Dr. Slaa Aanza Rasmi Kumpigia Kampeni Magufuli......Asema Lowassa Hafai Kuwa Rais

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Siku chache baada ya chama cha ACT-Wazalendo kutoa tamko rasmi kuwa hawataweza kumruhusu Dk. Wilbroad Slaa kupanda kwenye jukwaa lao kumnadi mgombea urais wa chama hicho kwa sababu za kiusalama, jana mwanasiasa huyo ameanza rasmi kumpigia kampeni mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli.

Akiongea jana kupitia Star TV , Dk. Slaa aliweka wazi mtazamo wake kuwa Dk. Magufuli ndiye anayefaa kuwa rais wa Tanzania kwa kulinganisha wote waliojitokeza kugombea nafasi hiyo.

Dk. Slaa alisema kuwa amengalia kigezo cha mtu anayeweza kupambana na ufisadi na amempa Dk. Magufuli asilimia 90 katika kigezo hicho.

“Ninasema sitamung’unya maneno, mimi nafikiri, baada ya kusikiliza mikutano michache ambayo nimeweza kusikiliza, na baada ya kuona clips mbalimbali kwa sababu siku hizi unaweza kuishi kwenye mwezi lakini ukapata taarifa ya kila mahali. Kwa hiyo mimi Napata taarifa kokote nilipo.

“Kwa kutazama yote hayo, mimi ambaye nimeendesha mapambano ya ufisadi ninatafuta rais ambaye atatuondoa kwenye ufisadi. Sasa aliyeniridhisha kwenye mapambano hayo baada ya kuona vigezo ni Magufuli. Sina njia nyingine ni lazima nichague mmoja. Na kumbuka tunapochagua rais hatuchagui vyama.. na haina maana kwamba mimi ni CCM, sina chama,

“Na tunapokwenda kwenye chumba cha kura tukumbuke tunamchagua kiongozi wa nchi, tusiangalie huyu ni wa chama gani. Je anatufaa au hatufai, anatufaa kwa nini. Kwenye vigezo vya rushwa, Magufuli nampa asilimia 90.”

Kadhalika, Dk. Slaa alieleza kuwa amekuwa akisikiliza sera za wagombea hao lakini anaona mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa anatoa hotuba isiyozidi dakika 10 bila kufafanua zaidi hivyo anaona hafai kuwa rais.

Dk. Slaa alitangaza kustaafu siasa baada ya kujiuzulu nafasi ya Ukatibu Mkuu wa Chadema na kuachana na chama hicho kwa kile alichokieleza kuwa ni hakuridhishwa na uamuzi wa chama chake hicho cha zamani kumpokea Edward Lowassa.

Hata hivyo, Dk. Slaa alikiri kuwa yeye ndiye aliyepeleka wazo la kumkaribisha Lowassa kwenye chama hicho baada ya jina lake kukatwa na CCM mjini Dodoma na kunyimwa nafasi ya kugombea urais.
 
Dk. Slaa alieleza kuwa wazo hilo alilitoa kwa Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, ambaye alimtaja kama ‘mshenga’.

Juzi, akiwa katika jimbo la Karatu, Dk. Magufuli alimsifia Dk. Slaa na kumuita mtu safi na shujaa.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

21 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. zeee zima kumbe hovyoooo, hela inamvua utu! c alisema ataachana na siasa huyu!! kumbe lafi tu!!! sasa alikuwa anawasema wenzake mafisadi kwanini, na yeye mwenyewe fisadi tu!! c limechukua hela za wananchi ili liongee hovyo!!

    ReplyDelete
  2. Ndo maana CCM walikwita shoga wewe dr slaa
    Na inawezekana kimada wako anajuwa mchezo mbaya
    Popobawa ndo maana hutoki kwake

    ReplyDelete
  3. Shoga hili lishau pokea mshiko CCM

    ReplyDelete
  4. Haki ya nani,baada ya kumaliza chuo nilikosa ajira lakini kulikuwa na fursa za kujiajiri,
    nilikopa bank sh.laki 2 tu napo ni baada ya kandika barua ipitie kwa mtendaji,sijui mwenyekiti wa mtaa,mara sijui lete hiki na kile kiasi kwamba kwa asiyekuwa na uvumilivu angeweza kukata tamaa,nilifanya walivyotaka nikapata mkopo,sasa hivi maisha yangu safiiiiiiii.Huwezi kuniambia chochote kuhusu CCM,(NINAIPENDA )na naamini huyu Dk.slaa yako anayokumbuka kuhusu Magufuli na ndio maana anamkubali.NI MAGUFULI TUUU MPAKA KIEWEKE.

    ReplyDelete
  5. Huyu Mzee anantangatanga bila msimamo!

    ReplyDelete
  6. MALAYA ANAWEZA KUWA MWANAUME,MALAYA ANAWEZA KUWA MWANAMKE.SLAA NI MALAYA WA KISIASA MWANAUME,TENA NI SHANGINGI YAANI DUME LILILOKUBUHU KWA UMALAYA.HAKUNA MTANZANIA MWENYE UFAHAMU WA SIASA ZA TANZANIA ASIYEJUA KWA SASA KUWA SLAA NI ,TENA CCM MKAKATI WA USHINDI.MUNGU YUPO PAMOJA NASI WANA MABADILIKO .SLAA KWA USALITI HUU YEYE NA MALAYA MWENZIWE JUA LITAWACHOMA,BARIDI ITAWAKAMATA,LAANA ITAWAFIKA NA MWISHO MSONGO WA MAWAZO NDIO UTAKAOWAFUNGIA KAZI.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Malaya shoga

      Delete
    2. Kama nihivyo basi ni kila sekta, dini, siasa, ndoa, mpaka kubeba mke wa mtu jamaa ni hatari.

