Faiza: Tuwe Tunahofu ya Mungu, Wanaomponda Lowassa na Ugonjwa Wake na Wema Kutopata Mtoto

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Saa nyingine ili uone uzito wajambo inabidi uvae viatu vya mwenzio- kwa kweli imefika wkt najisikia vibaya kuhusu kusoma ugonjwa wa LOWASA, watu wameona ndio fimbo ya kumchapia kuhusu ugonjwa wake kwa kweli sijisikii vizuri na sioni kama sawa

Pia katika pita pita huku insta nimeona Wema na mbwa na Zari na mtoto na maneno ya kashfa juu yake,  jamani watanzania mnamatatizo gani kuhusu maisha ya watu!

 Kwa nini unamsema vibaya mtu juu ya kilema chake ? Kwa nini usimsema mapungufu yake bila kumkashifu juu ya marazi au kilema ? Hii ni sawa kweli? .

Nakumbuka kuna wakati watu walinisema sana kuhusu ukimwi! Nikawa najiuliza hii ingekua kweli na ukimwi ingekuaje ningejisikiaje tena kuna watu walikua wana nitukana live ikiwemo na kumwambia mtu ambae niko kwenye mahusiano nae, hivi mnazani kuna mtu ameomba marazi kweli.

Nyinyi mnaosema watu kuhusu vilema vyao je mnajua mnawaweka watu kwenye wakati gani?, hivi unajua kwa kumuandama mtu unaweza ukamuua au kumuongezea matatizo na saa nyingine kuchukua hatua mbaya.

Unae msema mtu unataka kuwa sababu ya matatizo yake ? Kama ni hapana basi tafazalini jamani tusemane yote lkn sio kwa mambo kama marazi au ugumba au kilema- jamani kabla hujafa hujaumbika tumuogope MUNGU tuwe tunahofu ya MUNGU

Faiza Ally @faiza_ally on Instagram
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

13 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hapana!Wema sio mgumba,atazaa ni wakati tu haujafika,na hata kama ana ugumba tukumbuke kuzaa ni majaliwa.
    Mh. Lowasa kama ni mgonjwa tunamuombea na sidhani kama kuna mtu anabeza ugonjwa kwani ugonjwa hakuna anaeomba,ni Mungu ndio anampa mtu maradhi?????kama ndiyo,tukumbuke ni Mungu huyohuyo ndio kaumba madaktari na katufanya tujenge hospitali,kwa hiyo wagonjwa wanatakiwa wapumzike hospitali chini ya uangalizi wa madaktari.

    ReplyDelete
  2. Yaani fai katikasikuzote leo umeongea kitu cha muhimu sana na wapumbavu wanao zalilisha wenzao kanakwamba wenyewe nimalaika bilashaka watakuelewa mana unamgandamizaje mtu kisa mgonjwa au mgumba uku wewe ni binadamu uliyeumbwa na Mungu alie muumba unae mtukania kilema chake watanzania punguzeni midomo punguzeni ushabiki wakipumbavu uwezi jua litakalo kupata badae

    ReplyDelete
  3. URAIS NI KAZI AMBAYO INATAKA MTU MWENYE AFYA NJEMA,HILO NDIO WATU TULIO WENGI TUNATAKA,TUNAKWAZIKA TUNAPOMUONA RAIS MTARAJIWA ANAFANYA VITUKO VINAVYOTOKANA NA UGONJWA NA BADO ANAN'GAN'GANIA TUUUUUUUU.WEMA SIO MGUMBA,TENA UWE MWISHO WA KUMUITA WEMA MGUMBA,LOWASA MGONJWA,HOSPITALI TU NDIO INAMUHUSU KUEPUKANA NA HAYO YANAYOMTOKEA KILA MARA.

