Ray Aangua Kilio Ukumbini!..Kisa Mshindi wa TMT Kufanana na Kanumba..Kisa Kizima Hichi Hapa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

BONGE la soo! Katika hali ya kushangaza, msanii wa filamu Vicent Kigosi ‘Ray’ hivi karibuni alijikuta akiangua kilio ukumbini baada ya mshindi wa shindano la kusaka vipaji vya kuigiza kufananishwa na marehemu Steven Kanumba.

Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta, jijini Dar kulipokuwa na fainali za Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) ambapo washiriki 10 ndiyo walikuwa wakiwania kitita cha shilingi milioni 50.

Mara baada ya mshindi wa shindano hilo kutangazwa, ukumbi mzima ulizizima kwa kelele za furaha na kwenda kumpongeza Dennis Laswai aliyeibuka kidedea na wengi walikubaliana kuwa ni haki yake kutokana na kufanya vizuri.

Wakati mshindi na mashabiki wake wakiendelea kufurahia ushindi, kundi la vijana lilipanda jukwaani wakiwa wameshika fulana yenye picha ya marehemu Kanumba huku wakisema mrithi wake amepatikana.

Ndipo ghafla, Ray ambaye alikuwa na upinzani wa kisanii na muigizaji huyo, alipoanza kumwaga machozi hadharani na kujikuta amezungukwa na watu wakimshangaa.

“Jamani mrithi wa Kanumba amepatikana rasmi baada ya miaka mitatu kuishi bila yeye, sasa jembe limerejea tena, mama yetu hapaswi kuwa na simanzi kila siku,” kijana mmoja alisikika akisema huku akienda kumshika mkono mama Kanumba.

Hali ilikuwa mbaya zaidi kwa Ray baada ya mmoja wa vijana hao kumfuata na kumuonesha fulana hiyo ambapo alizidisha kilio kiasi cha wenzake kumfuata na kumtuliza ili awe katika hali ya kawaida.

Mtu mmoja ukumbini hapo alibeza kilio hicho, akisema hiyo yote ilitokana na kuzidisha ‘kiburudisho’ na wala haikuwa kwa sababu ya kummiss sana marehemu kwani hawakuwahi kuwa na ukaribu wa kiwango hicho.

“Ray hana lolote, pale amezidisha kiburudisho tu, hakuwa na mapenzi na Kanumba kiasi hicho mpaka leo hii alie vile, ni usanii tu hakuna lolote. Wapo watu wa kulizwa na kitu kama kile na si yeye, halafu Ray huwa hana ushirikiano mzuri na wasanii wenzie hasa wa kiume,” alisema mtu huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.

Kwa upande wake Ray alisema kilichomtoa machozi ni ukweli kwamba mshindi ana kipaji cha hali ya juu na yeye binafsi alipenda ushindi wake kiasi kwamba mawazo yake yalimfikisha mbali.

Imeandaliwa na Shani Ramadhani, Mayasa Mariwata na Musa Mateja.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad