Mapinduzi ya Burundi: Rais Pierre Nkurunziza Ahojiwa na Kituo cha habari cha Burundi RTBN.......Asema Yupo Tayari Kumsamehe Mwanajeshi Atakayesalimu Amri

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kituo cha habari cha Burundi RTBN kimemhoji rais Pierre Nkurunziza kwa simu mwendo wa saa sita.

Katika  mahojiano  hayo  ambayo  Shirika la habari la Reuters lilifanikiwa  kuyanukuu, Rais Nkurunziza amesema  yupo  tayari  kumsamehe  mwanajeshi  yeyote  atakayekubali  kusalimu  amri.

''Ninalishtumu kundi lililopanga mapinduzi, nawashkuru wanajeshi wanaorudisha hali ya kawaida na namsamehe mwanajeshi yoyote ambaye yuko tayari kusalimu amri''.Alinukuliwa akisema.

Muda  mfupi  baada  ya  mahojiano  hayo,  vita kali  ya  majibizano  ya  risasi  iliibuka  karibu na kituo hicho cha habari baina  ya  wanajeshi  watiifu  kwa  rais  huyo  na  wale  waliotangaza  kumpindua.

Hali  hiyo ilikilazimu  kituo  hicho  kuzimwa  na  kisha  kufunguliwa  tena  baada  ya  mapigano  kuisha

Jenerali anayeunga mkono jaribio hilo la mapinduzi amekiambia chombo cha habari cha AFP kwamba wanajipanga kukiteka kituo hicho cha habari cha RTNB  kilicho  chini  ya  udhibiti  wa  wanajeshi  watiifu  kwa  Rais
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. huyu nkurunzinza kwa nini sio muelewa awachie wananchi wachague wanaemtaka

    ReplyDelete
  2. Tamaa ya uongozi kwa sisi Wa Afrika, tungoje tuone ya kwetu Tanzania itakuwaje

    ReplyDelete
  3. Tamaa zake zitamponza , wamezoea kumwaga damu za watu

    ReplyDelete
  4. ANATAKA AWE KAMA GHADAF, MWISHO WA YOTE KABURI LINAMUITA

    ReplyDelete

Top Post Ad