      Delete
  7. Huo ndio ukweli wenyewe, Magufuli ni bora kuliko sio tu Lowasa, bali kwa wagombea wote 7.
    Mwaka huu CCM imelamba 'dume', ni mwendo wa ku'Magufulika tu.., USHINDI NI LAZIMA

    ReplyDelete
  8. Msema kweli ni mpenzi wa Mungu, Magufuli ndio mpango mzima

    ReplyDelete
  9. NJAA ITAMUUA HUYO , MBONA AMECHELEWA SASA

    ReplyDelete
  10. NAONA KAMA TAREHE 25 OCTOBA MBALI,YAANI NYWELE NYEUPE,MOYO MWEUPE NA,SAFARI YA IKULU NYEUPE.EDWARD NGOYAI LOWASSA DUME LA MADUME,KARIBU BABA UKAMATE DOLA.CHA KWANZA UFUFUE UCHUMI WETU,CHA PILI UTUKUMBUKE SISI MALOFA,CHA TATU IMARISHA UTENDAJI WA KAZI SERIKALINI TOKA ASILIMIA 20 YA SASA HADI ANGALAU KWA UCHACHE ASILIMIA 75 ILI TUKOMBOKE KIKWELI,CHA NNE MIKATABA YOTE YA KIKWETE TANGU 2005 IRUDI UPYA BUNGENI.ASANTE,NAITWA NANJELE KIUNGANI KALINJELE.

    ReplyDelete
  11. ukiona mpaka watoto wako wenyewe wanakudharau ujue umefika pabaya, huyu slaa watoto wake mwenyewe walikuja mbela ya umma na mama yao kumuumbua, ujue cyo mtu wa maana kabisa huyu!

    ReplyDelete
  12. DrSlaa wasukuma hawajui popobawa

    ReplyDelete
  13. ATUAMBIE BASI CCM MAGUFURI NA CCM YAKE WANAFAA KWA LIPI?

    ReplyDelete

  14. slaa ANA ROHO YA UASI, NDIO MAANA ALIASI KANISA NA KIOAPO CHA UCHUNGAJI (UPADRE) SS HATUMSHANGAI MAANA ANAROHO YA KUASI, KAASI FAMILIA, NA NDOA YAKE NA MKE WAKE WA KWANZA KAASI CCM KISHA CHADEMA SS KARUDI CCM. MZEE ASOKUWA NA BUSARA

    ReplyDelete

  15. Kuna watu respectable wenye CV zao za maana duniani…lakini walivyojihusisha na CCM wamechafua CV zao;
    Mfano;
    Getruda Mongela mwanamama aiyeongoza mkutano wa Beijing unajua kashfa za rushwa zilizokuja kumkumba
    Sospeter Muhongo-A respectable Journalist unajua Amefanya nini kwenye ESCROW
    Omar Nundu mtaalamu wa dunia wa usafiri wa anga unajua ni nini kimemtokea
    Prof Anna Tibaijuka mama aliyeongoza shirika la Umoja wa mataifa unajua nini kimemtokea
    Daudi Balali a respectable IMF and World Bank Economist unajua nini kimemtokea baada ya kujihusisha na CCM.
    Ukiachana na hao…Jakaya Kikwete wakati anaingia madarakani alikuwa mtu mchapa kazi…Katika wizara alizopita kabla ya hapo alikuwa mwadilifu na Mchapa kazi…alichaguliwa kwa 80% kumbuka….Nini kimetokea baada ya kuwa Ikulu?
    Benjamin Mkapa..Jembe la Nyerere aliingia kama mzee wa kazi ameondoka na kujimilikisha mgodi wa Kiwira.
    Magufuli anayegombea urais wa CCM Alishiriki kikamilifu katika kuuza nyumba za serikali….Ameshiriki kuiingiza hasara serikali majuzi kwenye kivuko ca kigamboni shs Bilioni 8…Kivuko hakina muda wa miezi mitano lakini hakifanyi kazi ….ameiingiza hasara serikali kwa maamuzi mabovu mengi aliyofanya.
    Ndio maana kwa tunaotazama mambo kwa umbali ni bora CCM ikakaa pembeni tuanze upya (Sio kwamba wapinzani ni wazuri sana)…Kutakuwa na maumivu ya miaka 5 lakini baada ya hapo tuta endelea kama taifa.
    Kama taifa inabidi tuweze kufanya maamuzi magumu kwa mustakabali wa vizazi vyetu vijavyo.
    Mfano kulikua na haja gani ya kumilikisha kampuni za wazungu gesi yetu kwa miaka 99…tena kwa mikataba ya siri…….
    Utakuwa kichaa kudahani magufuli ataipitia hio mikataba na kuifumua…You must be mad

    ReplyDelete
  16. SLAA NI SWETUWANI, NI WA MOTONI KWA USALITI KAMA YUDA ,NA MOTO HUO SASA ATAANZA KUUONA HAPA HAPA DUNIANI KABLA HAJAENDA AKHERA

    ReplyDelete

Top Post Ad