Kasi ya Rais Magufuli Yaibua Utata Kuhusu Home Shopping Centre Kufilisika Ghafla...

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwana masumbwi wa Marekani aitwaye Joe Louis aliwahi kusema, ''He can run, but he can't hide''.

Kitendo cha Rais wa Tanzania na Waziri Mkuu wake, Majaliwa Kassim Majaliwa kuigusa kiutaratibu na kisheria Mamlaka ya Bandari na Mamlaka ya Mapato kimetoa picha kwa wachambuzi kuhusu kile ambacho kilikuwa kinafanyika kuhusu rushwa/ufisadi unaoendelea katika Mamlaka hizo.

Kufilisika kiusanii kwa kampuni kama Home Shopping Centre wakati Uchaguzi Mkuu umebakiza wiki moja haikuwa ajabu kutokana na hali halisi ya utendaji wa mamlaka za nchi lakini kinachostaajabisha kwa sasa ni jinsi ambavyo mamlaka ya nchi imekuwa ikifahamu wakwepa kodi kuanzia wakuu wake mpaka waendesha gari la mizigo inayobeba makontena ambayo hajalipiwa ushuru.

Nimeshangazwa kusikia taasisi ya Rais Magufuli imedadavua mpaka kufahamu idadi ya makontena ambayo yameingia mitaani bila kulipiwa ushuru. Mshangao huu umenifanya kuangalia nyuma na kugundua kuna kampuni ambayo ilifilisika ghafla bila maelezo ya kutosha kisheria!

Tunafahamu there is no time limit for commencing proceedings for an indictable offence. Ninafahamu serikali inaendeshwa na principle inayosema, one is considered innocent unless proven guilty lakini hii haiwezi kutufanya tusipate mashaka kuhusu kufilisika kisanii kwa Home Shopping Centre na pia hakuwezi kuizuia serikali kupekuwa vitabu vyao hata kwa njia ya Piercing the corporate veil ili kuhakikisha kama walifanya biashara ndani ya taratibu na sheria za nchi.

Rais Mkapa aliwahi kusema, serikali ina mkono mrefu katika kazi zake. Natumaini serikali ya Rais Magufuli itawatendea haki watanzania wote katika msingi unaosema, you can run, but you can't hide.

Is Home Shopping Centre owner of one of 349 lost containers?

Majipu lazima yatumbuliwe!

By MsemajiUkweli/Jamii Forums
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Msoga hiyo
    Nina majina ya wauza unga hadi kaondoka nayo
    Fyuuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  2. Tushazoea kuona baadhi ya Viongozi wakuu wanapoteuliwa huwa na speed 120 lkn baada ya muda mchace hujisahau kabisa!

    Kikwete alipoingia madarakani alianza vizuri kuwashughulikia Majambazi sugu lkn baada ya muda mdogo tu sifa zilivyomjaalia alijisahau, kwahiyo sitoshangaa na huyu JPM ni povu la soda subirini aone utamu wa madaraka na kujua kula na matajiri vizuri ataanza kujisahau na kauli mbiu yake HAPA KAZI TU na itakuwa HAPA KULA TU.

    ReplyDelete
    Replies
    1. USHINDWE NA ULEGEE MFYUUUUUUUUU

      Delete
  3. Muulizeni magufuli Mtu wake Dubai atavunja nazi

    ReplyDelete
  4. Tatizo ni mfumo wetu
    Chonde Chonde anzia ikulu futa futa
    , usalama wataifa toa toa
    Jeshini toa toa
    Police toa toa
    Utafanikiwa vinginevyo nguvu ya soda

    ReplyDelete

Top Post Ad