google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Mengi akomalia Ikulu Kuhusu Kauli zinazoongeza Hofu ya Usalama wa Maisha yake | UDAKU SPECIAL

Mengi akomalia Ikulu Kuhusu Kauli zinazoongeza Hofu ya Usalama wa Maisha yake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MWENYEKITI wa makampuni ya IPP, Regnald Mengi ameendelea kung’ang’ania kuwa, kauli zinazotoka Ofisi ya Rais Ikulu, zinazidi kumpa wasiwasi na hofu kubwa katika maisha yake. Anaandika Sarafina Lidwino

Mengi ameeleza wasiwasi huo leo wakati akizungumza na wanahabari ofisini kwake, na kueleza masikitiko yake juu ya kauli za dharau na dhihaka zilizotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Salva Rweyemamu.

Mengi amesema kuwa, Aprili 17 mwaka huu, alizungumza na waandishi juu ya hofu yake, baada ya kupata habari kutoka kwenye gazeti la Taifa Imara la Machi 23 mwaka huu.
Habari hiyo iliosema, “Zitto Kabwe amchongea Mengi kwa Kikwete kwamba ndiye kinara wa kuihujumu Serikali yake.”

Mengi ameongeza “habari hiyo iliendelea kusema kwamba, nimeapa kumshuhgulikia Rais Jakaya Kikwete kwa nguvu zangu zote amalizapo muda wake wa urais, na kwamba Rais aliapa kupambana na mimi.

Amesema kauli hizo dhidi yake zilimshtua sana, na kwamba yeye hakuzitoa, hivyo kauli ya Kikwete ya kutaka kupamba naye ilizidi kumpa hofu ya usalama wa maisha yake.
Kutokana na mwingiliano wa kauli hizo, pia nililaumu sana Kurugenzi ya Mawasiliano- Ikulu na Idara ya Habari Maelezo kwa kukaa kimya zaidi ya wiki tatu bila kutoa ufafanuzi wowote katika jambo hili linalomhusu Rais na kuacha habari hizo kusambaa,” ameeleza Mengi.
Amedai kuwa, katika majibu ya Rweyemamu, alisema “Rais hakuwahi kuwa na mawasiliano yoyote na Zitto Kabwe kama ilivyoelezwa.”

“Hivyo, katika majibu yake Rweyemamu, alidai kuwa, hakufanya lolote eti kutokana na kuwa na majukumu mengi na alipuuza habari hizo kwa sababu aliziona ni jambo dogo na ni la upuuzi,” ameeleza Mengi.
Kwamba Rweyemamu kwa jeuri, aliongeza kuwa, alimshangaa sana kwa kutokutoa taarifa latika kituo chochote cha polisi kuhusu hofu ya maisha yake.
Kauli hizo, zinaongeza hofu ya usalama wa maisha yan
gu. Jambo hilo sio dogo la kupuuzwa kama linavyodaiwa. Rweyemamu hakutumia busara katika majibu yake, kutokana na kiti chake na heshima aliyonayo, alipaswa kutoa kauli nzuri na sio kuzidi kunipa hofu.
Na kwa upande wa Rais, mimi sina ugomvi naye na ninaamini yeye pia hana tatizo na mimi ila kauli za huyo mtu ndizo zinanipa shida,” amesema.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. MAISHA MATAMU BWANA ASIKWAMBIE MTU. PIGANIA UHAI WAKO DR.

    ReplyDelete

Top Post Ad