    ReplyDelete
  4. NAPE NAPE NAPE NAPE NAPE

    ReplyDelete
  5. TUNAFAHAMU KILA MTU NI MGONJWA MTARAJIWA NDIYO,LAKINI KWA LOWASSA WACHA WATU WAMSEME,KUNA LAZIMA YA KUWA RAIS WAKATI NI MGONJWA?KWA NINI ASINGEKUWA UKAWA KWA KUONGEZA NGUVU NA SIO KULAZIMISHA KUINGIA IKULU,ANATAKA NINI IKULU?NA SIDHANI KAMA WEWE HULIONI.

    ReplyDelete
  6. Tuna hofu ya Mungu na wala kusemea ukweli ugonjwa sio dhambi wala unyanyapaa.
    Luwasa mgonjwa,na hafai kuongoza watanzania kwa sasa hivi alivyo labda apone.
    Mungu atampa uzima kama ni chaguo lake,lakini ajitibu na kupumzika sio kuhangaika kiguu na njia.

    ReplyDelete
  7. Hapo umeongea Faiza, manake kuna watu wanajisahau sana utafikiri wana mkataba wa kuwa WAZIMA MILELE!! Hawajui kama SEKUNDE MOJA TU inambadilisha mtu mzima kuwa marehemu, kilema mgonjwa, nk. Na, wasijisahau kuwa MALIPO NI HAPA HAPA DUNIANI. Na wengine tumeshaona wameondoka kwa KAULI ZA KUMNYOOSHEA MTU KIDOLE kuwa ni mgonjwa ilhali ni jambo ambalo mtu hulitafuti ila unalipata pasi kujua.

    ReplyDelete
    Replies
    1. DUA LA KUKU HALIMPATI MWEWE BWANA WEE,UKWELI TUTASEMA HATA KAMA KUNA MAISHA BAADA YA UCHAGUZI.LOWASA ANATAKIWA APUMZIKE AANGALIE AFYA YAKE KWANZA.

      Delete
  8. Faiza kama unajisikia vibaya kusemwa ugonjwa wa lowasa,pole sana.
    Ila ukweli anatakiwa awe mzima kiafya,akiwa mgonjwa takuwa anafanyiwa kazi na watu wengine siku zote?ukizingatia ugonjwa alionao sio mafua au kuteguka mguu kwamba hauchukui muda kupona.Ikulu ni mahali pa mchapa kazi,
    bila afya njema huwezi kuchapa kazi.

    ReplyDelete
  9. Nakupenda wewe dada,sanasana ulipogundua kwamba kumbe nikifanya visivyo nawakwaza mashabiki wangu,ukabadili tabia,na kwa sasa nakupa asilimia 99.
    Ugonjwa sio kilema,tanzania yetu haibagui vilema na ndio maana tunaongozwa na vilema kwa kuwa wako waliolemaa wengi wanafanya kazi vyema.lowasa sio kilema ni mgonjwa.na usifananishe ya Wema na Lowasa au lowasa na yako wewe mwenyewe.Mtu unapoomba ajira unajihakikishia afya yako kwanza.Mungu ibariki TZ

    ReplyDelete
  10. TUNA HOFU YA MUNGU ILA TUNAJIULIZA KWA NINI HUYU ANAITAFUTA IKULU KWA NGUVU HIVI BILA KUJALI AFYA YAKE KWANZA?NA NI BAADA YA KUTEKETEZA MAPESA YAKE MENGI?IKULU KUNA NINI?KAMA KWELI ANA UCHUNGU NA WATANZANIA KWA NINI HAKUTOA SEHEMU YA UTAJIRI WAKE KUWASAIDIA HATA KUWEKA VISIMA HUKO KWAO?NIMESHTUKA!

    ReplyDelete
  11. Faiza, kajifunze tena kutamka au kuandika maneno ya kiswahili. Umeandika "unazani" badala ya "unadhani" na "marazi" badala ya "maradhi". Sikutegemea msanii anaweza kuandika hivyo

    ReplyDelete
  12. SEMENI YOTE LAKINI LOWASA NDIYE RAIS

    ReplyDelete

Top Post Ad