Wema, Kajala Tena, Wakutana Laivu Club Wakiwa Bwiii..Wakwepeshwa Wasizichape

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MAJANGA! Wasanii wawili mahasimu katika tasnia ya filamu, Kajala Masanja na Wema Sepetu ‘Madam’ wametengeneza tena vichwa vya habari baada ya kukutana ndani ya klabu ya usiku ya Maisha iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita na kuzua minong’ono miongoni mwa wadau wengi wa burudani, Risasi Mchanganyiko linakupa hatua kwa hatua.
Msanii wa filamu Bongo,Kajala Masanja akifurahia jambo.
Matukio hayo tofauti kwa wasanii hayo yalitokea ndani na nje ya ukumbi huo katika shoo maalum ya kumchangia mke wa msanii Mabeste  Venus, Lisa Karl Fickenscher  iliyowakutanisha mastaa wengi wa ‘category’ mbalimbali.
SHUNGULI YAANZA VIZURI
Shughuli nzima ilionekana kwenda vizuri, isipokuwa mara chache ambako kulitokea vituo vya hapa na pale, ingawa vingi kati ya hivyo vilisababishwa na baadhi ya wahudhuriaji kuzidiwa na kilevi.
Kajala Masanja akiwa na bandeji kichwani baada ya kupigwa chupa.
WATENGANISHWA
Wakati flani ‘usiku mnene’, Kajala alijongea kwenye jukwaa maalum la waalikwa (V.I.P) kutoka kujichanganya kwa wadau, ambako pia alikuwa amekaa Madam aliyeonekana kuzidiwa na ‘kiburudisho’.
Akitambua wazi kuwa lolote lingeweza kutokea, Petit Man, mtu wa karibu wa Wema, alimshika mkono na kumtoa eneo hilo, lakini muigizaji huyo alipohoji sababu za kuondolewa ‘V.I.P’, aliambiwa kuwa hapakuwa sehemu salama kwa wakati huo. 
Wema Sepetu akiwa kwenye gari.
KAJALA NDANI YA NYUMBA
Kajala alionekana akijiachia kwa mapozi na ‘mihangaiko’ ya hapa na pale ikiwemo kucheza na kubadili vinywaji akiwa sanjari na marafiki zake.Wakati wote, msanii huyo alionekana mwenye furaha iliyoambatana  na tabasamu na vicheko vya mara kwa mara jambo lililotafsiriwa kama tayari alikuwa amepata kiburudisho cha kutosha.
Wema akiongea na mashabiki wake ndani ya klabu ya usiku ya Maisha iliyopo Masaki jijini Dar.
AKUTWA NA MKASA
Mapambazuko yalipoanza kulivamia anga, Kajala na ‘kampani’ yake walitawanyika lakini wakati wakiwa nje ghafla jamaa mmoja ambaye hakufahamika ‘aliwa-join’ na kuwachangamkia kusiko kwa kawaida huku wao wakionekana kutompa ushirikiano aliouhitaji.
AMSHIKA MAKALIO
Hata hivyo, jamaa huyo ‘alifika mbele’ zaidi kwa kumshika makalio Kajala ambaye alimnasa kibao. Katika kujibu mapigo, jamaa huyo alimpiga na chupa ya bia kichwani na kusababisha jeraha usoni.
Baada ya tukio hilo, marafiki wa pande zote mbili walijitahidi kutuliza hali ya hewa iliyochafuka na kila mmoja akaendelea na hamsini zake.
Akiwa katika pozi nje ya klabu Maisha.
WEMA SASA
Kwa upande wake, Wema ambaye alipaswa kuwa Msema Chochote (MC) wa hafla hiyo, alipanda jukwaani kwa kusaidiwa na watu kutokana na kuzidiwa na kinywaji kisichojulikana.Baada ya kupanda, muigizaji huyo nyota alishindwa kumudu kuendelea na ratiba, kwani alizungumza maneno yasiyoeleweka na hatimaye kuishia kuwasalimu mashabiki, kitu kilichoharibu shughuli hiyo kwa jumla.
Kajala akiwa Maisha Club kabla ya kujeruhiwa kwa chupa. 
ATOKA UKUMBINI NA GLASI
Baada ya kushuka jukwaani, mmoja wa wapambe wake wa muda mrefu, Petty Man alimshika mkono na kumsindikiza hadi nje, ambako akiwa ameshikilia glasi yake ya kinywaji, Wema aliingia nayo kwenye gari, kabla ya kumwaga kilichokuwemo ndani na kumpa mtu mmoja glasi hiyo ili airudishe ndani.
Wema akiondoka.
Mwandishi wetu alipotaka kujua sababu ya Wema kulewa na kushindwa kufanikisha jambo muhimu, alimtaka kumuacha kwani hakuwa na muda wa mahojiano.“Tafadhali sana (akilitaja jina la mwandishi), sihitaji mahojiano, hapa nimekuja kwenye starehe, naomba uniache,” alisema Wema huku akibamiza mlango wa gari kwa nguvu na kumtaka dereva wake (Petty Man) kuondoa gari.
KUTOKA KWA WADAU
Baadhi ya watu walioshuhudia matukio ya Wema na Kajala kwa nyakati tofauti, walisikika wakisema kuwa ni kama mkosi uliowakumba wawili hao marafiki wa zamani.“Hawa bwana wana matatizo sana, wote wamekutwa na majanga kwenye eneo moja, lakini nadhani hata matatizo yao yanachangiwa sana na bifu lisilokuwa na kichwa wala miguu, wajishushe na wasameheane,” alisikika akisema mdau mmoja.
GPL
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Eti wakwepeshwa wasizicha[e dah mwajua kuunda habari kweli poleni

    ReplyDelete
  2. Ivi inakuwaje MC analewa tilalila !!! Wema hana maendeleo yoyote asipo jirekebisha

    ReplyDelete
  3. Duh!!!Ni yale yale ukipanda magugu kwenye shamba lako usitegemee kuwa utakuja kuvuna mpunga

    ReplyDelete

Top Post Ad