kufanya harambee, harambee zangu zinasaidia misikiti, makanisa na shule, hivi ni vitu vya maendeleo ya watu, nawashauri na wabunge wafanye hivyo kwenye majimbo yao. Hata shule za kata zilichangiwa kwa harambee, tusionee aibu ni jambo jema,” alisisitiza.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. huyu jamaa mgonjwa kweli, sidhani kama atakuwa hai baada ya miezi sita ikulu, makamu wake ajiandae kuongoza nchi akifa

    ReplyDelete
  2. Bull shit! Yaani umeawaona watanzania wote ni ma-brainless hawana memory yoyote! Kwa Richmond ilikuwa uzushi tu? Na hao waandishi wa habari nao matoyoyo wanakariri kama kasuku kila unachoongea bila kukusaili! Dah...Tanzania na Africa bado sana maana hakuna anayewajibika ila wananchi ndo mnawafanya kuwa ngazi za kupandia.

    ReplyDelete
  3. huyu jamaa cjui kwanini analilia uraisi, inabidi tumuulize hilo kwanini analilia sana kwenda ikulu? kuna nini kule? kama cyo kutaka kulinda utajiri wake ninini tena? alikuwa waziri mkuu takribani miaka mitatu? mbona mambo yalikuwa yale yale? watanzania aamkeni?

    ReplyDelete

Top Post Ad