Rais Wa Burundu "Apinduliwa"......Ndege Yake Jana Ilishindwa Kutua Burundi na Kuamua Kurudi Tanzania

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Nchini Burundi, aliyekua mkuu wa majeshi Jenerali Godefroid Niyombare ametangaza Jumatano Mei 13 kuwa rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza amepinduliwa madarakani.


Meja Generali Niyombareh alisema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza.
 
Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari alisema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa.
 
Wakati  Mapinduzi  hayo  yakitangazwa, Rais Nkurunziza alikuwa  nchini Tanzania kujumuika na viongozi wa kanda  ya Afrika Mashariki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu.

Baada  ya  tangazo  la  kupindulikwa  kwake, Rais  huyo  alipanda  ndege  kurejea  nchini  kwake  licha  ya  tangazo  la  kufungwa  kwa  mipaka  yote  na  viwanja  vya  ndege.

Kwa  mujibu  wa  taarifa  ya  BBC  asubuhi  hii  ya  mei  14, Ndege  ya  Rais  huyo  haikuweza  kutua  nchini  Burundi  na  badala  yake  ilirudi  tena  Tanzania  ambapo  mpaka  sasa  Rais  Nkurunzinza  yupo  jijini  Dar  es  Salaam- Tanzania

Rais kikwete alipohutubia waandishi wa habari Dar es Salaam akiandamana na Rais Nkurunzinza
Maafisa wa jeshi la Burundi wakisheherekea Barabarani Bujumbura
Raia wakisheherekea ''Mapinduzi''
Manuari za kijeshi zingali barabarani mjini Bujumbura
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Umoja ni nguvu. Hongoreni burundi, hawa maraisi wa africa bara hili wamekalia tamaa na ubinafsi ndio uliowajaaa, mrimpigia kura na mmetoa, ata kama alikuwa hataki kutoka, alitaka leta udiktata wake sasa mmemuweza

    ReplyDelete
  2. TAMAA NYINGI MBELE GIZA TOTOROOO!SASA UMEKUWA MKIMBIZI BONGO NAWASHANGAA NYINYI VIONGOZI HASA AFRIKA KWA KUNG'ANG'ANIA KUKAA MADARAKANI ILI WAWEZE KUJILIMBIKIA MALI WANAZOZIKIMBIZA KATIKA MABENKI YA ULAYA(WAZUNGU WANAFURAHIA SANA HUU UPAMBAVU KWANI MNAWATAJIRISHA WAO)KWA NINI MSIFUATE MFANO WA MWL.NYERERE WA KUJIUZULU MWENYWEWE BILA YA MLIO WA MTUTU?NA NYIE WENGINE MLIOPO MADARAKANI MJIFUNZE KUTOKANA NA HILI LILILIMTOKEA HUYU MWENZENU NA KUMBUKENI KUWA"WATU WAKITAKA HAKI ZAO WAPE USIPOWAPA KUNA SIKU WATAJICHUKULIA WENYEWEWE KWA NAMNA YEYOTE ILE WAIONAYO INAFAA KUPATA HAKI YAO IWE KWA MTUTU AU KWA AMANI BARE THIS IN YOUR GREEDY&FILTHY MINDS WEAKED POLITICIANS

    ReplyDelete
  3. Ndio akome kuwafanya wenzake wakimbizi

    ReplyDelete
  4. Safi sana na watanzania tungeweza kuking'oa CCM madarakani kwa njia hii mambo yangikuwa shwari.

    ReplyDelete
  5. Wabongo kamwe hawawezi, sababu wanatokana na UDONGO WA MWISHO yaani UDONGO ULIO BAKI...fundi mwashi akimaliza kujenga kuna udongo au mchanga huwa unabakia, hivyo hulazimika kuutumia katika kazi yoyote isiyo rasmi ili mradi usipotee bure. Wabongo wanajua KULA KULALA, UTASHI sifuri, UZALENDO sifuri, UPEO sifuri, HAKI ZAO hawajui , wana-enjoy BIA ZA BEI NAFUU na kupanda DALADALA bure. Hawatumikii wananchi ingawa wajiita wa wananchi. Upeo wao wa kuona umefunikwa na mikopo ya mashangingi, nyumba, posho za vikao nk wanajiona wako peponi

    ReplyDelete
  6. INSHALLAH kuna siku hao mafisadi wanaojiita CCM(CHUKUA CHAKO MAPEMA)Nao pia tamati yao itawadia watafunga virago vyao na kutokomea kabisa kutoka katika upeo wa Watanzania wanaoipenda na kuithamini nchi yao nzuri TANZANIA Amen

    ReplyDelete
  7. CCM TANGU LINI IKATOKA MADARAKANI HIVI NYIE AKIRI MUNAZO KWELI

    ReplyDelete
  8. Ushauri wa bure kwa mheshimiwa rais wa zamani Nkurunziza, usirudi tena burundi watakufanya hakuna maana tabu na vifo vinakuhusu, kumbuka Samueli Doe alifanywa nini.

    ReplyDelete
  9. NA WEWE MWENYE AKILI(NA SIYO "AKIRI"KAMA ULIVYOANDIKA)NA HIYO CCM YAKO HAMJUI KUWA KILA LENYE MWANZO HALIKOSI MWISHO?

    ReplyDelete

Top Post Ad