Mambo Bado Zanzibar: Dr Shein na Maalim Seif Kukutana Tena Leo Kwa Mara Ya Tatu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mazungumzo ya kutafuta muafaka wa mgogoro wa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar, yataendelea kufanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar leo.

Mazungumzo ya kikao hicho ambacho ni cha tatu, kitaongozwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein.

Wajumbe wa kikao hicho ni Marais wastaafu wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour, Amani Abeid Karume, mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.

Mazungumzo hayo yanasubiriwa kwa hamu kubwa na wananchi baada ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec), kufuta matokeoi ya Uchaguzi Mkuu visiwani humu Oktoba 28, mwaka huuu na kuibua mgogoro mkubwa wa Kikatiba.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Nassor Ahmed Mazrui, amesema kuwa hadi sasa mazungumzo hayo bado siri kubwa hata viongozi wa ndani ya chama chake, hawafahamu kinachoendelea tangu viongozi hao wa kitaifa kuanza kukutana.

Amesema inasikitisha mno vikao vyote vitatu vilivyofanyika pamoja na hicho kinachotarajiwa kufanyika leo, upande mmoja unawakilishwa na watu watano wakati upande mwingine ukiwa na uwakilishi wa Maalim Seif peke yake.

Amedai kuwa mashariti yaliyowekwa katika muongozo wa mazungumzo, ni magumu kwa kuwa hakuna mtu mwingine anayeruhusiwa kushiriki katika mazungumzo ya kutafuta muafaka wa uchaguzi wa Zanzibar zaidi ya Maalim Seif pekee.

NAFASI ZA AJIRA>>WWW.AJIRAYAKO.COM
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Na-nyie hebu yamalizeni bana, hayaishi, kila siku nyie tu, msituchoshe, JPJM yupo bize na kuitengeneza Tanzania mpya, mumsamehe bure...HAPA KAZI TU

    ReplyDelete
  2. Aaah jp na western wote sawa c kwa sababu znz ni waislam

    ReplyDelete
  3. amieni tanganyika raisi awe mmoja jp m'fuli then huko zenji tufanye eneo la utalii na kilimo sidhani kama mpo wengi sana mnaweza wote mkatosha pale katavi kwa mizengo pinda, tupate kudumisha amani nahisi bila hivyo huo mgogoro hauishi leo. karibuni tanganyika.

    ReplyDelete

Top Post Ad