Mwenyekiti wa CCM Marampaka Akutwa na Fuvu la Albino Pamoja na Viungo vya Mikono na Miguu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jeshi la polisi Mkoani Simiyu linamshikilia Chigila Gilala mkazi wa kijiji cha Bukigi kata ya Malampaka wilayani Maswa (45) kwa kosa la kukutwa na viungo zinavyodhaniwa kuwa vya binadamu likiwemo fuvu la kichwa.

Mtuhumiwa huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM katika kijiji hicho na Mganga wa tiba asili alikamatwa nyumbani kwake, baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa- alikuwa amewahifadhi majambazi kwa ajili kugangwa (kuzindikwa).

-Akitoa taarifa kwa waandishi wa kamanda wa -jeshi la polisi Mkoani Simiyu Gemini Mushy alieleza kuwa tukio hilo la kukamatwa kwa mwenyekiti huyo lilitokea Mei 9 mwaka huu -majira ya saa 11 jioni katika kijiji hicho.

Kamanda Mushy alisema kuwa askari wakiongozwa na mkuu wa upelelezi katika wilaya ya Maswa walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuwepo kwa majambazi nyumbani kwa mganga huyo, kuwa alikuwa amewahifadhi kwa ajili ya kuwazindika.

Alisema baada ya kupata taarifa hizo walifanya msako nyumbani kwa mwenyekiti huyo, ambapo- alibainisha kuwa walianza kufanya upekuzi ndani na nje ya nyumba.

“Wakati wakifanya upekuzi huo walikutana na mfuko wa sandarusi ukiwa chini ya lundo la kuni nje ya nyumba- ya mwenyekiti huyo..na katika mfuko huo kulipatikana fuvu la kichwa pamoja na mifupa ya mikono au miguu vinavyodhaniwa kuwa ni viungo vya binadamu” Alisema Mushy.

Kamanda alieleza kuwa jeshi hilo linaendelea kufanya uchunguzi kama kweli viungo hivyo ni vya binadamu na kama anahusika na uwepo wa viungo hivyo kutokana na -kukutwa nje ya nyumba yake.


Wakati huo huo kamanda Mushy alibainisha kuwa jeshi hilo linamshikilia- Gandula Mashimo mkazi wa kijiji cha Longalombogo kata ya Migato wilaya ya Itilima Mkoani hapa kwa kukutwa na Bunduki ya kivita SMG na risasi 273.

Alisema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa juzi majira ya saa 3:30 usiku kijijini hapo, akiwa embeba siraha hiyo pamoja na risasi katika mfuko wa sandarusi.

Alisema mtuhumiwa alikamatwa baada ya wananchi kutoa taarifa kwa jeshi la polisi wilayani humo, ambapo alikamatwa akiwa njiani kuelekea kusikojulikana.

-
Mushy alieleza kuwa uchunguzi unaendelea ili kubaini washirika wake, ikiwemo na matumizi ya silaha hiyo, huku akitoa wito kwa wananchi mkoani hapa kutoa taarifa za watu wanaowahisi kuwa siyo wema katika maeneo yao.

Aidha alitoa onyo kwa ambaye anamiliki silaha bila kibali rasmi, kuwa ajisalimishe pamoja na silaha yake mara moja kabla ya msako mkali kuanza.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Siku zote tunajua kuwa baadhi ya viongozi wa serikali na wanasiasa pamoja na matajiri wanahusika na mauaji ya Albino, lakini namna ya kuwapata ndio kazi kwani wanawalipa watu kufanya mauaji hayo,, ni lazima wanyongwe pia

    ReplyDelete

Top Post Ad