JE Unakichukuliaje Kitendo cha ZITTO KABWE Kubaki Bungeni Wakati Wabunge wa Upinzani Wote Wametoka Nje ?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

JE Unakichukuliaje Kitendo cha ZITTO KABWE Kubaki Bungeni Wakati Wabunge wa Upinzani Wote Wametoka Nje Kushinikiza Maalim Seif Atangazwe Mshindi wa Urais Zanzibar?
Toa Maoni yako

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

36 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. huyo anajulikana!! hilo c swali!!

    ReplyDelete
  2. Yule si mwanaccm. Hamuoni hata Jinsi ushindi wake ulivyokuwa rahisi wakati wabunge wengine wa CDM, CUF, NCCR wakilazimika kulinda kura zao na kupambana kweli kweli ili watangazwe.

    ZZK ni msaliti wa watanzania, hana Jipya

    ReplyDelete
  3. Hausiki na UKAWA! Angebaki Mbatia au Lissu ndo ungehoji kwanini!? Hivyo hawezi kuingilia mambo yasiyomhusu.

    ReplyDelete
  4. Kwani Zitto ni UKAWA?

    ReplyDelete
    Replies
    1. WALE WOTE WANAOTAFUTA AJIRA INGIA HAPA : http://newjobstz.blogspot.com/

      Delete
  5. Ukimuona mtu katika ugomvi wa (man to man) mtu kwa mtu yeye anakimbilia silaha ujuwe si mpiganaji ni mhalifu. Kukimbilia vurugu kwa ukawa badala ya kukaa na kupambana kwa hoja za msingi inaonesha jinsi gani walivyojiegemeza katika kutengeneza migogoro zaidi kuliko amani. Zito ni mweledi na mwenye nia ya dhati ya kuweka utaifa kwanza chama baadae.

    ReplyDelete
  6. ANA AKILI TIMAMU HIZO KENGE NDO TUMEZITUMA ZIKAPIGE KELELE BUNGENI, HUKO NDO KUTUWAKILISHA?

    ReplyDelete
  7. Ni sawa Tu, walitoka Ni ukawa na waliobaki Ni ccm.

    ReplyDelete
    Replies
    1. We hujui hata kutodautisha zitto ni ACT waliotoka ni CUF,NSSR,na CDM hao ni UKAWA kwahiyo zitto na chama chake wana utalatibu wao na hao wanao jiita UKAWA wanataratibu zao pia hivyo usilazimishe mtu aige ige tu ovyo mswahili alisema usiige kunya kwa tembo

      Delete
  8. ZITTO NDIYE ALIYESEMA ZANZIBAR HAKUNA RAISI, AU SIYO JAMANI? LEO HII AMESHAKUBALI ZANZIBAR KUNA RAISI AU....
    Check link hii ujue alichosema kuhusu uraisi zanzibar: http://niajetz.blogspot.com/2015/11/zitto-vs-president-of-zanzibar.html

    ReplyDelete
  9. Zito hana uzito mwache akae tu bungeni, anatimiza zile alama za unafiki

    ReplyDelete
  10. Ni kukua kisiasa tena anahekima ya hali ya juu amewatendea haki wananchi wa jimbo lake

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wazanzibari ni Watanzania. Inawabidi Watanzania wote kutatua tatizo la Zanzibar kwanza kabla ya kufanya chochote. Hamuwezi kulikwepa. Zito hawezi kuleta maendeleo Kigoma kama serikali inayumba. Ni upumbavu na ujinga mkubwa kujidanganya. He is a Hippocrates.

