Wachezaji Mbali Mbali Wajinyakulia Zawadi Katika Michuano ya Gofu ya Waitara

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mkurugenzi Mkuu (Mstaafu) wa Kampuni ya bia ya Serengeti Steve Ganon akizungumza kwenye hafla ya jioni kwa washiriki wa michuano ya gofu ya Waitara ambayo ilifanyika katika viwanja vya gofu vya Lugalo mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam. Michuano hiyo hudhaminiwa na Kampuni ya bia ya Serengeti ambayo hufanyika mara moja kila mwaka kwa madhumuni ya kuenzi mchango wa kimichezo wa Mkuu wa Majeshi (Mstaafu) Jenerali George Waitara kwa kuasisi uwanja wa gofu wa Lugalo golf club.


Mkurugenzi Mkuu (Mstaafu) wa Kampuni ya bia ya Serengeti Steve Ganon (kulia) akiwasilisha zawadi yake kwa Mkuu wa Majeshi (Mstaafu) Jenerali George Waitara (Kushoto). Aliyeshika zawadi hiyo ni balozi wa pombe kali ya Johnnie Walker Winfrida Kimario. Michuano hiyo hudhaminiwa na Kampuni ya bia ya Serengeti ambayo hufanyika mara moja kila mwaka kwa madhumuni ya kuenzi mchango wa kimichezo wa Mkuu wa Majeshi (Mstaafu) Jenerali George Waitara kwa kuasisi uwanja wa gofu wa Lugalo golf club.



Mshindi wa michuano ya gofu ya Waitara kwa wachezaji wakongwe wanawake Priscilla Karobia (Katikati) akikabidhiwa zawadi yake baada ya kuwapiku wenzake kwa mikwaju 82. Akikabidhi zawadi hiyo kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya (NIC) Dk. Edmund Mndolwa. Michuano hiyo hudhaminiwa na Kampuni ya bia ya Serengeti ambayo hufanyika mara moja kila mwaka kwa madhumuni ya kuenzi mchango wa kimichezo wa Mkuu wa Majeshi (Mstaafu) Jenerali George Waitara kwa kuasisi uwanja wa gofu wa Lugalo golf club.

Mkuu wa Majeshi (Mstaafu) Jenerali George Waitara (Kushoto) akipokea zawadi ya wiski ya Johnnie Walker (Platinum Label) iliyotolewa na Kampuni ya bia ya Serengeti katika kuthamini mchango wake kimichezo kwa kuasisi uwanja wa gofu wa Lugalo. Anayekabidhi zawadi hiyo ni balozi wa pombe kali ya Johnnie Walker Winfrida Kimario.

Mgeni rasmi wa michuano ya gofu ya Waitara Mhe. Jaji Mstaafu Mark Bomani (katikati) akikabidhi zawadi kwa mshindi wa pili wa jumla wa michuano ya gofu ya Waitara Bw. Michael Obare (wa kwanza kulia). Pamoja na Mgeni rasmi ni Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara(wa kwanza kushoto) na Meneja chapa wa vileo vikali wa Kampuni ya bia ya Serengeti Shomari Shija (wa pili kulia). Michuano ya gofu ya Waitara hudhaminiwa na Kampuni ya bia ya Serengeti na hufanyika mara moja kila mwaka kwa madhumuni ya kuenzi mchango wa kimichezo wa Mkuu wa Majeshi (Mstaafu) Jenerali George Waitara kwa kuasisi uwanja wa gofu wa Lugalo golf club.

Mshindi wa jumla wa michuano ya gofu ya Waitara George Nyakundi (katikati) akiwa na nyuso ya furaha baada ya kutangazwa rasmi kama mshindi wa jumla wa michuano hiyo ambapo alikabidhiwa kikombe pamoja na zawadi mbalimbali. (wa pili kushoto) ni Mgeni ramsi wa michuano hiyo Jaji (Mstaafu) Mark Bomani na (wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa majeshi (Mstaafu) George Waitara na wa kwanza kulia ni Meneja chapa wa pombe kali wa Kampuni ya bia ya Serengeti Shomari Shija. Michuano ya gofu ya Waitara hudhaminiwa na Kampuni ya bia ya Serengeti na hufanyika mara moja kila mwaka kwa madhumuni ya kuenzi mchango wa kimichezo wa Mkuu wa Majeshi (Mstaafu) Jenerali George Waitara kwa kuasisi uwanja wa gofu wa Lugalo golf club.

 Mshindi wa jumla wa michuano ya gofu ya Waitara George Nyakundi akionyesha zawadi yake ya kikombe mara baada ya kutangazwa rasmi kama mshindi wa jumla wa michuano hiyo iliyofanyika katika viwanja wa gofu vya Lugalo jijini Dar es salaam. (Kushoto) ni Mkuu wa majeshi (Mstaafu) George Waitara. Michuano ya gofu ya Waitara hudhaminiwa na Kampuni ya bia ya Serengeti na hufanyika mara moja kila mwaka kwa madhumuni ya kuenzi mchango wa kimichezo wa Mkuu wa Majeshi (Mstaafu) Jenerali George Waitara kwa kuasisi uwanja wa gofu wa Lugalo golf club.

Mkurugenzi Mkuu wa Abstrat Limited Abdallah Singano kutoka klabu ya (Gymkhana) Dar es salaam akishiriki kikamilifu katika michuano ya gofu ya Waitara ambayo yalifanyika katika viwanja vya gofu vya Lugalo jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. Michuano hiyo ambayo huandaliwa na kudhaminiwa na Kampuni ya bia ya Serengeti hufanyika mara moja kila mwaka kwa madhumuni ya kuenzi mchango wa kimichezo wa Mkuu wa Majeshi (Mstaafu) Jenerali George Waitara kwa kuasisi uwanja wa gofu wa Lugalo golf club.


