JOHN MAGUFULI: Polisi Atakae ua Jambazi Hata Shtakiwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema serikali yake haitamshtaki askari polisi ikiwa ataua jambazi mwenye silaha.
Mgombea huyo alitoa ahadi hiyo jana katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye  uwanja wa Mashujaa, mjini Mtwara.
“Katika serikali yangu askari akimpiga jambazi mwenye silaha kwa risasi hashtakiwi. Kila mara (majambazi) wanavamia vituo vya polisi, mbona hawavamii kambi za jeshi, Jeshi la Kujenga Taifa au Ukonga FFU?, wanaona polisi wana nidhamu sasa wanawaonea na kuwaua,” alisema Magufuli.
Mgombea huyo wa urais wa CCM pia aliahidi kwamba ataboresha maslahi ya askari polisi ili wafanye kazi zao kwa ufanisi na wakiwa na furaha.
Kadhalika, aliahidi kuwa akichaguliwa kuwa Rais, atahakikisha makusanyo ya kodi kwa mwezi yanaongezeka mara mbili kutoka yanayokusanywa sasa ya Sh. bilioni 900 hadi Sh. tirioni 1.8.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Top Post Ad