Msanii wa Nyimbo za Asili Mkoani Mwanza Ahukumiwa miaka 10 Jela kwA Kumiliki FISI Wawili Bila Kibali

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MAHAKAMA ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Misungwi, mkoani Mwanza, imemhukumu msanii wa ngoma za asili, Mng’ahwa Kazanza (42), kwenda jela miaka 10 kwa kosa la kumiliki fisi wawili na kuwatumia kwenye sanaa zake bila kibali.

Awali akisomewa mashtaka katika mahakama hiyo na Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Doroth Mgenyi, ilielezwa mahakamani hapo kuwa mnamo Septemba 28, mwaka huu, kwenye Kijiji cha Sisu wilayani Misungwi, majira ya saa 7:30 mchana, Mng’ahwa Kazanza (42) alikamatwa akiwa na fisi wawili wenye thamani ya Sh milioni 4.8.

Mara baada ya kusomewa mashtaka, msanii huyo alikiri kosa hilo na kudai alikuwa akiwatumia fisi hao katika sanaa zake bila kutambua kama ni kosa kuburudisha mashabiki wake kwa lengo la kuongeza kipato.

Kutokana na kukiri huko, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Ruth Mkisi, alimtia hatiani kwa kosa la kupatikana na nyara za Serikali kinyume cha sheria Na. 5 ya mwaka 2009 na kumhukumu kwenda jela miaka 10 au kulipa faini ya Sh 4,840,000 ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaomiliki nyara za Serikali kinyume cha sheria.

Msanii huyo alishindwa kulipa faini hiyo na hivyo kwenda jela kutumikia adhabu hiyo ya miaka 10.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Inashangaza sana waua tembo waiba twiga hawaguswi lakini mcheza na fisi anafungwa

    ReplyDelete
  2. Ndio maana watu awaitaki ccm wanyonge ndio wanaonewa juzi tu watu walikua wanasafilisha twiga akuna chochote kilichoongelewa aizidi wamekanusha pole Kaka mungu atakusaidia

    ReplyDelete
  3. Watu wanaouwa mnawaachia kiulaini lakini Kaka wa watu mnampa adhabu kubwa faini kubwa hiyo fain ingekwenda wapi wizi mtupu hakuna sheria kifungu wala nini wizi tu au angelipwa baba ake fisi na mama ake kwa kuibiwa watoto wao

    ReplyDelete
  4. you said it well brother, sheria kwa masikini tu matajiri wanapeta.

    ReplyDelete
  5. Pole sana kijana hiyo ndo Tanzania ikiwa mnyonge jela utakwenda ila wanao wasafilisha kila siku hawahukumiwi hata kidogo kimsingi tafuta wakiri ukate rufaaa huoo ni uonezi

    ReplyDelete
  6. Duuh mh Jaji hata km ungelikuwa ww ndio mama yao hao fisi yaani ww umuwazaa mwenyewe hao fisi basi sio miaka 10 jela, mh jaji sidhan km hyo hukumu inalingana na kosa la huyo baba wa watu jaribu kufikiria kabla hujatoa hukum, na ingekuwa Anna tibajuka alonunu mboga kwa milion 10 ungeweza kumfunga hata miez 10? Achen uonevu jaman

    ReplyDelete
  7. Duuh mh Jaji hata km ungelikuwa ww ndio mama yao hao fisi yaani ww umuwazaa mwenyewe hao fisi basi sio miaka 10 jela, mh jaji sidhan km hyo hukumu inalingana na kosa la huyo baba wa watu jaribu kufikiria kabla hujatoa hukum, na ingekuwa Anna tibajuka alonunu mboga kwa milion 10 ungeweza kumfunga hata miez 10? Achen uonevu jaman

    ReplyDelete

Top Post Ad