Michuano ya gofu ya Waitara yanayodhaminiwa na Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia pombe yake kali ya Jonnie Walker imefana na kumalizika vizuri siku ya jumamosi ambapo MCHEZAJI George Nyakundi ameibuka mshindi wa jumla wa mashindano ya kila mwaka ya Kombe la Waitara yalilofanyika kwenye Viwanja vya gofu vya Klabu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo jijini Dar es Salaam.
Nyakundi anayecheza katika kiwango cha ubora wa mchezo wa gofu (handicap) 22 alionesha kiwango cha juu zaidi katika mashindano hayo kwa kupiga mikwaju nett 65 na kuwashinda wachezaji zaidi ya 118 waliokuwa wakiwania Kombe hilo.
Nafasi ya pili ya jumla ilikwenda kwa Michael Obare ambaye alichuana vikali na mshindi akirejea na mikwaju nett 66.
Akizungumza na waandishi wa habari waliofika katika viwanja hivyo, Meneja Chapa wa pombe kali wa kampuni ya bia ya Serengeti Shomari Shija alisema kuwa wamedhamini mashindano hayo kwa mara ya tano sasa ili kuendelea kuenzi heshima ya muasisi wa klabu hiyo Jenerali Mstaafu George Waitara.
Akitangaza matokeo ya washindi mbalimbali katika makundi tofauti Kapteni wa klabu ya gofu Lugalo Japhet Masai alisema katika kundi la wachezaji wa viwango vya Daraja A ambao ni wa kiwango cha juu katika mchezo huo mchezaji chipukizi Suleiman Kessy mwenye handicap 9 alishinda kwa kupiga mikwaju nett 69, Jumanne Ally handicap 8 alishika nafasi ya pili akiwa na mikwaju 70, wakati Juma Likuli mwenye handicap 8 alimaliza nafasi ya tatu akiwa na mikwaju 70 pia.
Mchezaji Nicolaus Chatanda handicap 11 alishinda kombe kwa wachezaji wa Daraja B akiwa na mikwaju 68, akifuatiwa na nahodha wa Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam, Akhil Yusufali handicap 16 akiwa na mikwaju 71 na Priscus Nyoni handicap 12 alishika nafasi ya tatu akiwa na mikwaju 72.
Kelvin Manuhwa handicap 19 alishinda kwa kundi la wachezaji wa Daraja C akiwa na mikwaju 72 na kufuatiwa na R. Rwiguza handicap 24 aliyepiga 74.
Kundi la wachezaji waandamizi wanaume kombe lilikwenda kwa Joseph Tairo handicap 13 mikwaju 73, nafasi ya pili alikuwa Jenerali Mstaafu Mirisho Sarakikya handicap 19 aliyepiga mikwaju 73 pia , wakati Edmund Mndolwa handicap 9 alipiga mikwaju 74 na kumaliza nafasi ya tatu.
Pricilla Karobia handicap 17 alishinda kwa upande wa wachezaji wakongwe wanawake akiwa na mikwaju 82 na Lina Nkya handicap 15 alishika nafasi ya pili baada ya kurejea na mikwaju 88.
Kwa upande wa kundi la wanawake Tayana William handicap 24 aliibuka mshindi kwa kupiga mikwaju 72, akifuatiwa na Vailet Peter handicap 13 akiwa na mikwaju 74 na Vicky Elias handicap 13 alishika nafasi ya tatu baada ya kurejea na mikwaju 76.
Mbali na wachezaji wa ridhaa mashindano hayo pia yalihusisha kundi la wachezaji wa kulipwa ambapo Geofrey Leverian alirejea na mikwaju 75 gross na kuibuka mshindi wa kundi hilo lililohusisha wachezaji 18. Nafasi ya pili na tatu ilikwenda kwa mchezaji mkongwe Mbwana Juma na Nuru Mollel waliopiga mikwaju 76 na 77.
Kwa upande wake muasisi wa michuano hiyo Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali George Waitara aliwashukuru washiriki wote kwa kuonyesha ni jinsi gani wameendelea kuthamini michuano hiyo na kuwataka kuendelea na moyo huo.
Waitara pia alitumia nafasi hiyo kuishukuru Kampuni ya bia ya Serengeti na kumpongeza Mkurugenzi Mkuu (mstaafu) wa Kampuni hiyo Bw. Steve Ganon ambaye mara zote hakusita kudhamini michuano hiyo na kuomba wadau wengine kuiga mfano huo.
Naye Mgeni rasmi wa michauano hiyo Jaji (Mstaafu) Mark Bomani alitoa changamoto ya wadau wa mchezo huo kushiriki katika kuongeza viwanja vingi zaidi vya mchezo huo huku akianisha maeneo kama Dodoma, Mwanza na Mbeya ambapo wadau hao wanaweza kuendeleza mchezo huo.
Mashindano ya gofu ya Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali George Waitara huandaliwa na kufanyika kila mwaka kwa madhumuni ya kuenzi mchango wake wa kimichezo nchini kwa kuasisi uwanja wa gofu wa Lugalo golf club. Uwanja huo ulianzishwa mwaka 2006 kwa mchango mkubwa uliotolewa na Jenerali mstaafu George Waitara kipindi alichokuwapo madarakani, pia kuendelezwa na Mkuu wa Majeshi aliyefuata na aliyeko madarakani kwa sasa Jenerali Davis Mwamunyange.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad