Uso Kwa Uso na Mke Wa Rafiki yangu Gesti

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wakuu weekend iliyopita nilimuaga mke wangu kuwa Nina semina nje ya dar kikazi maana hiyo ndo huwa mbinu yangu ya kwenda kwenye dhambi zangu kwa siku tatu NNE
Nilikua nime import mchepuko wangu kutoka arusha so nika check in kwenye hotel moja bagamoyo tukajipumzisha hapo alhamisi,Ijumaa, Jumamosi jumapili asubuhi tuka check out

Wakati nafunga mlango wa room nashtuka kumuona mke Wa Rafiki yangu akitoka Chumba mkabala na changu akiongozana na zee moja hivi nao wakifunga Chumba chao shemeji alitetemeka na kupata mshtuko mkubwa hadi yule Mzee kumuuliza kuna nini

Mchepuko wangu ulishatangulia kwenye gari nikamsalimia shemeji nikamwambia mm ndo na check out nilikua semina ya siku tatu ndo imeisha, akaitikia kwa kichwa tu,
Nikapiga hatua za haraka kwenda kwenye Gari ili asiuone mchepuko wangu ambao ulishatangulia kwenye gari

Jumatatu akanipigia simu mwenyewe akaniambia shemeji naomba unifichie siri sitarudia tena
Nikamwambia naomba tuongee baadae kwa sasa nipo busy

Mchana wake akanitumia meseji inasomeka hivi "" Shem naomba kama vipi tafuta sehemu nije tumalizane kiutu uzima and you stay silence forever "" naomba unijibu i can't afford to loose this marriage

Wakuu nipo njia panda, ingawa mm ni mzinzi na sina utakatifu lakini siwezi kutembea na mke Wa Rafiki yangu kipenzi tulieshibana miaka nenda miaka Rudi
Na nilishawahi kukaa kwake sana wakati sijapata kazi yy alianza kuja dar kabla yangu

Kwa sasa huyu jamaa yupo mkoani kikazi alihamishiwa huko mke alishindwa kumfuata kwa yy mwenyewe ana kazi hapa dar .

Jana kanitumia M-PESA laki tano ikisindikizwa na msg kuwa vipi shemeji lile suala letu umeamuaje ukimya wako unaniumiza.
Sikujibu kitu

Wakuu naomba muongozo wenu
Kweli nisimwambie Rafiki yangu kuhusu uzinzi Wa mkewe?

Na mm ndo nimepewa jukumu la kumuangalizia familia yake kwa mambo mbali mbali kwa kuwa yupo mbali

Nawasikiliza wakuu

By Montana
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kumbuka wewe mwenyewe hauko sahihi japokuwa hajakuona nawewe unamkosea mkeo jua ipo siku hataukimwambia rafiki yako na wewe mambo yako kama ulivo muona shemeji yako na wewe utaonwa nawengine, nijisi gani Mungu amekuonya wewe kupitia hilo tukio ushauri wangu muite faraga huyo mwanamke mwambie usaliti sio mzuri muonye asirudie tena pia mwambie huwezi mfanyia hivo rafiki yako ila umuhakikishie utamtunzia siri but asirudie kitendo hicho nadhani ameshajifunza kama ana akili ila na wewe ubadili tabia unavomfanyia mkeo sio vizuri nyie wote niwakosaji ila bahati yako wewe hujaonywa ukiendelea na yako yatawekwa wazi

    ReplyDelete
  2. Kwa maoni yangu mie huna haja ya kumsaliti rafiki yako, ila mwambie na kumhakikishia huyo shemeji yako mkwale kwamba hutasema mbona na hela kakupa si ndo rushwa yenyewe tayari hiyo.

    ReplyDelete
  3. Chuna ukisema utavunja ndoa utalaumiwa wache wavunje wenyewe

    ReplyDelete
  4. wewe nani kakusemea kwani, lakini pia huyo mke wa rafiki yako anakupenda

    ReplyDelete
  5. Mwambie tu mie na wewe ngoma droo hata mie nilikuwa pale na mchepuko wangu, ukinisemea umeniona Bagamoyo na mie ntakusemea.

    Duh ndio maana mvua za gharika kila siku haziishi kwa ajili yenu.

    ReplyDelete
  6. we kuwa mpole tu mbona na wewe hujaenda semina ulikuwa mchepukoni? akimwambia mkeo kaukuona hapo inakuwaje? na pesa yake mrudishie kwani na wewe ni mkosaji tu ukichukua hiyo pesa amini ipo siku na wewe utagharamia mara tatu ni bora ingekuwa kweli ulikuwa semina.

    ReplyDelete
  7. bola ukae tu kimya kwa sababu wanawake ni madelila unaweza ukasema alafu wakiwa uchi tuu unageukiwa wewe upo.

    ReplyDelete
  8. Gonga mzigo, then chuna mkuu

    ReplyDelete

Top Post Ad