Kasi ya Magufuli Yamzindua Usingizini Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.....Nae Awapiga Chini Mawaziri Wote Wenye Kashfa Za Ufisadi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Uhuru Kenyatta
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amefanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri na kuwapiga chini mawaziri wote ambao wizara zao zinakumbwa na kashfa za ufisadi.

Uamuzi wa Rais Kenyatta umekuja siku moja baada ya kutangaza ufisadi kama tishio la usalama wa kitaifa huku akiazimia kufanya mabadiliko makubwa kwenye ofisi ya Rais hivi karibuni.

Katika mabadiliko hayo, Kenyatta ameongeza pia idadi ya wizara kutoka 16 hadi 20 na kuongeza idara mpya chini ya wizara hiyo, kutoka idara 26 hadi 41 kwa kile alichoeleza kuwa ni kusaidia wizara kutekeleza majukumu yao bora zaidi.

Baadhi ya mawaziri walikuwa tayari wamekwisha jiondoa kwenye wizara zao kwa tuhuma za ufisadi huku wengine wakiwa na kesi za kujibu mahakamani.

Hivi karibuni, Waziri wa Ugatuzi, Anne Waiguru alikuwa wa mwisho kujiondoa kwenye wizara akiwa na kashfa zilizopata umaarufu zaidi kwa kipindi cha hivi karibuni za kununua kalamu moja kwa shilingi zaidi ya 200,000 za Tanzania.

Hata hivyo, Uhuru Kenyatta hakuwa na budi ya kuvunja baraza lake na kuunda upya kwa kuwa katiba ya nchi hiyo inataka idadi ya mawaziri isiwe chini ya 14. Baada ya Waiguru kujiuzulu nafasi ya uwaziri, baraza la mawaziri lilibaki na mawaziri 13 pekee.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kichwa cha habari na maelezo yaliyomo kwenye habari haviendani,poor mwandishi!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad