Serikali Yakanusha Hazina Kuachwa Tupu Bila Fedha na Rais Kikwete

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Serikali imekanusha taarifa zinazosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa amekomba fedha hazina na kuiacha Serikali bila fungu lolote.

Hayo yamesemwa jijini dare es salaam na Kamishina wa Bajeti kutoka Wizara ya Fedha Bwa. John Cheyo huku akiwataka wananchi kupuuza habari hiyo kwani hazina ukweli wowote.

“Hazina inazo pesa za kutosha  na tunajivunia kufanya uchaguzi wa mwaka huu,  kununua mashine za BVR  kwa kutumia pesa za watanzania bila kutegemea msaada wowote kutoka nje ya nchi  na kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu mwaka huu” alisema Bwa. Cheyo.

Pia aliongeza kuwa serikali imeendelea kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa bomba la gesi ambalo limekamilika hivi karibuni, vinu vya kuchakata gesi na ujenzi wa barabara nchini.

Aliendelea kusema kwamba mfumo wa serikali wa bajeti unaiwezesha serikali kupanga vipaumbele vya matumizi kulingana na bajeti ilivyopangwa ambapo fedha zinazokusanywa kupitia mfuko mkuu wa serikali ndizo hutumika.

Bajeti iliyoidhinishwa na Bunge kwa kipindi cha 2015-2016 ni shilingi Trilioni 22.5 na bajeti hiyo inatengenezewa mpango wa makusanyo na matumizi kwa kulipia mishahara ya wafanyakazi na miradi mbalimbali iliyoidhinishwa.

Pia katika matumizi mengine bajeti hiyo inalipia chakula cha wanafunzi, mikopo ya wanafunzi elimu ya juu, ununuzi wa dawa na vifaa tiba na chakula cha hifadhi ya taifa
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Vasco da dagama
    Chezea wewe
    Bi salma chezea wewe
    Msoga Na lindi ikulu likuwa haitishi
    Wengine hadi mikocheni
    Hazina kutabaki kitu
    Magufuli ziara ya kwanza fedha alijua
    Chezea wakwere wewe kwa shughuli Na matanuzi

    ReplyDelete
  2. Model au president huyu
    Maakaji mengine fyuuuuuu
    Mikono hiyo fyuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  3. Hii Picha danga mtoto wa kiume
    Oooooooooops
    Fyuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  4. Kucha mtoto wa kiume mikono kwa pozi
    CCM hiyo
    Nape Na Makonda mpo

    ReplyDelete
  5. Pete vidole vya mwisho mtoto wa kiume
    Fyuuuuuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  6. sawa sawa kama hazina iliachwa ikiwa katika hali nzuri ya hifadhi na matumizi ya kawaida ya serikali kwa maana ya bajeti ya nchi,sisi wananchi tumeendelea kushitushwa na hii tabia mpya ya serikali na kufuta maadhimisho ya sikukuu za kitaifa kwa kuweka mbele hesabu ya matumizi yaliyopangwa na kamati hizi za sherehe.jambo hili ilikua ni jepesi sana.mheshimiwa rais kuikataa bajeti ya sherehe na kuagiza utaratibu huu muhimu sana wa kumbukumbu kubwa za matukio ya kihistoria ya nchi yetu uendelee yaani uwepo wake usivurugwe na utashi mwingineo.nina wasiwasi kuwa kwa mwenendo huu hakutakua na wiki ya utumishi wa umma,saba-saba na nane-nane.utata,utata,utata.

    ReplyDelete

Top Post Ad