      Delete
  11. Watu mnashindwa kuelewa. Zito hana siasa za ukawa wala hashiriki vikao vya ukawa. Zito anachama chake na sera zake. Kukaa bungeni haimaanishi kwa anakubaliana na yanayotokea zanzibar. Kama msomi na pia mwanasiasa alishatoa mchango wake wa kimawazo na misimamo kuhusu uchaguzi wa zanzibar. Katimiza wajibu wake. Lkn hakuwahi kusema Kama aliyoyasema hajafanyiwa kazi eti atatoka bungeni. Zito c kiongozi wa migomo. Zito ni kiongozi wa hoja tena zenye maslahi mapana ya kitaifa. Kama wenyemamlaka wameamua kuukandamiza uchaguzi wa zenj wengine hata mngefanyeje ni shida tu. Mnaona leo police yote na magari ya kuwasha wamehamia dodoma. Eti kuwapiga wabunge. Hii inathibitisha ubabe wa watawala na viburi walivyonavyo. Wajibu wetu ni kusema hasa ktk mambo Muhimu kwa taifa. Ukawa ilifahamika wazi wangetoka hata si tu kwa sababu ya zanzibar, ingepatikana sababu nyingine. Mwacheni zito afanye kazi na wajibu wake. Na haina maana kumwita msaliti. Wasaliti kwenye siasa halieleweki.

    ReplyDelete
  12. Wananchi wakimchakua mbunge wanategemea atawatetea kwenye sera zoa,sio kukimbia na kutoka bungeni,inawapasa wabunge wazungumze matatizo ya watu waliowachagua,ikiwa wantoka bungeni ni waoga na mishahara wasipate.
    Msimbazy

    ReplyDelete
  13. Wachaga waliona uwezo wa zito kwenye chama ni tishio wakaamua kumtumua na kusambaza taarifa za usaliti. Mm namshauli hata mbatia angehamia tu chadema ili nccr wajijenge upya. Usaliti wa zito uko wapi. Hivi zito, slaa Ndo wakulinganishwa na edo au mbatia. Acheni mambo yenu ya kutafuta zito. Mlimtimua mlizani kaisha kisiasa. Zito ni jembe watanzania tunamtaka na atafika mbali na chama chake.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Simamia Taifa. Zanzibar ni sehemu ya Tanzania. Nyinyi msioona mbali na kujua madhara ya jambo hili. Hamtaweza kuelimika hata. Ni watu kama nyinyi tatizo na mzigo duniani. Hamna mapana. Narrow minded people.

      Delete
  14. Zito atoke nje ye kwani ukawa, SI walimfukuza cdm sasa kwanini Leo awaunge mkono ilhali yeye kkaingia bungeni kwa tiketi ya act na sio cdm na act haipo ukawa, safi Sana zito big up endelea kuwakilisha wanakigoma, shame on them wabunge wote waliotoka nje, wagome na posho basi, safi Sana ndugai umefanya kitendo cha kishujaa kuwatimua, hivyohivyo adi wanyooke

    ReplyDelete
  15. ZITTO ANA AKILI SIN SAWA NA HAO UKAWA WASIO NA AKILI

    ReplyDelete
  16. Ndugu sikuwa na nia ya kukujibu,ila hujaeleweka umetumia lugha gani.Fanya marudio ya ulichoandika kabla ya kupost.

    ReplyDelete
  17. LABDA AJE AONGEE YEYE MWENYEWE.NI WAZI BAHASHA NZITO IMETUMIKA.HII NI AIBU NA FEDHEHA KUBWA KWA ZITTO MBUNGE PEKEE WA ACT BUNGENI,CCM HAWAJACHOKA,WANANUNUA UTU NA HESHIMA BUNGENI WAMEMVUA NGUO ZITTO.PESA CHAFU ZA CCM BADO NI TATIZO ZINAGAWIWA KAMA NJUGU NA ZITTO KAMEZWA.AIBU,AIBU,AIBU,NI WIZI MTUPU,WIZI!

    ReplyDelete
  18. zitto maskini,kaelemewa na bahasha nono ya ccm,kajivua utu kwa pesa.kamkosea muumba wetu,adhabu ya wasaliti ni moto wa dunia na jehanamu.bahasha ya january na nape zimemtoa utu.fedheha,aibu,uchafu.

