Mama Diamond Ambana Diamond Kuhusu Uhalali wa Mtoto Latiffah Katika Familia Yao..Mengi Yasemwa Mtaani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mama wa staa wa muziki Bongo, Sanura Kassim ‘Sandra’.SINEMA limeanza! Sanura Kassim ‘Sandra’ ni mama mzazi wa ‘kichaa’ wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ hivi karibuni anadaiwa kuingia katika figisufigisu na mwanaye huyo kwa kumuhoji kama kweli Latiffah ‘Tiffah’ ni damu yake kwa kumzaa na Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Amani limenyetishiwa.
Akizungumza na mwandishi wetu Jumatatu ya wiki hii, mmoja wa wanandugu wa Diamond alisema ishu hiyo ilijiri hivi karibuni nyumbani kwa Diamond, Madale jijini Dar ambapo mama na mwana hao walikuwa katika mazungumzo ya kawaida.

Ndipo, mama Diamond alipojikuta akiponyokwa na sentensi hiyo ya kuhoji uhalali wa Tiffah kuwa mtoto wa Diamond kauli ambayo awali ilichukuliwa kama utani wa bibi na mjukuu!

‘Kichaa’ wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.‘Yuda’ huyo wa Diamond, alizidi kusema kuwa, mama huyo alijikuta akimtaka Diamond aachane na wazo la kumhesabu Tiffah kama mwanaye kwani hafanani naye hata kidogo na kwamba ameuziwa mbuzi kwenye gunia kama si mfuko wa chumvi!

“Diamond alibadilika sura na kumtaka mama yake aachane na utani wa namna hiyo. Lakini mama alisisitiza kuwa si utani bali ni ukweli ambao amekuwa akivizia autoe kwa njia gani, hivyo siku hiyo aliona ndiyo muda mwafaka wa kutoa la moyoni.

“Kaka (mwandishi), ilibidi Diamond aondoke pale maana anampenda sana mama yake na huwa hapendi kumuudhi. Hivyo ili kuepusha mambo mengine, aliamua kwenda chumbani kwake. Lakini mama haikuishia hapo, alimfuata na kugonga mlango huku akisisitiza juu ya suala hilo.

“Sasa ninavyoongea na wewe, Diamond ana kama siku mbili au tatu hajaonekana nyumbani, anamkwepa mama yake maana naye amekomaa akimtaka mwanaye amuweke wazi anachofahamu kuhusu uhalali wa Tiffah kuwa damu yake,” alisema mtoa habari huyo ambaye ombi lake kubwa kwa mwandishi wetu ni hifadhi ya jina lake ili kuepuka kuonekana ni ‘kikulacho’ cha familia hiyo.
Kama kawaida ya gazeti hili, ambalo ni mashine bab’kubwa kwa habari za ndani za mastaa wa Bongo, kujiridhisha na kila habari kabla ya kuichapisha na kuipeleka kwa msomaji, ‘kiranja mkuu’ wa dawati alimtafuta mama huyo kupitia simu yake ya mkononi ambapo aliposomewa madai hayo mpaka mwisho, aliishia kusema:

“Jamani, kwanza mimi naumwa! Sitaki kabisa maswali magumu kiasi hicho cha kuumiza kichwa, niacheni na familia yangu,” (akakata simu na kuizima).
Amani lilimsaka Diamond mwenyewe kwa njia ya simu kwa kumtumia meseji na ilimfikia (deliva) lakini hakujibu kitu.
Agosti mwaka huu, Zari alimzalia Diamond mtoto huyo na kuibua hisia tofauti kutoka kwa wadau, hasa wa nchini Uganda ambako Zari ana asili nako, wakidai mtoto huyo si wa Diamond.
Hata hivyo, Diamod amekuwa akisema Tiffah ni mtoto wake na ana uhakika na hilo.
GPL
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

27 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Haya ya mtu Na mwanaye mmeyasikia wapi jamani

    ReplyDelete
  2. tulisema mwanzo mkajitia ooh tunamuonea wivu, ninii kikowapi? mpaka bi sandra kaanza kustuka.

    ReplyDelete
    Replies
    1. bibie we ni kama nani? Ulishaachwa pwaaa peleka njaa zako kwa waume za watu.

      Delete
  3. jamani huyo mtoto anafanana na katunzi na kidogo Zari mwenyewe, dai anajua ila anawaogopa maa x wake watamcheka.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ila ni kama wa baba yako mzazi kabisa, muuliza.

