Zari wa Diamond na Mama Diamond ni Vita Kwa Kwenda Mbele....Mama Hamtaki Mkwe, Zari Atoa Masharti

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

NI vita! Baada ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwenda nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ kumwangukia mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari’ kufuatia kuwepo kwa figisufigisu kati yao huku mama wa msanii huyo, Sanura Kassim ‘Sandra’ akihusishwa, mazito yameibuka.

TUJIUNGE NA CHANZO
Habari kutoka chanzo cha ndani ya familia ya Diamond zinamwagika kwamba, Zari amekubali kuja Bongo lakini akatoa sharti: “Nakuja Bongo, Desemba 8, lakini mama (mama mkwe) aondoke pale nyumbani (Tegeta-Madale, Dar).”

ZARI ATIA NGUMU, AKUBALI
Chanzo hicho kilimwaga ‘ubuyu’ kwamba, awali Zari alimtilia ngumu Diamond lakini baadaye alikubali kurejesha amani kama ilivyokuwa zamani hivyo watakuja wote Bongo baada ya kujiachia vya kutoka huko Sauzi nyumbani kwa mwanadada huyo.


DIAMOND KICHEKO SAUZI
Kuhusu kuweka mambo sawa na kuwa atarejea Bongo na Zari na mtoto wao, Latiffah ‘Tiffah’, Diamond alilidokeza gazeti hili kwamba, sasa ni ‘full’ kicheko na anamshukuru Mungu kwa kufanikisha kufanya mambo kuwa kama mwanzoni.
Alitamba kuwa atatinga Bongo wiki hii au mapema wiki ijayo akiambatana na familia yake kwani kwa sasa wapo poa na hakuna manenomaneno tena.
“Nakuja na familia yangu. Kwa sasa tupo poa sana na maisha yanaendelea. Kiukweli huku South (Sauzi) tuna amani sana,” Diamond aliliambia gazeti hili wikiendi iliyopita.

TURUDI KWA CHANZO BONGO
Ilidaiwa kwamba, baada ya mama Diamond kusikia kuwa, mwanaye atarejea Bongo, Desemba 8, mwaka huu akiambatana na Zari alianza kuhaha kwa vile alishamtolea maneno makali akidai kuwa, mkwewe huyo alikuwa analeta uzungu kwenye familia yake.
“Unaambiwa ndugu wanapomuonesha mama Diamond picha za Zari akijiachia na Diamond na mtoto wao, Tiffah, anaamini kweli anaweza kuja Bongo jambo ambalo hataki kulisikia,” kilisema chanzo hicho.

MAMA DIAMOND KAMA MAGUFULI
Kufuatia hali hiyo ilitonywa kuwa, mama Diamond alifunguka kimipasho:
“Hata kama akija ataondoka kurudi kwao kama alivyokuja kwani ‘Hapa Kazi Tu’ kama ilivyo kauli mbiu ya Rais John Pombe Magufuli.”
Ili kupata mzani wa habari hiyo, mmoja wa vijumbe wetu alimtafuta mama Diamond kwa njia ya simu ambapo aliwaka mara tu baada ya kuulizwa ishu hiyo.
Katika majibu yake ya hasira, mama Diamond alisema haogopi lolote na yupo tayari kwa lolote.

MSIKIE MWENYEWE
“Siogopi chochote Zari kurudi hapa, kama atakuja, atakuwa amekuja kama alivyokuja mwanzoni na ataondoka hivyohivyo kama alivyoondoka awali.
“Sasa kwani nina hofu gani wakati niko nyumbani kwangu hapa? Watu watuache na waache unafiki wa kufuatilia mambo ya watu,” alisema mama D kisha akakata simu.

TUJIKUMBUSHE
Mapema baada ya Zari kujifungua mtoto wa Diamond, kuliibuka maneno ya mama mkwe huyo kutoelewana na mama Tiffah ambapo mara tu baada ya sherehe ya 40 ya mtoto huyo, Zari alitimka Bongo kwa maelezo kwamba hatarejea lakini sasa anaweza kuja kupambana tena na mama mkwe wake anayeonekana bado ana jambo moyoni.

Imeandikwa na Gladness Mallya, Mayasa Mariwata na Musa Mateja
GPL
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

27 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ondoka Mtu mzima ovyo
    Yamekushinda yako wewe Na wema wako
    Ffuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  2. Ondoka bibi Mtu mzima ovyo
    Una nini wewe yamekushinda yako kuwa Na mwanaume
    Kama unamtaka wema shangingi Malaya mwenzio
    Mwanao ananipedenda Zari
    Niache

    ReplyDelete
  3. Jamani Bi Sandra mwaache mwanaona akae na anaye mpenda, mbona uswahili hivyo? Let him be a man and raise his daughter grandma. Uswahili shida sana.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyu bi Sandra mpumbavu kama yule mwanae Esma alitemwa na Petit man. Waswahiliii. Shule 0.0%. Wanaishia kuzaa zaa na kuvuruga maisha ya watu. Sandra kkabayaa kakavuuu manina zake. Zee zima kazi kugombana na wakweze. Au zamani Dai alikuwa anaku*om*a.?? Unaona wivu kuchangia na zari??

      Delete
  4. wee mbwa kaa kimya bi Sandra hayajamshinda ndo maana Dai kawa staa.

    ReplyDelete
  5. YAMEMSHINDA NN BI SANDRA? KAMA NI NYUMBA ALIISIMAMI NA MWANAE KAKUA KWENYE MIKONO YAKE. LEO BI KIZEE ANATAKA KUJIFANYA TOO MUCH. MAMA GANI ATAKAEKUBALI.

