Baba yake Diamond: Nililia Sana Kutoalikwa Kwenye Arobaini ya Tiffah

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Baba wa staa wa muziki Diamond Platnumz, Abdul Juma amesema hakuna siku alilia kwa uchungu kama siku ambayo mjukuu wake Tiffah alifanyiwa sherehe ya arobaini bila yeye kualikwa.

Akizungumza katika kipindi cha The Weekend Chat Show cha Clouds TV Jumamosi hii, Mzee Abdul alidai licha ya kuwa anawasiliana mara kwa mara na mama yake Diamond, lakini hakuwai kupewa taarifa yoyote kuhusu tukio hilo mpaka alivyoona picha kwenye magazeti.

“Hakuna kitu kiliniuma kama kufanyiwa shughuli kwa yule dogo bila kualikwa.” Alisema Mzee Abdul.

“Yaani nakumbuka nilipigiwa simu nikaambiwa baba mwanao amepata mtoto lakini sio siku ya arobaini, niliumia sana, nililia, nililia sana kutoalikwa kwenye arobaini. Mimi nachoomba (Mama Diamond) asinisahau, kuna kazi nilifanya mpaka akawa hapo,” aliongeza.

Katika hatua nyingine mzee huyo amemtaka Diamond kufanya kazi kwa bidii.

“Mimi nampenda sana, kama kuna baya niliwatendea wanisamehe, mzazi akosehi, pia aendelee kujituma zaidi,” alisema Mzee Abdul

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

17 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. atakualikaje na mtoto si wake? labda ungestukia issue.

    ReplyDelete
  2. mwanao anajiona tajiri, na mama yake hamwambii ukweli wa kuachana kwenu ya kuwa ulimfumania. labda anaona aibu.

    ReplyDelete
  3. siri zinatoka mzee Abdul aliroga mwanae awe staa, sasa wanampiga chenga. na kuachana kwao kumbe bi sandra aligawa nyapu. pole babu ndo dunia

    ReplyDelete
  4. HAHAAAAA. NICHEKE MIE. BABU ALIFANYA KAZI YA KUROGA ILI DOMO AWE TAJIRI SASA WAMEMSAHU. SIRI NJEEEEEEEEEEEEE.

    ReplyDelete
  5. TULIA MZEE ABDUL NA YEYE YATAMKUTA. TULISHA WAONA WENGI KAMA DAI.

    ReplyDelete
  6. Dai unanichekesha watu wanatafuta wazee Wao wewe unamtosa wako wee haya wee

    ReplyDelete
  7. Mayweather boxer WA marekani amemtafuta mama yk aliekua Drug User Na kumuokoa vp wewe mtoto WA kiungwana ulielelewa Na mama mwema anamtosa mzee wako mpaka anayatoa yt hivyo sivyo Kuna Leo hatujui kesho

    ReplyDelete
  8. Dah ninawAtoto wakiume najisikia vibaya Sana ,yote yamepita msamehe mtu mzima hatakiwi kulalamika Na wewe utafika age km Ile ya mzee wako

    ReplyDelete
  9. Wewe unaendika comment na kujijibu hapo juu umekosa kazi ya kufanya

    ReplyDelete
  10. Ni aibu tupu,kukataa wazazi kisa una mali

    ReplyDelete
  11. Toeni laana hizi hapa

    ReplyDelete
  12. Haituhusu sisi it's private matter we are feedup with his story
    Fuck fuck
    Akitaka umaarufu aanze na kutoa missada au harambee ya shughuli za maendeleo
    Siyo scandaly zake Na family yake
    Manager wake mbu mbu sana

    ReplyDelete
  13. Binadamu hatujakamilika, ndio maana tunakosea Sana Tu. Lakini kukosea kwako haimaanishi utengwe na jamii yako. Ni kweli ulimkosea mzazi mwenzio na mwanao, lakini haimaanishi wao Ni wakamilifu. Mungu alituwekea kusameheana Mara zote ili maisha yaende. Najua mzee unaumia lakini nakushauri achana nao. Mshukuru Mungy kwa kukupa wale wanaokupenda na kuzikubali kasoro zako. Hao ndio ndugu zako. Huyo mwanao akija kukusslimia mpokee asipokuja mshukuru mungu maisha yaendelee. Al islaamil nadhwiif.

    ReplyDelete
  14. Ndio fundisho mzee nyie wa baba washenzi Sana pale alikua anakuhitaji Kama baba ulikua wapi? Leo unaona amebarikiwa ndo unakumbuka Kama Ni mwanao? Miaka yote hiyo ulikua wapi kumuonesha mapendo yako hunajua huyo mtt aliteseka kiasi gani mpaka kufikia hapo? Sasa ka ukijua malipo Ni hapa hapa duniani Na Hilo ndua la kuku maneno yako hayata mpata mwanao. Utavuna hulicho panda. Baba

    ReplyDelete
  15. tetetetetet baba inauma hasa ukiona unahitaji msaada ambao unawezekana kupata bila tabu lkn kuna vigisu ulivyojiwekea wewe mwenyewe

    ReplyDelete
  16. mbegu ya Chuki uliipanda mwenyewe baba, pale ulipomuacha mwanao ahangaike na mamaye. Kama ungetengana na Mama yake na ukawa karibu na Mwanao yasingekufika haya. Je kama huyo Daimond asingekuwa na pesa na kama si jitihada zake na mama yake ungewatafuta au ungekuwa unawasanifu kwa mbaali. Tubu kwanza dhambi ya kutelekeza watoto ili Mungu afanye njia na uweze samehewa kweli. Hata hivyo kwani mtoto uliye naye ni Diamond tu? dili na hao wengine.

    ReplyDelete
  17. Ndo muache kuzaaa watoto bila kuwatunza mbuzi nyie........ugomvi wako na mkeo unasusaje kumuhudumia mtoto na kujifanya unakula ujana. haya sasa ujana umeisha maisha bado yamekaza na mtoto katusua maisha.......unataka nini??!!!kua mpole na shika adabu yako ukileta ukuda nakupotezea tu.....ita pains mama anakomaa na mtoto mwenyewe mwanaume anakula bata tu na vibint..........

    ReplyDelete

Top Post Ad