Majambazi wavamia nyumba ya Alikiba na kupora mali na kujeruhi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Majambazi waliokuwa na silaha usiku wa kuamkia leo yamevamia nyumbani kwa Alikiba na kupora mali mbalimbali.

Kwa mujibu wa mdogo wake, Abdu Kiba, majambazi hao waliokuwa zaidi ya 15 waliivamia nyumba wanayoishi pamoja na Ali iliyopo Kunduchi jijini Dar es Salaam mida ya saa tisa za usiku.

Abdu amedai kuwa wakati wa tukio hilo hakuwepo nyumbani na alipigiwa simu na kaka yake akimuomba msaada kwa kudai kuwa nyumba yake imevamiwa. Kutokana na simu hiyo, Abdu alirejea nyumbani haraka na bahati nzuri wakati akielekea nyumbani alikutana na gari la polisi alilolipa taarifa aliyopokea kutoka kwa kaka yake na kuongozana nao.

Abdu anadai majambazi hao waliokuwa wamebeba silaha mbalimbali zikiwemo mapanga na visu, yalivunja milango ya nyumba hiyo na kupora mali mbalimbali za thamani na kuwajeruhi baadhi ya ndugu zake wanaoishi hapo.

Pia yanadaiwa kumpiga na kumtesa mlinzi wa nyumba hiyo yakimtaka ayapeleke kwenye chumba anacholala Alikiba.

Hata hivyo hayakuweza kumpata Alikiba kwakuwa yaliyoeshwa kwenye chumba cha Alikiba ambaye muda huo hakuwemo. Alikiba alikuwemo ndani ya nyumba hiyo lakini kwenye chumba kingine.

Majambazi hao walifanikiwa kuiba vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na pesa taslimu shilingi milioni mbili na nusu. Picha zilizochukuliwa baada ya tukio hilo zinaonesha milango kadhaa ya nyumba hiyo ikiwa imevunjwa na uharibifu mkubwa unaonekana kufanywa.

Abdul Kiba amepost picha Instagram na kuandika: Tunamshukuru M/mungu tupo salama.”

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Pole sana Kiba!

    ReplyDelete
  2. Thank God live is more important than properties.Utabarikiwa zingine

    ReplyDelete

Top Post Ad