Mwigulu awaomba radhi wanafunzi elimu ya juu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

SIKU moja baada ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kile cha St Joseph vyote vya   Dar es Salaam kuanza mgomo kutokana na kukosa fedha za kujikimu, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amewaomba radhi.

 Nchemba aliomba radhi bungeni jana baada ya Mbunge wa Viti Maalum, Ester Bulaya (CCM) kuomba muongozo, akihoji sababu za Serikali kushindwa kupeleka fedha hizo vyuoni.

 “Mheshimiwa Spika, naomba nipewe mwongozo ni kwa sababu gani serikali imeshindwa kupeleka fedha huku ikijua wazi kwamba wanafunzi hao ni watoto wa masikini,

Katika taarifa yake, Nchemba alisema kutokana na kuchelewa huko aliwaomba radhi wanafunzi ambao wanasoma kwa kutegemea mkopo wa serikali huku akizitaka mamlaka husika kuhakikisha fedha hizo zinawafikia wanafunzi mara moja. Alisema  Hazina imekwisha kuidhinisha fedha hizo.

 “Juzi hazina ilikamilisha miamala ya fedha ambazo zinahitajika katika vyuo hivyo na mamlaka zinazohusika zilipaswa kufikisha fedha hizo jana kwa wahusika (wanafunzi),” alisema Nchemba na kuongeza:

 “Ni muda mrefu migomo haijatokea kutokana na ukweli kuwa mtiririko wa utoaji wa fedha haukuwa na matatizo. 

 “Hakuna hata wa kulikuza suala hili kwa sababu msingi wake ulikuwa ni wa halali lakini kwa sasa limepatiwa ufumbuzi,” alisisitiza.

 Kuchelewa kutolewa fedha hizo za mkopo kumesababisha wanafunzi wa vyuo hivyo kugoma kuanzia juzi  hadi watakapopewa fedha hizo za kujikimu.

Bulaya katika taarifa yake alisema wanafunzi zaidi 7,000 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) juzi waligoma kuingia darasani kwa sababu ya kukosa fedha za kujikimu huku wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo cha Mtakatifu Joseph kilicho Mbezi, Dar es Saam wakisimamishwa masomo.
Mwisho
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad