LOWASSA Amesikia Vilio vya Watanzania Kuhusu Babu Seya na Mashehe wa Kiislam Walioko Jela...

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Leo Jagwani Katika Uzinduzi wa Kampeni za Ukawa Lowassa Amewagusa Wengi baada ya Kuzungumzia Suala la Babu Seya ambaye yupo jela amefungwa kifungo cha Maisha yeye na mtoto wake ..Lowassa Amesema kuwa amesikia kilio cha wengi kutaka aachiwe huru hivyo atakapo ingia madarakani atalitazama swala hilo....
Pia Lowassa Ameongelea kuhusu Mashehe wa Kiislam ambao wako Mahabusu na wengine Jela nakusema kuwa atashughulikia endapo atapewa nafasi ya kuwa Rais.....
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

16 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hivi huyu Edo sera za UKAWA ni Babu Seya na mashehe walioko gerezani wamefungwa kwa ajili ya kupigania haki za watanzania au hasa nini walichofanya kiharakati kuwakomboa watanzania ndo wakatiwa jela ndo imekuwa tukose uongozi bora wa kuleta maendeleo sasa lazima wafunguliwe ili kupambana na ukombozi wakututoa kati ufisadi hichi ndio kilio cha wengi Edo nikuingia madarakani kupitia sera za kiania jamani wacheni jokes UKAWA mmeishiwa

    ReplyDelete
  2. Ni vigumu kuisimamisha nguvu ya UMMA. PIPOZ PAWA! HATA MAGUFULI ALIJISAHAU AKASEMA PIPOZ PAWA katika hotuba YAKE. Nafikiri anakubaliana na sera za ukawa sasa na huenda akaipigia KURA ukawa

    ReplyDelete
  3. LEO NDIO NIMEAMINI UPINZANI ZERO ,JAMANI MMEJIONEA .LEO .HIVI SERA YA LOWASSA NI KUMTOA BABU SEYA ,UAMSHO,NA KUMREJESHA BALALI .AMA KWELI LEO PUMBA ZIMEZIHIRIKA ,HALAFU ANAWAAMBIA WAPIGA KURA WAKE AMBAO YEYE ANAWAITA WANYONGE WAKAANGALIE SERA ZAKE KWENYE TOVUTI ,HAWA MABODABODA,HAWA MAMA NTILE ,HAWA MAKONDA .AMA KWELI AKUTUKANAE AKUCHAGULII TUSII .LOWASSA WEWE NI WA OVYO ,NA UMESIBITISHA LEO KWA UMMA WA WATANZANIA .NA RUDI KWA WEWE JUMA DUNI WEWE NDIO PUMBA KABISA .LOWASSA ANASEMA KIPAUMBELE CHAKE ELIMU BURE KUTOKA STANDARD ONE MPAKA CHUO KIKUUU NEVER IN THIS EARTH. NILIWASHANGAA SANA MLIPOITWA MALOFA MKAHAMAKI ,LEO LOWASSA KASIBITISHA WOTE MLIOENDA PALE NI MALOFA KWA AHADI ALIZOWAPA .ACHENI OYAOYA .SIKILIZENI SERA FANYENI MAAMUZI.SHAME ON YOU ALL MLIOKWENDA KUSIKILIZA UPUUZI

    ReplyDelete
  4. huyo lowassa anakuja kutuletea machafuko ,wacha niwarudishe kwenye historia .zanzibar tukishuhudia makanisa yakichomwa,wazungu kumwagiwa tindikali,machafuko ya mara kwa mara lakini baada ya hawa uamsho kukamatwa na kuletwa huku machafuko yameisha na hatusikii tena ,leo mpuuzi mmoja anasema atakuja kuwatoa ili wakaendelee kufanya matukio yao ya kigaidi .hawa uamshu ndio waliokuwa wakimtukana mwalimu nyerere na kusema ndio aliofanya watu wa zanzibar kuwa vile ,jamani lowassa atatupeleka katika machafuko .swala la babu seya jamani babu seya amekutwa na hatia .kama kweli lowassa anawapenda wale ,alikuwa ana uwezo wa kuwasimamia hata kuwa tafutia wanasheria wa kuwatetea ,kwa nini atake kuwatoa leo? huyu mzee amechanganyikiwa

    ReplyDelete
  5. msimlaumu Lowasa hawezi kusema sana anaugonjwa mbaya, ndo maana Sumaye anamsemea na anajua L. akianguka atachukua yeye, ni uchu wa madaraka huo.

    ReplyDelete
  6. Mnaona ukawa mliacha silaa ambaye anasela huyu jamaa vipi siku zote bado anaongelea wabalaji kuwatoa jela ndio sera ya chadema your joking

    ReplyDelete
  7. na bado ccm wooooooooooooote jamba che che enhe..kwa taarifa yako yule mzee na mwanae are innocent,ni mambo ya kugombea mwanamke na kiongozi tu hakuna la ziada,.kwanza wewe haikujii akilini awali waliwachukua yeye na familia yake yote kwa kosa la ubakaji is impossible.. ccM Ziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii..kudaddeki,,na fanaleki kifo hakina break...

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyo kiongozi alosababisha afungwe kwa jinsi mnavyosingizia issue za wanawake ingekuwa kweli leo wanaume nusu ya waliopo tz angekuwa amewafunga maana kila mwanamke mnasema wake lol.

      Delete
  8. Hivi wewe ulisoma au kwanini haulewi jaribu kufuata nini aliongea kuhusu speech yake kama haujasoma kaa kimya

    ReplyDelete
  9. Magufuli mbele kwa mbele, UKAWA hamna sela, wengne n vipofu walikuwa wanatakiwa sikia kutoka mdomoni kwako leo unawaambia watu wakaingia kwenye website wasome hao vipofu na wasio juwa hata hizo website aunataka wafanye nini? EDO huna mpya

    ReplyDelete
  10. Wewe ndio umeishiwa kwa ufinyu Wa kufikiri kama ulitazama pale jangwani vizuri hoja hizo zililetwa na wananchi wenyewe na walitaka kulisikia I'll ndipo raid akawahaidi atalishugulikia pia mpumbavu wewe hii nchi si ya udini au ukabila sawa wewe hao mashehe walifanya nini hasa kiasi chakutupwa jele bila sababu wanastahili kutendewa haki ikiwa muislamu mwenzao ambse nirais sasa hakuwajali wala kuwasikiliza ikiwa walisingiziwa ama la yeye alipenda kuwafurahisha anao wajua yeye uku akiacha watu magerezani wasio stahili sote tunajua babu sea alisingiziwa iweje rais kikwete asimsikilize na walimtumia ombi he unakumbuka alicho jibu kikwete wewe mbona mafisadi hawajatiwa ndani hadileo kiss nimatajiri au sea na hao mashehe wangekuwa matajiri wakubwa kama hao mafisadi wangefungwa soma Alana za nyakati sio kutuma comment za kihayawani uwo wote ni ukosefu Wa elimu kichwani nakuchangiwa na fikra duni itakuhusu mwaka huu ukawa mbeleeee

    ReplyDelete
  11. Kwa kweli sijaona watu wapotoshaji kama comments za mwanzo nashukuru kwa comment ya mwisho l

    ReplyDelete
  12. Lowassa na mwenzake ni uroho wa madaraka Tu..Kama kweli yeye na mwenzake Sumaye ni wakweli na wanataka mabadiliko ya ukweli,mbona hawakuhama CCM kabla ya Mchujo?Hao walipokuwa CCM,mbona hata Siku moja hawakupita mitaani na masokoni kuwatembelea walalahoi?kwani walalahoi wamezuka Leo? Watanzania mutafakari hayo..!!!!! Majuto ni Mjukuu.

    ReplyDelete
  13. Edward Lowasa pamoja na mambo mengine anapaswa kuzungumzia kuhusu haki za raia. Sote tunajua kuwa Tanzania ina wafunwa wengi sana, tena waliohukumiwa baada kuthibitika kisheria kuwa walifanya ukatili mkubwa wa kinyama. kwa nini Watanzania wanung'ukie kufungwa kwa Babu Seya kwa kiwango kikubwa namna hii? Si lazima mfungwa awe amelifanyia taifa jambo kubwa ndipo Wananchi na viongozi makini waweze kumpigania; Ni suala la HAKI za kila raia kulindwa ipasavyo. Watanzania tusiwe vipofu. Nani asiyejua kuwa kuna kesi ambazo hufunguliwa kwa shinikizo za kisiasa, na watu wengine wamefanya uhalifu mkubwa lakini hawaguswi kutokana na shinikizo za kisiasa. Watu wangapi wanalalamikiwa na Wananchi kutokana na tabia zao za kufanya uhalifu lakini hawaguswi kutokana na sababu za kisiasa? Sasa kwa miaka kumi wananchi wengi sana wananung'unika kuwa Babu Seya hakufungwa kwa haki, wamepuuzwa.Kwa nini waendelee kupuuzwa? Watapuuzwa namna hii hadi lini? Mimi sijui kilichotokea mpaka Babu Seya akafungwa, Lakini vilio hivi vya Watanzania, tena kwa miaka mingi,vinanifikirisha sana, vinanipa shauku ya kujua kulikoni. Natamani kuona jambo hili likipatiwa ufumbuzi. Kwa kweli sipati picha kabisa ikiwa itakuja kuthibitika kuwa Babu Seya alifungwa kwa kesi ya kutunga!

    ReplyDelete

Top Post Ad