WANA CCM NISIKILIZENI..!! Kama Mlimkata LOWASSA Kwa Maslahi ya Watu Wachache Kwa Kutumia Akili Ndogo Basi Mnalo na Kazi Mnayo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

WANA CCM NISIKILIZENI..!!
Nina ushauri kwa wana CCM wenzangu; Lowasa kuhamia CHADEMA msipaniki. Kama kweli tulimaanisha kuwa hafai, ana uchu wa madaraka, alikiuka kanuni na maadili ya chama, ni mwizi na tena ni fisadi basi inabidi tushangilie kuondoka kwake, kwani kuvuja kwa pakacha sio ndio nafuu ya mchukuzi? Ila kama tulimkata kwa maslahi ya watu wachache na ikiwa tulitumia akili ndogo kulikata jina lake basi itabidi tujilaumu wenyewe kwa lolote tusilolitarajia litakalotokea. Na tukiendelea kutumia akili ndogo za kudhani tutashinda kwa "magoli ya mikono", basi tunakwenda na maji mchana kweupe! Tukijidanganya kuwa matusi, kejeli, mipasho, maneno ya kwenye kanga na nyimbo za Komba kwamba zitabadilisha huu upepo, pia tutajikuta tunakuwa chama cha upinzani bila hata kujiandaa kisaikolojia. Mwana CCM utakuwa unajichanganya kuushambulia uamuzi wa Lowasa kuhamia CHADEMA kwa sababu kimsingi CCM yetu ilishabariki vijana kadhaa wamshambulie majukwaani ili aonekane hafai na hao vijana wakazawadiwa vyeo. Mtu tuliemuona hafai kwetu inatuuma nini akiondoka kwetu? Ukioa mke kisha ukamtuhumu mbele za watu kuwa ni mzinzi na mshirikina; kisha mkaachana na akaolewa na mume mwingine, unaanzaje kuhangaika nae tena huko alikoenda? Tuwaache wapiga kura waamue kama ni sisi CCM ama UKAWA. Hata Mh. Mwenyekiti JK alishasema kila mtu ana haki kuongoza hii nchi; tunategemea kushinda lakini haitakuwa ajabu UKAWA wakitwaa madaraka kutokana na makosa yetu kimkakati. Wana CCM tusipaniki, kukomaa kisiasa ni pamoja na kuhimili na kukubali usichotarajia!
Wenu,
Mfurukutwa wa Shina.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. safi saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa mfurukutwa name nakuunga mkono swaiba hakuna cha kupaniki wala kele tuuche tuu na kusubili matokeo na tuyakubali,,, CcM NINI TENA !!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. kula gwala mwanangu una akili sana yaani article yako imemaliza kitu,wewe kichwa sana.

    ReplyDelete
  3. JIamini kijana Magufuli yupo hayo maneno ya kupokelewa ukawa yasikutishe tupo gado sana

    ReplyDelete
  4. Muongo wewe, ccm hatuna watu kama wewe

    ReplyDelete
  5. wana ccm waoneshe demokrasia ya kweli na kutambua ukuaji wake.
    Wasianze kuzusha mambo ambayo walistahili kusema na kuyakemea since 2008 punde the white hair Mr.Edo alipojiuzulu uwaziri mkuu.Wana ccm wajiipange kwa uchaguzi tu.Kama Mr Edo ni mwizi iwaje mpaka leo hakuna aliyempeleka mahakaman?..Leo kawakimbia kwenda UKAWA mnatakakuwaambia watzee et jamaa ni fisadi.I say no mbona hamkuna kiongozi wanchi wala ccm tangu 2008 aliyesema ?
    Iachen na iruhusu demokrasia na siasa safi itawale tzee

    ReplyDelete
  6. well done Lowasa move on Sir.... the choice is yours .... welcome....

    ReplyDelete
  7. ccm hamna lolote wizi mtupu mna siri kubwa sana ndiyo maana mkaogopa kumpitisha lowasa mkijua atawafilisi mtaumbuka tu hakuna kinachoshidikana chini ya jua hili haki itatendeka tu mpooooooooooooooooo

    ReplyDelete
  8. Ccm lazima ijue mabadiliko ni lazima. Hata mafuriko ya urusi na Arab Springs hayakuzuilika. Waende wamwulize mmoja wa ma jirani zetu mfano Kenya: je KANU yuko wapi siku hizi

    ReplyDelete

Top Post Ad