LOWASSA Aahidi Kuishinda CCM Uchaguzi Mkuu 2015

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Waziri mkuu wa Zamani Edward  Lowassa  amewaahidi wafuasi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema pamoja na wale wa umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba 25 mwaka 2015.

Lowassa alisema hayo jana mara baada ya kukabidhiwa fomu ya kugombea urais kwa tiketi ya chama cha Demkorasia na Maendeleo ambayo itampa ridhaa ya kugombea urais kupitia umoja wa Katiba ya wananchi ukawa unaundwa na vyama vinne vya siasa nchini Tanzania ambavyo ni Chadema, NCCR-Mageuzi, Cuf na NLD.

Aidha, Lowassa aliyekabidhiwa fomu na Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe katika ofisi za Chadema makao makuu yaliyopo Kinondoni jijini Dar es salaam jana,alichangiwa kiasi kadhaa cha pesa kitakachomsaidia katika yake ya matumaini iliyofufukia Ukawa. Katika hafla hiyo  Lowassa aliongozana na Mkewe pamoja na wana familia na ndugu wengine mbalimbali.

Mwanasheria mkuu wa Chadema Tundu Lissu alisema kwamba  ili mgombea ameweze kuwania urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ni lazima awe mwanachama wa chama chochote cha Siasa nchini Tanzania, hivyo Lowassa ni mwanachama halali wa Chadema pia amechaguliwa na vikao mbalimbali vya kamati kuu ya chama hicho iliyoketi hadi usiku wa manane.

Uamuzi wa Lowassa kugombea Urais ulipokelewa kwa shangwe na umati wa wananchi uliohudhuria hafla hiyo makao makuu ya Chadema kinondoni jijini Dar es salaam.

Mwanasiasa huyo Mkongwe atapambana  na Mgombea kutoka chama cha Mapinduzi Dk.John Magufuli katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu utakaokuwa wa aina yake  mwaka huu wa 2015.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kaza mwendo mzee ila kazi ipo kutamka ni rahisi sana lowasa lakini mchakato wenyewe ndo ishu kubwa......

    ReplyDelete
  2. sasa kuweka picha ya kikwete na Lowasa maana yake ni nini?..au kikwete anamsaliti Magufuri?...Kila la kheri Magufuri

    ReplyDelete
  3. Hana sumu huyu.. Kama angekuwa slaa sawa..lakin huyu! Mwenye uchu na madaraka kimasrah binafs hamsumbui m2

    ReplyDelete

Top Post Ad