      Delete
    2. wanalijuwa hilo tatizo katunzi ni mme wa mtu,mwache dai alee lakini siku akichokwa tu na malaya zari siri inafichuliwa mtoto ni katunzi mtupi ila diamond ana force kuepuka aibu ya mwakaaaaaaaaaaaaaaaaa,Bi sandra kasema hivyo kuofia urithi wa nyumba kwenda kwa mtoto amabaye si damu yao.

      Delete
  4. PENNY ALISEMA KWELI. LOL. AIBU YA MWAKA.

    ReplyDelete
  5. angesema mwingine Domo yangemtoka matusi, sasa mama mazazi hana la kujibu imebidi akimbie nyumba.

    ReplyDelete
  6. mbona bado tutasikia mengi. wametukanwa sana Wema, joketi na penny

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wivu walijitanua hawakuzaa sasa kinawauma nini?

      Delete
  7. Du! na ile 40 ya mashauzi yoote, Dai anajitahidi kuwafumba watu macho? kumbe....

    ReplyDelete
    Replies
    1. Vipeeeee mapovu ulitaka amzalishe shangazi yako sasa?

      Delete
  8. KAMA TIFAA NI WAKE KWA NINI HATAKI KUMPIMA DNA? AKAMUONYESHA MAMA YAKE? KUNA NAMNA WALLAH.

    ReplyDelete
    Replies
    1. usiende mbali mama yako mwenyewe hiyo dna alipiga??

      Delete
    2. muulize kabisa yeye ana uhakika huyo anayemjua ni babaye ni babaye kweli? fyuuu kufuatilia ya wenzenu tu

      Delete
  9. kweli mtoto si wadai wengi wanajua. Almasi anajitahidi sana kuficha ukweli.

    ReplyDelete
  10. haya hayaaaaaaaaaaaaa, ngoma ikilia sana mwishoe hupasuka. Mama mzazi haeliwi elewi. Zari kafata jumba kafikiri atawaingiza mkenge family imeshastuka.

    ReplyDelete
  11. Yele mwanamke msaniii sana na hicho ndio kinamfanya atulie tuli South, unafanya mchezo na machale ya kina mama wewe. Yule mwanamke asinge kaa mwezi bila kurudi dar!!! lakini naona anaona mama mkwe kesha shitukia usanii wake duuu simchezo. But i kind like what she did lol maana wanaume wa bongo mmezidi. Ngoja mfundishwe adabu.

    ReplyDelete
  12. Huyu sijui Sandra mama Dai ni bora angechunga matamshi yasio na utashi na kuleta sintofahamu na mwanae je anataka Tiffa yane alelewe na mama yake kama vile yeye alivyo ziriwa Dai na baba yake akamlea pekee yake

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mwishowe tutamfikiria vibaya khaaa maana sasa siyo kisirani tena bali atazushiwa ana wivu wa kimapenzi.

      Delete
  13. Chizi kabisa nyie......inawahusu nini sasa hata kama kabambikiwa??!wivu tu umewajaaaa. Kapimeni dna na nyie hao baba zenu walibambikiwa tu sio baba zenu halali hata kidogo

    ReplyDelete
  14. Chizi mama yako alomzaa babu yako, hayawani weeee. mwenyewe Mama mzazi wa Bakuli kastuka itakuwa sie. wivu wa nini kwa mfano kuchangia dyudyu na kila demu mpaka kina Kajala? kapime wewe kwanza upate uhakika wa baba yako mzazi shwain Anony 10.33 AM.

    ReplyDelete
  15. Zari hana shida nyiye
    Ana kila kitu
    Si kina wema, kajala Na penny
    Zari gari kubwa dogo alikwenda pale kwa msuno

    ReplyDelete
    Replies
    1. acha uongo vyooote ni mali za ivan,sasa hivi hana kitu,ubishoo wa magari kama zamani kwishney

      Delete
  16. dna ndio jibu la yote haya jamani

    ReplyDelete
  17. NA NYIE KAPIMENI BASI DNA ZENU, MBONA KUWA WEPESI KUSEMA YA WENZENU MAMA SANDRA YEYE ANAJUA NINI DAI HUWA ANATOKA PEKE YAKE NA YEYE NDIE ANAJUA HATA KAMA MTOTO SIO WAKE YEYE SI ALEE MJUKUU MTOTO KAMKUBALI TATIZO NI NINI DUNIA HII BWANA WATOTO WENGI HAPA BABA ZAO SIO HAO WANAOWAJUA JAMANI KUWENI WAPOLE TU.

    ReplyDelete

Top Post Ad