Sijapenda Majibu ya Msanii wa Diamond Harmonize Kuhusu Mimi- Rose Ndauka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rose Ndauka
Msanii Rose Ndauka amesema kitendo cha msanii Harmonize kujibu majibu yenye utata alipokuwa akihojiwa na kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Televisio, hakupendezwa nacho kwani kinazidi kuleta sintofahamu.

Rose Ndauka ameyasema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba Harmonize alitakiwa kujibu moja kwamoja kuwa hawana mahusiano yoyote zaidi ya kufahamiana nae kikazi.

“Mi Harmonize namfahamu kama msanii, na hii issue sio mara ya kwanza, tayari nilishaona alihojiwa kwenye interview nyingine alihojiwa kuhusu mimi, what I didn't like ni kwamba angeongea straight, unajua kama huna mahusiano na mtu na ukaulizwa unaongea moja kwa moja, kitendo cha kutengeneza mazingira na watu wakaanza kuweka doubt kwamba Rose na Harmonize watakuwa na mahusiano, hicho ni kitu ambacho mimi sikukipenda”, alisema Rose Ndauka.

Rose Ndauka aliendelea kwa kusema kwamba yeye na Haronize hawana mahusiano kama ambavyo Harmonize alielezea, na kwamba iko tofauti na watu wanavyofikiria.

“The way alivyolijibu ilo suala kwamba mimi na yeye tunafahamiana kwamba naongea nae sana, mi na Harmonize hatuongei sana, na hata kama tunaongea labda Rose naomba nipostie hiki, sio kwamba ni mtu ambaye namfahamu sana au tuna mahusiano ya karibu sana, iko tofauti sana na yeye alivyojibu”, alisema Rose Ndauka.

Wiki iliyopita Harmonize alihojiwa kuhusu uhusiano wake na Rose Naduka kwenye kipindi cha Planet Bongo baada ya kuonekana wana ukaribu sana, na kutoa majibu ambayo yalileta sintofahamu kwa jamii.

EATV.TV
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. LABDA HARMONIZE ANAMTAKA ROSE, ILA ANASHINDWA KUMWAMBIA....NI UTOTO TU, AKIKUA ATAACHA

    ReplyDelete
  2. Tatizo la watoto hilo wanatafuta kiki

    ReplyDelete

Top Post Ad