Mimba ya Jokate Yazua Balaa, Familia Yashtuka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kwani kimenuka? Siku chache baada ya kubumburuka kwa habari ya kunasa mimba ikimhusisha ‘mtoto mzuri’ Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ huku mhusika mkuu akitajwa kuwa ni msanii nguli wa Bongo Fleva, Ali Kiba, ishu hiyo imezua balaa kufuatia familia ya mrembo huyo kushtushwa na hali hiyo, Ijumaa Wikienda limenyetishiwa.

TWENDE OYSTERBAY
Mwishoni kwa wiki iliyopita, ‘kijumbe’ wa gazeti hili alitua getini nyumbani kwa akina Jokate, Oysterbay jijini Dar kwa lengo la kutaka kujua nini kinaendelea juu ya binti yao kunasa mimba nje ya ndoa ilihali familia hiyo inasifika kwa misingi bora na maadili ya kidini.

Gazeti hili lilipotia timu nyumbani hapo, lilifanikiwa kuzungumza na mmoja wa wanafamilia hiyo aliyekuwa nje akifanya usafi ambaye bila simile ‘alifunua kinywa’ na kuweka hadharani mambo mazito.

GAZETI LA IJUMAA LAIBUA MAMBO
Kama anayeogopa jambo fulani, memba huyo wa familia ya Jokate alisema kuwa, mrembo huyo alikuwa akifanya siri kubwa juu ya ujauzito wake huo, lakini baada ya gazeti pacha la hili, Ijumaa, kuibua habari hiyo, familia hiyo, hususan mama yake mzazi (jina lipo), alizua utata mkubwa kwa binti huyo na kwamba alishtushwa na hali hiyo na kumlazimu kumkalisha ‘kitako’ Jokate ampe ukweli.

“Jokate alikuwa akifanya siri sana, lakini ninyi mlipoandika habari hiyo, hapakutosha, mama yake alimuitisha kikao na baadhi ya ndugu wengine, lakini Jokate hakutaka kuweka wazi juu ya hali hiyo.

“Ninavyosikia, kuna uwezekano mkubwa wa Jokate kuhama hapa nyumbani akajitegemee ili kuififisha aibu hii kwani familia inadai amewatia aibu kwa kitendo chake cha kubeba mimba nje ya ndoa,” alidai mhusika huyo.

JOKATE ATOWEKA
Mnyetishaji wetu huyo aliendelea kudai kwamba, baada ya kuona anabanwa, alitoweka nyumbani hapo kwa siku mbili kabla ya kurejea na kuondoka kisha kurejea tena.

Kama kawaida ya gazeti hili kujiridhisha kwa kila habari kabla ya kuichapisha na kuwapelekea wasomaji wake, ‘kiranja mkuu’ wa dawati la Ijumaa Wikienda, mashine kubwa kwa habari za ndani za mastaa wa Kibongo, alimtafuta mrembo huyo kupitia simu ya mkononi na alipobaini kuwa mpigaji ni mwandishi wetu alishindwa kusema chochote zaidi ya kuiacha simu hewani na baadaye kuikata.

ATUMIWA SMS
Hata hivyo, ili kujizolea ushahidi madhubuti, mwanahabari wetu alimtumia ujumbe mfupi wa maandishi (sms) na kumsomea madai hayo, lakini hakujibu ujumbe huo licha ya simu ya mwandishi wetu kuonesha kuwa ujumbe ulikuwa umepokelewa (delivered).

KIBA KIMYAA
Pia, kwa upande wa Ali Kiba, simu yake ilionekana kutokuwa hewani muda mwingi, lakini mwandishi wetu alituma ujumbe wa kutaka kusikia chochote kutoka kwake ili akiiwasha simu akutane na ujumbe huo, lakini hadi gazeti hili linaenda kuchapishwa, hakuwa amejibu ujumbe huo achilia mbali kupiga simu hivyo jitihada zinaendelea.

Hata hivyo, mashabiki wa mastaa hao wameendelea kuwapongeza kwa namna ambavyo wamekuwa wakioneshana mahaba na kwamba suala la kupata mtoto ni jambo la heri bila kujali wamefunga ndoa au la.

Chanzo: GPL
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. MLIMKATALIWA ASIOLEWE NA NA ALI KIBA SASA KATIEA MIMBA

    ReplyDelete
  2. Familia ilikaa kimya kipindi cha mahusiano na Kiba leo hii mnapiga kelele kapewa mimba nani wa kulaumiwa hapo. Wazazi msichoke kujifunza,kutiwa aibu sio kuzaa nje ya ndoa tu hata mtoto kuwa malaya sio heshima vilevile..Tupa kuleeee

    ReplyDelete

Top Post Ad