Nyumba ya Diamond Katika Hati Hati..Mafuriko Yaizengea ,Yazungukwa na Mifereji ya Maji ya Mvua

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MAFURIKO yanayotokea katika sehemu mbalimbali nchini kutokana na mvua  zinazoendelea kunyesha, yanaizengea nyumba ya nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Diamond Platnumz iliyopo Tegeta Madale, nje kidogo ya Jiji la Dar.

Kwa mujibu wa majirani wa staa huyo, nyumba hiyo imejengwa katika njia ya maji (mkondo), jambo ambalo hakulielewa hapo mwanzo, kwani ndiyo sababu kubwa iliyodondosha ukuta wa uzio wake muda mfupi baada ya Diamond kuhamia wiki kadhaa zilizopita.

Kabla ya ujenzi, kiwanja hiki kilikuwa na njia kuu mbili za maji ambazo wakati wa mvua, zilikuwa zinatiririsha maji kuelekea bondeni, lakini baada ya ujenzi, nguvu ya yale maji yakadondosha ukuta.

Sasa ukiacha ukuta uliobomoka mwanzoni, kuna njia nyingine ambayo inapitisha maji mengi zaidi ambayo inapita kwenye ukuta wake mwingine na tayari yameanza kuuchimba kwa chini. Mnaweza kuja kuangalia,” alisema jirani mmoja aliyekataa kutaja jina lake.

Waandishi wetu walifika nyumbani hapo na kumkuta fundi ujenzi akijaza kifusi nyuma ya ukuta uliovunjika mwanzo huku upande mwingine wa ukuta  maji yakionekana kutiririka kwa kasi.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad