google-site-verification: googleb0bc30c3e5fdb812.html Kwa Nini UKAWA Wameamua LOWASSA Awe Mgombea wao wa Urais??..... Tundu Lissu Amelijibu Swahi hili kwa Ufasaha Kabisa | UDAKU SPECIAL

Kwa Nini UKAWA Wameamua LOWASSA Awe Mgombea wao wa Urais??..... Tundu Lissu Amelijibu Swahi hili kwa Ufasaha Kabisa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kwa  Nini  UKAWA  Wameamua  LOWASSA  Awe  Mgombea  wao  wa  Urais??..... Tundu  Lissu  Amelijibu  Swahi  hili  kwa  Ufasaha  Kabisa  hapo  chni:

Edward Lowassa anajiunga na CHADEMA na atakuwa mgombea urais wa CHADEMA na wa UKAWA. Lowassa is perhaps the most controversial and divisive political figure in the country right now.

Na amekuwa hivyo kwa muda mrefu. Sisi CHADEMA tulimweka kwenye Orodha ya Mafisadi kutokana na kuhusika kwake na Kashfa ya Richmond mwaka 2007.

Kwa hiyo swali halali kabisa ambalo lazima tulijibu kwa ufasaha ni hili: kwa nini tumekubali, sio tu kumpokea kama mwanachama, bali kumpa heshima ya kuwa mgombea wetu wa urais.

Na kwa nini washirika wetu wa UKAWA nao wamemkubali kuwa mgombea wao wa urais??? Jibu ni kwamba tupo katika kipindi na mazingira ya kipekee ya kisiasa katika nchi yetu. Kwa mara ya kwanza katika historia yetu kama taifa, tunaona mfumo tawala ukipasuka vipande vipande.

Kwa mara ya kwanza tunaona CCM ikipasuka katikati. Na mtu aliyeipasua CCM na mfumo tawala ni Edward Lowassa. Sisi CHADEMA tumefanya kazi kubwa ya kujenga chama tangu 2010.

 Tuna wagombea wengi na bora katika majimbo mengi ya uchaguzi na ngazi ya madiwani kuliko ambavyo tumewahi kuwa nao kwa miaka yote ya nyuma. Hata hivyo, ni ukweli pia kwamba kuna maeneo mengi ya nchi ambako tuko dhaifu sana.

Kwa kuingia kwake CHADEMA na UKAWA, Lowassa anayaingiza maeneo hayo kwenye ulingo wa kisiasa and very much within our reach.

Na Lowassa ataiporomosha CCM kwa sababu ana nguvu kubwa ndani ya chama hicho kuliko mwanasiasa mwingine yeyote. Katika mazingira ya sasa ya kipekee, tunahitaji kuamua nani ni adui mkubwa zaidi wa nchi yetu na ustawi wake:Edward Lowassa mtuhumiwa wa ufisadi au CCM na mfumo tawala ambao unajenga mazingira yanayostawisha na kulinda ufisadi.??

Sisi Chadema na UKAWA tumeamua kuwa adui yetu mkubwa wa sasa na siku zote ni CCM na mfumo tawala.

Tumemkaribisha Edward Lowassa kwa sababu kuwepo kwake kutaharakisha kuiangamiza CCM na mfumo tawala. Tunaomba wananchi mtuelewe na kutuunga mkono.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Uchaguzi mwaka huuu mchezo wa kuigiza

    ReplyDelete
  2. kwaio adui wa UKAWA sio mafisadi wala wala rushwa!!? adui wa UKAWA sio viongozi wanaotumia uongozi wao kujitajirisha!? adui wao mkubwa ni CCM!!!!
    Duh! hilo jibu nalo limenishangaza!!
    Mimi nilidhani hawa UKAWA ndio tumaini letu kumbe nao njaa tu inawasumbua!! kwaio wanakubali kuongozwa na fisadi eti ili tu awawezeshe kuwafikia watu wengi!!! PUMBAVU!!

    ReplyDelete
  3. ".....CCM kuongelea ubaya wa Lowassa kwa sasa ni sawa na mtu kujichungulia nyeti zake...Chadema kuongelea uzuri wa Lowassa kwa sasa ni sawa na mtu kujitekenya na kucheka mwenyewe....Vyote vinahitaji uso usio na soni"-Edo kumwembe.

    ReplyDelete
  4. Pesa zitawaua na zimeshaua UKAWA wenu ikulu mtaisikiatu ndo mmjinyea kabisa poleni sanaaaa sijui mtasema nini kwa watanzania ili waelewe watanzania wa sasa sio wa zamani ni wakisasa zaidi lowasa hatuko tayari kudanganywa mmejikoroga

    ReplyDelete
  5. IT IS TRUE KUWA NI PIGO KUBWA KWA CCM KWA KIPINDI HIKI CHA LALA SALAMA.NI MATUMAINI YANGU WATANZANIA WATAJIFUNZA KITU HAPA.KUTAFUTA HAKI YAKO NI JAMBO LA MSINGI SANA NA UKIONEWA UKIKAA KIMYA NI DHAMBI KUBWA.HONGERA SANA LOWASSA FOR YOUR RELIABLE DECISION

    ReplyDelete
  6. Ccm ni sawa na UKIMWI

    ReplyDelete

Top Post Ad