Mkurugenzi Mkuu Vodacom aliyejiuzulu Aula Qatar ......Mitandao Yahusisha Kujiuzulu Kwake na Kashfa ya Upotevu wa Bilioni 700 za Kitanzania

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Aliyekuwa  Mkurugenzi  mkuu  wa  Vodacom  aliyejiuzulu hivi  karibuni  Rene Meza amepata shavu katika kampuni nyingine ya mawasiliano  nchini Qatar ijulikayo kama Ooredoo Mynmar kuwa Mwenyekiti  mtendaji  wa tawi la Mynmar.

Aidha, taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana  na kampuni hiyo imesema kwamba Rene Meza atachukua nafasi ya  Ross Cormack ambaye anatarajiwa kuachia nafasi hiyo mwaka huu.

Kwa mujibu wa mtandao wa Afrika Kusini umebanisha kwamba Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom amejiuzulu  ili kufanya kazi nyingine.

Hata hivyo mitandao ya kijamii  mbalimbali  nchini Tanzania imehusisha  kuondoka kwake  na kashfa ya upotevu wa takribani  bilioni 700 fedha za kitanzania ambazo ni sawa dola za Kimarekani  milioni 350.

Taarifa  hizo  zinaarifu  kuwa  bwana Meza alikuwa kwenye  ‘kitimoto’ cha maofisa wa juu wa Kampuni hiyo akihusishwa na kashfa ya kupokea dola milioni 5 kutoka kwa Mmiliki wa Shivacom,Tanil Somaiya ambaye  alimpa  ili  kumziba mdomo   kutokana  na  kashfa   ya  uzalishaji, usambazaji na uuzaji  wa  vocha  bandia  zilizokuwa  zinajulikana  kwa  jina  la  "Jero jero".

Rene Meza alijiunga na Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom mwaka 2011 akitokea kampuni ya Bhati Airtel Ltd ya nchini Kenya.

Ifuatayo  ni taarifa iliyotolewa na kampuni ya Ooredoo Mynmar ya nchini Qatar.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nchi ya wezi hakuna legal mambo yenyewe ni illegal kwenda mbele wabongo tutasubiri sana maendeleo ya kila mmbongo kwa speed hiyo

    ReplyDelete

Top Post Ad