    ReplyDelete
  6. Malaya wewe na ukoo wako Anony 2.51 PM. ukome kumtaja Wema hayamuusu ndo maana alimkataa kitambo Domo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Malaya Mimi
      Zari fyuuuuuuuuuuuu
      Sina shida wala Mimi mpira wakona
      Wanaume wote wanitaka duniani
      Pamoja Na paji la USO
      Wewe wema una nini
      Utafunga mbwa na kuku
      Chukuwa dna za mbwa na kuku Malaya mchanga wewe
      Hunipati kwa mvua wala jua wewe
      Fyuuuuuuuuuuuuuuuuuu
      Koma tena koma

      Delete
    2. Kila kukicha wema anamtaka domo
      Hata Malaya mwenzie kimambi wanamtaka domo

      Delete
    3. Mange
      Baba yake alikuwa muuza unga mkubwa
      Eti Leo mange ataja wauza unga Kinondoni
      Fyuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
      Mange wewe. Aliyekuwa Malaya Kinondoni

      Delete
    4. Kila kukicha wema anamtaka domo
      Hata Malaya mwenzie kimambi wanamtaka domo

      Delete
  7. Heee Bila bi Sandra angempenda Diamond wa Mbagala? Mxxxx

    ReplyDelete
  8. Ndoa kwa Ivan ilimshinda sababu hataki ndugu she is selfish. Mbona ndugu zake wanajimwaga?

    ReplyDelete
  9. Wema team
    Humpati wala kumfikia Zari
    Kwa sura hadi pesa

    ReplyDelete
  10. Wema hampati Zari kwa nini? lol pole majaalana, kwa sura gani alokuwanayo na komwe juu. ndo maana anangangani kwa mtoto wa miaka 25. na magari yalikuwa ya Ivana bibi wee! humuoi sasa amebaki kupiga picha za sebule.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wema hampati Zari kwa kuzaa.

      Delete
  11. Wema hana muda kabisaaa wa kutaka kufananishwa na bi kizee, ndo maana aliikataa offer ya kurudiana na Domo na akasema hawezi kurudi kwenye ukoo wa kiswahili. sasa anashida gani na utajiri wa magari ya Ivan. toa funza kichwani.

    ReplyDelete
  12. MASKINI UGONVI WA BI SANDRA NA BI KIZEE ZARI MNAMUGIZA NA WEMA? MNAHASIRAAAA. PANDENI JUU MKAZIBE.

    ReplyDelete
  13. Mange Wema juuuuuuuuuuuu. watu wanaweweseka, wamefungiwa kwa kichwa mdudu wamekuja huku. mnalo limewaganda.

    ReplyDelete
  14. ndio maana lowasa alisema kipaumbele cha kwanza elimu, kipaumbele cha pili elimu, kipaumbele cha tatu elimu. pasipo elimu ni giza totoro, ona sasa familia zisizo na shule zinavyojuta kwa kushindwa kutatua vitatizo vidogo sana....

    ReplyDelete
  15. Diamond angetafuta mwanamke wa age yake aoe atulie. Tena a very simple lady aachane na mastar uchwara

    ReplyDelete
  16. mama ni mama dai alijue hilo na Mungu kumjaalia bi Sandra kumzaa dai na kumlea kwa shida na raha mpk kuwa star na kupendwa na kila rika leo zari hampendi mama wa dai kw sababu hawana elimu? UKIPENDA BOGA UPENDE NA UA LAKE, lakini hili alilolitaka ni huyu dai kicheche sana angetafute mke wa rika yake ambaye ni kicheche mwenziwe wa hapa bongo akaoa na akaendelea na maisha kwa raha mustarehe tena wabongo ambao wanapenda familia za waume zao lakini ana misifa sijapata kuyaona zari ni mtu wa starehe na pesa only. angalia wazazi ni wazazi na pepo ipo chini ya nyayo ya mama zetu. unamtukanisha mama yako kwa mwanamke aliyeweza kuritadi

    ReplyDelete
  17. RUDINI KWENYE MADA.HAYAMUHUSU WEMA AU MUMEPATA SABABU ZA KUMTUKANA?

    ReplyDelete
  18. Hivi kipimo cha DNA hakitatatua mzozano wa mtoto na baba yake halali?ikiwa kinatatua kinachoogopewa ni nini ?

    ReplyDelete
  19. Nashangaaaa! kipimo kipo lakini Domo anajifanya hakijui.

    ReplyDelete
  20. wote hapo amuelewi siri ya bi sandra,hana hakika kama tiffah ni damu yao ndio maana siku hizi kama unafuatilia amuweki zari kwenye page yake,yule tiffa ni katunzi product hata katunzi aalijuwa hilo tatizo katunzi ni mme wa mtu,na huku daimond anaogopa fedheha ya utasa basi inajiridhisha ila dai mwenyewe hana hakika kama tiffa ni wake.tatizo la bi sandra ni state house,zari mjanja ana invest kila nchi,ile state house zari kaipigia maesabu,kwa tifa,bi sandra kastuka,eti hana hakika kama tifa ni wao.

    ReplyDelete
  21. hahaaaaaaaaaaa
    yani naona mambo mengi yanapita sana hapa ila yote ni familia ya Dai na Zari kukaa pamoja na kusuluhisha migogoro yao
    hakuna jipya chini ya jua

    ReplyDelete

Top Post Ad