    ReplyDelete
  19. Ni mwana ccm kwa mlango wa nyuma

    ReplyDelete
  20. Nilichotaka kuongea ni hiki. Wazanzibari ni Watanzania. Bila wao hakuna Tanzania bali Tanganyika na Zanzibari. Sasa Watanzania tunapowadharau Wazanzibar, tunaposhindwa kupigania haki za wenzetu wa Zanzibar, Tunaposhindwa kufuata demokrasia, Tunapopindisha sheria makusudi na kuadhibu watu, Huu ni uonevu, huu ni uharamia, huu ni uhujumu, matumizi ya nguvu yanayoonekana wazi lazima Watanzania wote tuungane na kuyakataa pamoja. Sasa kama Raisi ni wa Muungano utatawala namna gani ikiwa hujali vilio vya wananchi. Utawapuuzaje ukitegemea uwe kiongozi. Je kama unamsimamo huru wako binafsi bila kupandikizwa na Raisi aliyeamua kukuachia mzigo si wako. Kwa nini usiukatE.kAMA ccM INANIA YA MABADILIKO KAMA ILIVYOSEMA Kabla ya uchaguzi. Je haya ndiyo hayo mabadiliko? hii ni misukosuko. Je kama Mlimwamini Magufuli kwa uchapa kazi, Je atachapaje kazi kwa kuigawa Tanzania? Kwa nini Watanzania kama binadamu mnashindwa kuwa na vionjo na kuumia kama mwenzio anaumia. Magufuli ameambatana na raisi aliyepita na kushindwa kumtangaza Raisi ambaye Wazanzibari kwa kutumia kura wamemchagua. Watanzania ni Wajinga kiasi gani kukubali kuburutwa na chama kongwe hata kwa bunduki na kukaa kimya. Ilibidi nchi nzima iiandamane kuwaunga mkono Wazanzibari. Nashangaa jinsi sisi watu wa bara tulivyo waoga, mbumbumbu, na ni mainfirio kutokuweza kusimama na kudai haki zetu.
    Inashangaza tunasifiwa kwa amani na mtu aliyepewa zawadi kwa kudumisha Amani kashindwa kuleta amani nyumbani kwake. Ni hawa mabwana wenye maslahi nchini wamembeba kuhifadhi maslahi ya wizi. Je huu ndio udemokrasia wanaouleta Tanzania? Je Watanzania hajui demokrasia ni nini. Je Kwa nini mnapiga kura, Kwa nini mmekubali vyama vingi kama chama gogo ni dictata.
    Na zitto simfahamu msimamo wa bwana huyu nduma kuwili mpiga kelele aliyebaki bungeni lakini alitoa kauli ya kumambia Magufuli amtamke raisi aliyeshinda. Kajibwedeka pale. Kijana ndumila kuwili ni huyu. Wazanzibari ni ndugu zetu, Kwa nini mnawaacha kama Wanyama.

    ReplyDelete
  21. Zito anateteya maslayi ya inchi siyo maslayi ya ukawa

    ReplyDelete
  22. Zitto si mtu wa kufuata mkumbo ana uelewa wahali ya juu amelinda heshima zake kuliko hao vibaka (ukawa) wangepingakwa hoja tungewaona sana wa maana lkn mpaka hapo mazombii

    ReplyDelete
  23. WEWE UNAYESEMA ZITTO KAPEWA BAHASHA NA CCM UNA UHAKUKA GANI WA UNACHOKIONGEA, NA MOTO HUO UTAWAWAKIA, MUNGU SIO WA KUCHEZEWA. MLITAKA KILA HATUA YA KUTATUA MGOGORO WA ZANZIBAR MUAMBIWE NYINYI KAMA NANI, WAKUBWA NDIO WANAJUA WAMEFIKIA WAPI KATIKA SWALA LA ZANZIBAR.

    ReplyDelete
    Replies
    1. SUALA LA ZANZIBAR NI LA WATANZANIA WOTE UKISEMA MKUBWA SIJUI UNAMLENGA NANI ?

      Delete
  24. Zito Kabwe anajitambua, hawezi kuingilia mambo yasiyo na maana. Zito anamuhitaji Magufuli kwa ajili ya jimbo lake, hata wafanye nini ni LAZIMA narudia LAZIMA wapeleke shida zao kwa serikali hiyohiyo kwa ajili ya majimbo yao. Sawa, ukawa wametoka......THEN WHAT??? Bunge liliendelea au halikuendelea???? WAJIPANGE UPYA.........HAPA KAZI TU

    ReplyDelete
    Replies
    1. KAMA SUALA KUBWA LA ZANZIBAR UNAONA HALINA MAANA NINA MASHAKA NA UPEO WAKO WA UELEWA WA MAMBO

      Delete
  25. Zitto anaelewa. Bunge ni chombo cha kutunga na kupitisha sheria. Na anaelewa kuwa serikali yetu Ina mihimili mitatu ambapo kila mhimili Una kazi yake. Mihimili mingine Ni chombo cha kusimamia utekelezwaji za sheria zilizotungwa na mhimili wa mwisho Ni chombo cha kutafsiri sheria inapokosewa. Akiwa mbunge aliyechaguliwa na wananchi wajibu wake Ni kufikisha kilio cha matatizo yetu watanzania ktk bunge letu ili yapatiwe ufumbuzi nasi tusonge mbele. Naamn ,kila mambo limo ndani ya sheria. Na kama Kuna mambo linaonekana kukandamiza wananchi kisheria, naamn ktk vikao vyao basi waliwasilishe ili hiyo sheria kandamizi ifanyiwe marekebisho au ifutwe. Ni kweli tunaiga mabunge ya nchi zingine. Lkn SI kila kitu Ni cha kuiga. Tusipojiangalia tutaiga hata sheria za kuruhusu ushoga na tutaona Ni hali yetu kuiga. Hii ya kuiga vurugu za mabunge ya nje, hamuoni ni kutufundisha ss tulioko majimboni tabia za ajabu ajabu? Unategemea nn kwa mtanzania ambaye atafanyiwa uhalifu? Adai haki yake kwa kukusanya wapendwa wake na kumfanyia vurugu? Mkumbuke wanaoliangalia bunge ni watanzania na kila binadamu Ana tafsiri tofauti kwa mambo analoliona mbele yake. Hilo ni bunge letu sisi. Wazanzibari wana bunge Lao. Na siku zote wamekuwa wakigombana na kuwekana sawa wenyewe. Waachieni matatizo Yao watayamaliza wenyewe. Hapo bungeni mmeenda kututetea sisi na kutuletea maendeleo wa tz. Kuna vyombo vingi kimataifa vyenye uwezo wa kusimamia migogoro ya Zanzibar endapo wazanzibar watashindwa kuitatua ki region.kuna OAU, UN, nk. Demokrasia zingine zitatuingiza kwenye tuvikundi twa kudai haki like Boko haram. Fanyeni tulichowatuma bungeni.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umeanza vzr lakin huku mwishoni nadhani hauko sawa mkuu, Zanzibar ni part ya Tanzania na ndio maana hata kabla ya JK kuondoka madarakani tulihitaji ashughulike na hili tatizo, kinachoendelea Zanzibar kila mtu anakijua, unaposema matatizo ya Znz watatue wenyewe hauko sawa kabisa. ccm wanapora ushindi kila mtu anaona kama kweli watz tunahitaji maendeleo ya taifa letu kiujumla tuacheni siasa za kivyama

      Delete
  26. mnao muunga mkono zito wote hamjielewi!! ndio nyie mliunga mkono JPM kuvamia muhimbili bila kujua source ya tatizo ni nini!! mkamkashifu alyetolewa kumbe mwisho wa siku tatizo ni hazina wanadaiwa bilioni saba!! na hili hajalipima kwa makini kumbukeni siku ile kulikuwa hakuna kuchangia hoja bali rais kuhutubia bunge, na wao walimpa masharti kuwa shein hasiende kwani siyo rais tena waznz muda wake umekwisha!!! na kama anaenda basi awe kama mgeni mualikwa asipewe itifaki za kirais, lakini bunge likampa itifaki za kirais ambazo zilitakiwa ziwe za Maalim!!! ndipo hapo ili kuonyesha dunia ccm inachofanya sicho ndio ukawa wakaamua kufanya vile walivyofanya. na ni haki kwani si walikuwa wanaonyesha hisia zao ni kiasi gani hawakubaliani na mambo yanavyoendelea nzn!!! sasa kosa lipo wapi hata muanze kuwaona hawafanyi kazi waliotumwa na wananchi!!???

    ReplyDelete
  27. Kuhusu swara la Zanzibar mh zitto mbona kishalitolea ufafanuzi we upo nchi gani? Tena alieleza kisheria na kikatiba ya Zanzibar

    ReplyDelete

Top Post Ad